Ni lini Rais Samia ataanza ziara kusikiliza kero za Wananchi?

Hujui kazi za Rais wewe, ungefunga mdomo wako tu.
 
Alisema tumpe miezi minne ajipange.Sasa ndani ya Ofisi hata hajakaa sawa mmeanza kelele aje nje.Mwacheni Mama aweke sawa Kwanza Ofisi.Mkumbuke hii Ofisi hajakabidhiwa na Hayati,kwa hiyo kuna tofauti kati ya kukabidhiwa Ofisi na kuikuta Ofisi.Orientation Kwanza.
 
Tatizo tumekariri kwamba changamoto ni huku chini tu vijijini, Inamaana kwako wale wafanya biashara waliokwama mpakani na mahindi yao sio changamoto?,
Masikini hudhani yeye tu ndiye ana changamoto. Alafu kuna majitu yanafurahi kuwa wanyonge
 
Msiba uliisha siku ile shujaa wenu alifukiwa karibuni.Hizo nyingine zote baada ya hapo ni mbwembwe tu.
 
Kwanini mtu mwenye akili timamu, sio mlemavu pia una afya tele ukubali kujiita mnyonge?

Hii habari ya kujiita mnyonge siipendi.
Awamu hii watu wamekazana kufuta neno mnyonge. Mnyonge toka zama za Nyerere ilijulikana ni mtu asiye na kipato cha kuweza kujikimu kwa mahitaji yake muhimu. Mfano chakula milo mitatu, Elimu, afya na malazi.

Mnyonge si maumbile ya mwili ati kilema, hapana! Aweza kuwa kilema lakini kiuchumi yupo uzuri na anajitegemea.
Kulikataa ili neno wakataeni wazungu walio waita "Third world Countries" kataeni kuitwa " Stricken Poverty countries" kataeni kuitwa "nchi zenye teknolojia duni"

Wabongo wananifurahisha kisa Magufuli alipenda litumia hilo neno basi awamu hii utasikia nani ni mnyonge? Wakati wengi wao hata uwezo wa kujikimu wao na ndugu zao hawana. Ukweli haupingwi bali ukweli uleta suruhisho la kutafuta ufumbuzi wa tatizo.
 
Wapinzani wakichukua nchi kuna tatizo gani ?
Wapinzani sio watanzania wanaofanya kazi zao kihalali nchi hii???
 
mimi binafsi sielewi, kuna mambo yalikuwa yananifurahisha sana kwa mtangulizi yule hadi kufikia kupanga foleni na kumpigia kura yangu na wala sikujutia. Yale mambo yamekatika ghafla kiasi kwamba ukiniambia nipige kura leo naweza kugoma nikihisi napoteza muda. Yule jamaa alitugusa wengi sana katika staili yake ya kuongoza nchi. Kweli mwanaume ni KICHWA cha nchi
 
Tukubali tu awamu hii imekuja bahati mbaya, tujipange tena 2025 kumchagua raisi tunayemtaka. Magufuli ametufungulia njia we can now tell a good leader and the worse one, magu katuamsha usingizin
Yule kambale alale anapostahili.
 
Kwanj kuna mwananchi alimpigia kura mama?
 
Wewe ungekuwa unaelewa kazi za Rais ungetaka aende kutatau matatizo ya shule kukosa mashimo ya choo na migogoro ya ndoa za wanavijiji??
Hivi unaelewa maana ya raisi? Unaelewa kazi za raisi? , mnaanza kujikosha mapema kwa kuwa mshajua kaanza kuaribu
 
Watendaji wa vijiji/mitaa, madiwani, wabunge, wakuu wa wilaya na mikoa wote ni ccm nchi hii, hao wote hawawezi kupeleka kero za wananchi kwa rais mpaka rais aende? Halafu mnajisahau na kuleta propaganda mfu kuwa chini ya Magufuli ccm imeimarika sana. Sasa imeimarika nini kama hata kero za wananchi lazima rais azunguke kuzisikiliza mwenyewe? Au unataka yale maigizo ya Magufuli na huyu mama ayaige hivyo hivyo?
 
Wapinzani wakichukua nchi kuna tatizo gani ?
Wapinzani sio watanzania wanaofanya kazi zao kihalali nchi hii???
Sijapinga wapinzani kuchukua nchi. Ndiyo maana nikasema wapinzani watachukua nchi. Naomba usome uelewe. Ningepinga ningesema wapinzani wasichukue nchi. Elewa andiko.
 
Bora udaku wa mitandaoni kuliko Jiwe alikuwa 'anawatrepu' akina Nape, Kinana na January na pia alikuwa anasoma meseji za wasaidizi wake wakisutana.
Ila mama nae pamoja na majukumu yake ya kazi ila ana muda wa kufuatilia udaku wa mitandaoni kuliko hata ma jobless.
 
Imekuja kwa bahati mbaya ulikuwa hujasoma katiba inasemaje kuhusu Rais akifa? Au mlidhani ana guarantee ya kuumaliza urais wake kwa sababu ya pushups zake uchwara tu??
Tukubali tu awamu hii imekuja bahati mbaya, tujipange tena 2025 kumchagua raisi tunayemtaka. Magufuli ametufungulia njia we can now tell a good leader and the worse one, magu katuamsha usingizin
 
Kwanini mtu mwenye akili timamu, sio mlemavu pia una afya tele ukubali kujiita mnyonge?

Hii habari ya kujiita mnyonge siipendi.
Unaweza usijiite ila uhalisia ukawa wewe ni mnyonge ni sawa mwanamke anayejiuza hata asipojiita malaya ila uhalisia itabaki kuwa ni malaya.

Nafikiri sababu ya watu kukubali kujiita wanyonge pengine walijiona wanathaminiwa na kusikilizwa hali ya kuwa wao ni watu wa hali ya chini kitu ambacho pengine hakikuwahi kuwepo huko awamu za nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…