Ni lini Rais Samia ataanza ziara kusikiliza kero za Wananchi?

Ni lini Rais Samia ataanza ziara kusikiliza kero za Wananchi?

Akisema warumi ataonekana ana mdomo... hata msiba haujaisha vizur huyo kashaanza kukimbilia nchi za watu Sijui anatafuta nini

Magu alikua ana mapungufu yake ila ulikua unaona kabisa he was dedicated in serving the people of Tanzania, alikua na uchungu na nchi yake, ila huyu mama yupo kimaslahi, yani tutalia na kusaga meno had miaka minne iishe
Miaka 4? Unaota au? Mama ana miaka 14, so yaandae hayo meno yako vizuri.
 
Ila mama anasafiri sana,tangu aanze urais hajatulia kabisa sijui muda wa kufanya maamuzi sahihi anaupata sangapi,muda wa kufikiria changamoto za wananchi na namna za kuzitatua,hata muda wa Ibada na Mwenyezi Mungu anaupata kweli,kila leo safari,events....na ndo ameanza tu majukumu
Waswahili bhana!

Asipo safiri utasikia

Oooh tutajichanganya vipi na jumuiya ya kimataifa kama raisi asipotoka....

Oooh inabidi atoke tupate misaada....

Ooooh uwoni kikwete alitoka tukapata uwekezaji wa Dangote

Akisafiri utasikia

Raisi anatoka sana, safari zake hazina tija kwa taifa

Hivi anapata muda wa kuabudu kweli

Lini ataanza kusikiliza kero za wananchi

Hakuna jema kwa wananchi ukitoka maneno usipotoka maneno
 
Ila mama anasafiri sana,tangu aanze urais hajatulia kabisa sijui muda wa kufanya maamuzi sahihi anaupata sangapi,muda wa kufikiria changamoto za wananchi na namna za kuzitatua,hata muda wa Ibada na Mwenyezi Mungu anaupata kweli,kila leo safari,events....na ndo ameanza tu majukumu
Kwa hiyo hujui kwamba Rais ni taasisi! Safari ni sehemu ya majukumu yake, kuhusu ibada kwa Muslim mbona ni jambo la dakika chache tu!
 
Mnataka raisi aanze kutafuna mahindi na kunywa kahawa barabarani
 
Ubora wa kutoingilia faragha za watu kwa kuwa 'trepu" bila ridhaa yao. Udaku wa mitandaoni kila mtu anaruhusiwa kushiriki.
Kwani Magufuli asingeweka wazi kama anasoma hizo msg za watu wake wewe ungejua? Umekuja kuhusisha jambo ambalo hata haliendani na nilichozungumzia mimi, rais wa nchi anapata wapi muda wa kufuatilia udaku wa mitandaoni kushinda hata watu wasio na kazi za kufanya?
 
Kama mlichagua wabunge na madiwani bom imekula kwenu.
Rais anapata taarifa kuhusu wananchi wake kupitia wawakilishi wenu kwani si rahisi mtu mmoja amfikie kila mtu nchi nzima.

Jiwe maranyingi alifanya hivyo kwenye vijiji vya barabara ya Moro - Dom- Mwanza.,, akitokea Mwanza au akitokea Dodoma. Alikuwa ansababisha foleni kubwa barabarani hata ajari wakati mwingine.

Mama hataki kusababisha foleni kwenye barabara zetu hizo nyembamba ,,anaruka na jet smoothly.
Tujifunze kuwa serious na maisha yetu tunapochagua wawakilishi wetu. (Ondoa uchaguzi wa mwaka jana, najua hatukupata hiyo fursa.)
Hao viongozi wote wanamsaidia rais, sasa yeye anahakikisha vp kwamba watendaji wake wanafanya kazi vizuri au ndio hata wakimuongopea ni sawa tu?
 
Unaweza usijiite ila uhalisia ukawa wewe ni mnyonge ni sawa mwanamke anayejiuza hata asipojiita malaya ila uhalisia itabaki kuwa ni malaya.

Nafikiri sababu ya watu kukubali kujiita wanyonge pengine walijiona wanathaminiwa na kusikilizwa hali ya kuwa wao ni watu wa hali ya chini kitu ambacho pengine hakikuwahi kuwepo huko awamu za nyuma.
Huko kwenu ndio kuna hao wanyonge na wanawake malaya siwezi kukukatalia maana uhalisia unao wewe!
 
Hao uliowataja sio wakuwaamini japo wanakuwa ni wateule wako kama raisi!!!! Lakini mjuba alikuwa mpambanaji san aisee ile kuingia front mwenyewe sio mchezo na ndio ilileta heshima kwa watumishi wake... Ni vizuri mama nae akawa anatembea kuangalia watendaji wake wanafanya kama anavyoagiza au ndo somjo na wao
Sasa kazi ya wakuu wa mikoa, wilaya,watendaji wa kata,wabunge,TISS n.k itakuwa ni nini.

Kweli kichaa alifanikisha kuwabrainwash wapumbavu wengi.
 
Hao viongozi wote wanamsaidia rais, sasa yeye anahakikisha vp kwamba watendaji wake wanafanya kazi vizuri au ndio hata wakimuongopea ni sawa tu?
Ana mawaziri na wakuu wa mikoa na wilaya ,, hawa wote wanamwakilisha yeye.
 
Kwani huko kwenu hamna viongozi wa ngazi za chini?Unadhani kazi zao ni nini?mnataka kila kitu Afanye Raisi? Basi waondolewe ofisini abaki Raisi tu!
Walizoea zile za one man show,, nchi ikawa ianjiendea tu bila uelekeo.
 
Acha kuuliza maswali ya kitoto
Rais haitaji kutembelea kila kijiji kujua kama waziri anafanya kazi zake vizuri.Nchi inaendeshwa kwa mifumo na kama unahisi mfumo uliopo sio madhubuti dai katiba mpya na serikali za majimbo sio kutaka Rais akakague mashimo ya choo ya shule na convoy.
Hao viongozi wote wanamsaidia rais, sasa yeye anahakikisha vp kwamba watendaji wake wanafanya kazi vizuri au ndio hata wakimuongopea ni sawa tu?
 
Kama hawaaminiki kwa nini pesa za walipa kodi zinatumika kuwalipa.Hizo ofisi zao zifutwe kwa sababu hawana tija.
Mjuba hakuwa mpambanaji, alikuwa hajui wajibu wake mkubwa ni nini akaishia kuwa anafanya kazi za mwenyekiti wa kijiji na mkuu wa wilaya.
Hao uliowataja sio wakuwaamini japo wanakuwa ni wateule wako kama raisi!!!! Lakini mjuba alikuwa mpambanaji san aisee ile kuingia front mwenyewe sio mchezo na ndio ilileta heshima kwa watumishi wake... Ni vizuri mama nae akawa anatembea kuangalia watendaji wake wanafanya kama anavyoagiza au ndo somjo na wao
 
Tanzania ni kubwa mkuu wangu ukikaa tu officen huwezi kupata yote kwa usahihi...
Kama hawaaminiki kwa nini pesa za walipa kodi zinatumika kuwalipa.Hizo ofisi zao zifutwe kwa sababu hawana tija.
Mjuba hakuwa mpambanaji, alikuwa hajui wajibu wake mkubwa ni nini akaishia kuwa anafanya kazi za mwenyekiti wa kijiji na mkuu wa wilaya.
 
Paint it any color you want laki uozo utabaki kuwa uozo tu hivyo basi utaendelea kuitwa uozo, kutuletea fabricated stories kana kwamba hatuna ufahamu na historia ya tawala zilizopita alimradi tu mpate pa kumkandamiza rais wa awamu ya 6 haitasaidia chochote.
Bora sasa tuko kwenye phase ya utawala ambao hauna muelekeo wa kuuana, kutesana na kutekana hivyo basi hizo rubbish mletazo hazina mashiko.
Hii haina maana ya kuwa madam President akitupeleka alijojo tutamnyazia, la hasha.
Siishi katika ushabiki na kujipendekeza, ukweli utabaki kuwa ukweli. Hata yeye mama karuhusu kukosolewa. Nawashangaa ninyi mnaokataa asikosolowe. Pia hata yeye ushukuru uongozi mbalimbali wa nyuma ulopita. Ni ninyi washabiki ambao mnataka asikosolowe anapo kosea. Legacy ya Magufuli haito potea kamwe. Alikubalika duniani si Tanzania pekee. Alirejesha hesima ya Tanzania.
Nitasema na hakuna mtu wa kuniziba mdomo. Sibabaiki kwa lolote lile. Na siogopi chochote kile. Na wala sitegemei kujikomba ili nipate liziki yangu.
 
Boss ungetoa data za ziara za JPM katika miaka mitano 2015 to 2020. Wanufaika wakubwa wa ziara zake walikuwa Tabora, Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga
 
Acha kuuliza maswali ya kitoto
Rais haitaji kutembelea kila kijiji kujua kama waziri anafanya kazi zake vizuri.Nchi inaendeshwa kwa mifumo na kama unahisi mfumo uliopo sio madhubuti dai katiba mpya na serikali za majimbo sio kutaka Rais akakague mashimo ya choo ya shule na convoy.
Sijasema rais atembelee kijiji, bali nauliza atajuaje kuwa kama watumishi wake wanafanya kazi kiufasaha, mfano kama si kuingia mitandaoni asingejua kuwa huku mitaani vitendo vya ujambazi vimeudi.
 
Back
Top Bottom