Ni lini Rais Samia ataanza ziara kusikiliza kero za Wananchi?

Ni lini Rais Samia ataanza ziara kusikiliza kero za Wananchi?

Hivi unaelewa maana ya raisi? Unaelewa kazi za raisi? , mnaanza kujikosha mapema kwa kuwa mshajua kaanza kuaribu
Tujikoshe Ili tuvumbue nini? Fuatilia michango yangu yote sijawahi ona zuri kwa mwendazake ,huyu yuko kwenye raiti traki in Mwendazakes voice
 
Akiangalia bunge atafahamu changamoto za wananchi wake.
Mleta uzi nakuunga mkono.
Rais wa Tanzania lazima aijue Tanzania, ndani nje. Yeye si Rais wa dar au dom au zenj pekee.

Lazima akashuhudie changamoto za watu wake kwa kuwatembelea na kuongea nao. Huo ndio uongozi. Kuwa Rais wa nchi kubwa kama hii si kazi ya lelemama.

Msidanganye hapa kwamba asubirie dom au dar taarifa za wananchi wake. Hawezi kufika kila sehem lakin lazima awe na utaratibu wa kutembelea huko mawilayani. Lasivyo yale yaleee. Kwamba alikuwa Rais mzuri ila wasaidizi wake wamemuangusha
 
Huna mbunge wa kukusemea bungeni???
Mkuu, ndo wanavyotaka.

Ikikaribia uchaguzi au wakati wa kampeni ndo eti tuanze kumuona mara anaenda Sikonge, mara Liwale mara Songwe. Kwasasa hawataki. Wanataka wawe wanamlisha matango pori. Bosi kila kitu kiko shwari Rombo kumbe hamna lolote

Au wanamuonea huruma kuwa atakuwa anachoka?

Aende akashuhudie watu wake wanavyoishi hukoooo
 
Akiangalia bunge atajua kijiji chako hakina matundu ya kutosha ya choo katika shule zake. Relax.
Tatizo ni kwamba watz sio waaminifu ndo sababu unaona mjuba alikuwa front!!! Hawa wateule wengi usipo wafatilia ni ujanja ujanja tu huko uraiani mkuu
 
Kwamba unanambia rais anajua hayo yote akiwa barabarani kila siku akinunua mahindi na mapapai?
Dikteta anayetaka kutawala milele ndiyo huwa na hizo tabia ili kupata popularity.
Rais anayejielewa anakutana na wananchi lakini hawezi akawa anashinda barabarani kila siku kufanya propaganda.
Sina chuki na mtu, naipenda Tanzania, na naheshimu marais wote. Sihitaji toa kashifa za uongo kwa chuki binafsi. Nina imani, ambayo inanifundisha kuthamini utu wa binadamu wengine. Sihitaji kutoa maneno ya chuki na dharau. Sijafunzwa hivyo na wazazi wangu wala walezi wangu.
Nakosoa kwa hoja bila chuki nafsini mwangu. Na penye kusifu nitasifu kama kiongozi kafanya vizuri. Matuasi uwajaa watu waliopoteza mwelekeo na kukoswa hoja. Huku mioyo yao ikijazwa chuki.
 
Asikuongopee mtu aisee. Ukitaka kuwa kiongozi mzuri lijue eneo lako la kazi. Wajue watu wako unaowaongoza. Wajue wasaidizi wako na uwajue wa chini kabisa. Elewa maisha yao.

Lasivyo ukija ulizwa kwanin nchi yako au watu wako ni maskini utaishia kusema 'hata mimi sijui'

Ukielewa watu wako na maisha yao na changamoto zao na mafanikio yao hata ukitoa hotuba utakuwa unahutubia kiuhalisia. Lasivyo utakuwa unaongea vitu visivyo na mashiko kwa watu wako/ visivyo na uhalisia

Huwezi kujua yote hayo ukijikalia ofisini huku ukisubiri wabunge wetu hawa na wengne hawa wa kuteuliwa ambao wako bize kuhakikisha wanamfurahisha mkuu kwa kila hali
 
Ndiyo, Rais hawezi kutembelea vijiji vyote vya nchi hii
Hawezi kutembea vijiji vyote kweli. Lakin anaweza kutembea maeneo ya kutosha kuwakilisha maeneo mengine. Rais yeyote bora lazima ajue watu wake na uhalisia wa maisha yao
 
hapa tatizo ni mwendazake tu. aliwabrainwash sana watu kiasi wakaona ile staili ya uongozi ndo yenyew. huko chin kuna marc, madc na wengine kibao.
 
Maeneo ya kutosha ni mangapi katika kipindi cha miaka minne??
Ameshakuwa waziri kwa miaka mingi na makamu wa Rais kwa miaka mitano anajua vizuri watu wake na uhalisia wa maisha yao.
Hawezi kutembea vijiji vyote kweli. Lakin anaweza kutembea maeneo ya kutosha kuwakilisha maeneo mengine. Rais yeyote bora lazima ajue watu wake na uhalisia wa maisha yao
 
Tantarira nyingu tu zisizo na mashiko
Asikuongopee mtu aisee. Ukitaka kuwa kiongozi mzuri lijue eneo lako la kazi. Wajue watu wako unaowaongoza. Wajue wasaidizi wako na uwajue wa chini kabisa. Elewa maisha yao.

Lasivyo ukija ulizwa kwanin nchi yako au watu wako ni maskini utaishia kusema 'hata mimi sijui'

Ukielewa watu wako na maisha yao na changamoto zao na mafanikio yao hata ukitoa hotuba utakuwa unahutubia kiuhalisia. Lasivyo utakuwa unaongea vitu visivyo na mashiko kwa watu wako/ visivyo na uhalisia

Huwezi kujua yote hayo ukijikalia ofisini huku ukisubiri wabunge wetu hawa na wengne hawa wa kuteuliwa ambao wako bize kuhakikisha wanamfurahisha mkuu kwa kila hali
 
Ndiyo, Rais hawezi kutembelea vijiji vyote vya nchi hii

Ila wakati wa kuomba kura wanatembea hadi kata zote na viduku wanacheza, Siku yao ipo tu, Kwan uchaguz mbali bhas, tutakutana, Akili zenu huwa zinawaza mavi tu mbwa nyie
 
Ila mama anasafiri sana,tangu aanze urais hajatulia kabisa sijui muda wa kufanya maamuzi sahihi anaupata sangapi,muda wa kufikiria changamoto za wananchi na namna za kuzitatua,hata muda wa Ibada na Mwenyezi Mungu anaupata kweli,kila leo safari,events....na ndo ameanza tu majukumu
Huyu alikuwa makamu wa raisi anajua sehem ambazo boss wake alichemsha, safari zake zinalenga kutatua changamoto au ushirikiano uliodumaa na washirika wengine, mfano Leo Kenya wameruhusu wafanyabiashara wa mahindi waingize mama kaenda kumalizana na uhuru maana hali ilikuwa mbaya Sana..kaenda kwa miseveni kafanya vikao au mazungumzo na maraisi takribani saba, kukaa ndani ya nchi nakusikiliza kero za wananchi haziwez fanya wawekezaji waje na washirika wabiashara ambao tunahitaji fedha nyingi ili kutatua hizo changamoto na ajira za kutosha kwa wananchi muacheni atengeneze mifumo kero za wananchi anazijua maan alikuwa makamu wa serikali iliopita
 
Back
Top Bottom