Rais wetu anakwepa, majukumu yake. Basi ingekuwa kutumia watendaji wake hata huko nje asingeenda, angeacha waziri wa mambo ya nje amwakilishe. Kwani majukumu ya Waziri wa mambo ya nje ni nini?
Katiba inatoa haki ya wananchi kusikilizwa na Rais wao. Si migogoro au Kero zote uweza kutatuliwa na wakuu wa wilaya au Wakuu wa mikoa. Mfano kuna mgogoro ulishawahi tokea, halmashauri iliona vyema kubadili eneo litumike kama makazi. Hivyo viwanja viligawiwa kwa wananchi na wananchi walijenga.
Wizara ikaibuka ikasema hapana, eneo libaki kama hifadhi. Mkuu wa mkoa nae akawa upande wa wananchi.
Nakumbuka ilibidi Rais kuingilia kwani hata hao watendaji wa wizara kidogo wapingwe na wananchi walipojitokeza eneo husika.
Pia kuna migogoro baina ya maeneo ya jeshi na raia, mara nyingi uhitajika kauli ya Rais kama Amiri Jeshi Mkuu. Si hayo tu ni mengi kivyovyote Rais hawezi kukwepa majukumu akasingizia ana wawakilishi. Hatukatai kuwa na wawakilishi, na wanasaidia mengi.
Ila ajue kama mama hawezi acha kila jambo dani ya nyumba kutatuliwa na dada wa kazi. Kuna watoto wakorofi hawatomsikiliza dada au kumtii mpaka wasikie sauti ya mama. Huu ni mfano tu.
Wakuu wa mikoa wapo ila kutokana na utendaji na kanuni za kiutumishi kuna maeneo wanakwama.
Mfano kuna mama alikwamishwa malipo ya haki ya kijana wake kulipwa ambaye alifariki akiwa kazini. Katika kufatilia kote shida ilikuwa wizara ya fedha, walimsumbua yule mama miaka 9 bila kupewa haki ya kijana wake huyu mama alikuwa mzee kaachiwa wajukuu. Na aliishi mikoani.
Mkuu wa mkoa akashughulika na hii kesi ila Wizarani
wakawa wanazingua pamoja na kuwepo kwa mawasiliano lukuki.
Mkuu wa mkoa hawezi mwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha.
Kivyovyote kuna mengi ambayo Rais anatakiwa apate muda wa kuwasikiliza wananchi. Asikwepe kijanja. Kama vipi abaki ikulu kukaa tu kwani wawakilishi anao kila mahala. Tujue moja.
Hata marais wote walio pita waliwasikiliza wananchi. Atakuwa Rais wa pekee kukwepa kinamna majukumu yake. Kwanza ukiwasikiliza wananchi, unaelewa nini kinaendelea katika mfumo mzima wa utawala. Wakati mwingine wasaidizi udanganya kwa manufaa yao.