Ni lini Serikali ya CCM itanunua laptop kwa kila mwanafunzi kuanzia shule za kata?

Salaam, Shalom!!

Nimewahi kuandika Thread isomekayo,

Ushauri: Chakula Bure mashuleni kirudishwe Ili kuboresha uelewa wa wanafunzi.

Katika mada hiyo, Nimeshauri Serikali kuhakikisha inaweka mfumo Nchi nzima utakaosaidia wanafunzi shule za msingi angalau wapate kikombe Cha uji wawapo mashuleni.

Ikiwa jambo hili dogo halijatekelezwa Hadi sasa,

Je itachukua miaka mingapi Serikali ya CCM kuweza kuhakikisha Shule za msingi zinaunganishwa na Nishati ya umeme au solar Kila Kijiji, Ili Kila mwanafunzi aweze kupata na kutumia LAPTOP?

Ikiwa Nchi ndogo ya Rwanda imeweza,

Tujue, katika Nchi yetu chini ya utawala wa CCM itatuchukua muda Gani kama nchi kufika huko?

Ikiwa viongozi waliopo hawana MAONO hayo, tuchukue hatua Gani wananchi?

Karibuni.🙏

Amen.
Mlete Kagame afanye hivyo, awe kiongozi. Ameshavya hivyo. Atafanya hivyo ndani ya mwaka.

Pia, maji, umeme, SGR, Bwawa la umeme vito vingekamilika kwa wakati.
 
Kama nyumba za Waalimu na kununua vitabu wamegoma,itakuwa kompyuta?
Serikali ya CCM hii tunayoijua wote au Kuna nyingine mpya imeundwa!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Ni Kweli,

Kuna vijiji havina nyumba za kupangisha,

Mwalimu analazimika kusafiri umbali mrefu kwenda shule kufundisha na kurudi, ambapo ikiwa pangekuwa na nyumba ya shule Kwa ajili ya staff, ingeboreshwa ufanisi wa Elimu.

Bado tuna safari ndefu.
 
Mlete Kagame afanye hivyo, awe kiongozi. Ameshavya hivyo. Atafanya hivyo ndani ya mwaka.

Pia, maji, umeme, SGR, Bwawa la umeme vito vingekamilika kwa wakati.
Mlete wewe na uongozi wenu ulioshindwa kutimiza majukumu hayo madogo.
 
Isingebadilisha chochote. Sanasana kuna treatment ambayo mtoto wa kiongozi ataipata tofauti na wengine. Hapa namna ni kuboresha mazingira yaliyo kuanzia walimu, walipwe mishahara ya kueleweka na hii fani iwekwe mbali na wanasiasa na siasa
Tatizo la elimu ya nchi hii si kukosekana kwa hizo laptops kwa hao wanafunzi ila kukosekana kwa utashi wa serikali hasa katika kusimamia maslahi ya watekelezaji wa mitaala ambao ni walimu wetu.Walimu wanadai maslahi yao kibao kama vile malimbikizo ya mishahara hela za likizo na hela za masomo.Hilo suala la malimbikizo ya mishahara limelalamikiwa kwa miaka mingi licha ya kisingizio cha enzi za mwendazake kwamba tunahakiki limekoma.Kwenye issue ya madaraja kwa kweli mh Rais apewe maua yake amejitahidi mwalimu akipanda anabadilishiwa mshahara wake ndani ya miezi miwili wakati wa yule jamaa mwalimu alikuwa anaweza akakaa mpaka miezi 20 yuko na barua ya cheo kipya ila mshahara mpya holaa.Tatizo sugu kwa sasa ni hizo arrears za watumishi wetu walio katika mamlaka za serikali za mitaa i.e halmashauri ambako maveo manesi na walimu wetu wanalilia malimbikizo yao .Tatueni changamoto hizo wanafunzi wataanza kupata elimu bora
 
Salaam, Shalom!!

Nimewahi kuandika Thread isomekayo,

Ushauri: Chakula Bure mashuleni kirudishwe Ili kuboresha uelewa wa wanafunzi.

Katika mada hiyo, Nimeshauri Serikali kuhakikisha inaweka mfumo Nchi nzima utakaosaidia wanafunzi shule za msingi angalau wapate kikombe Cha uji wawapo mashuleni.

Ikiwa jambo hili dogo halijatekelezwa Hadi sasa,

Je itachukua miaka mingapi Serikali ya CCM kuweza kuhakikisha Shule za msingi zinaunganishwa na Nishati ya umeme au solar Kila Kijiji, Ili Kila mwanafunzi aweze kupata na kutumia LAPTOP?

Ikiwa Nchi ndogo ya Rwanda imeweza,

Tujue, katika Nchi yetu chini ya utawala wa CCM itatuchukua muda Gani kama nchi kufika huko?

Ikiwa viongozi waliopo hawana MAONO hayo, tuchukue hatua Gani wananchi?

Karibuni.🙏

Amen.
Nia ya ya serikali ni kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia, lakini pia kuhakikisha kila mwanafunzi ana nyenzo muhimu ya kujifunzia yaani Laptop.
Hata hivyo haya yote yatafanikiwa kulingana na upatikanaji wa fedha.
Asante
 
Nakiri, tatizo ni mfumo,

Mada unajaribu kuforecast, ikiwa tutaendelea na mfumo uliopo, itatuchukua miongo mingapi kufikia hatua ya kuhakikisha wanafunzi wa shule za kata wanapata vitendea KAZI kusaidia kujifunza?
 
Salaam, Shalom!!

Nimewahi kuandika Thread isomekayo,

Ushauri: Chakula Bure mashuleni kirudishwe Ili kuboresha uelewa wa wanafunzi.

Katika mada hiyo, Nimeshauri Serikali kuhakikisha inaweka mfumo Nchi nzima utakaosaidia wanafunzi shule za msingi angalau wapate kikombe Cha uji wawapo mashuleni.

Ikiwa jambo hili dogo halijatekelezwa Hadi sasa,

Je itachukua miaka mingapi Serikali ya CCM kuweza kuhakikisha Shule za msingi zinaunganishwa na Nishati ya umeme au solar Kila Kijiji, Ili Kila mwanafunzi aweze kupata na kutumia LAPTOP?

Ikiwa Nchi ndogo ya Rwanda imeweza,

Tujue, katika Nchi yetu chini ya utawala wa CCM itatuchukua muda Gani kama nchi kufika huko?

Ikiwa viongozi waliopo hawana MAONO hayo, tuchukue hatua Gani wananchi?

Karibuni.🙏

Amen.
Wewe! Watafilisi hawa wapenda cha juu, labda aitwe Magufuli asimamie.
 
Nia ya ya serikali ni kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia, lakini pia kuhakikisha kila mwanafunzi ana nyenzo muhimu ya kujifunzia yaani Laptop.
Hata hivyo haya yote yatafanikiwa kulingana na upatikanaji wa fedha.
Asante
Una HAKIKA upatikanaji wa Fedha ndo kikwazo?

Pesa za kulipa billion 75 fine, pesa za kununua mav8, pesa za makongamano, pesa za safari za nje za viongozi, pesa zinazoibwa Kwa billions zimepatika wapi ikiwa upatikanaji wa pesa ni kikwazo?
 
Fedha za v8, fine, laptops, Afya, Elimu, Maji n.k zote ni muhimu sana kwajili ya maendeleo ya nchi.
Serikali usiku na mchana inapambana kukusanya mapato ya kutosha ili kusudi kuwahudumia waTanzania wote mahali walipo.

Tuendelee kuwa wastahimilivu na kuiunga mkono serikali wakati ikiendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutafuta na kuhakikisha masuala mengi muhimu yanatengewa fedha za kutosha na kutekelezwa ikiwa ni pamoja na hilo unalopendekeza wewe.
Asanti...
 
Ushasema nchi ndogo ya rwanda
Ameongeza kuwa,hiyo nchi ndogo haina bandari,maziwa wala bahari ambavyo vyote vingekua vinaongeza mapato,kwenye nchi hiyo,ila sisi tuna kila kitu tajwa hapo juu,yaani nchi ni kubwa,idadi ya watu ni kubwa,walipa kodi ni wengi,tuna bandari,mito,maziwa hadi bahari ya Hindi,lakini eti tunazidiwa na Rwanda.Aisee eti tuliwahi kukopa tuchimbe vyoo vya huko mashuleni,aisee sembuse kununua laptops?
Mi naona kuna shida kwenye uongozi.
 
Wananchi tuendelee kujiunga mkono Serikali Hadi lini ilhali wanamaliza shule za msingi watoto wasiojua hata kuandika barua ya maombi ya KAZI?

Output hiyo, itajiajiri vipi kusaidia Serikali kupata Kodi ya kutosha kuhudumia wananchi,

Mimi nikifika hapo,

Naona tunaenda kuwa watumwa wa vinchi vidogo tulivyovisaidia kujitawala mfano randa nk nk.
 
Asee shida ni kubwa,

Tusipobadili uongozi uliopo,

Tutatawaliwa na Nchi Jirani, weusi wenzetu.

Ikiwa Kenya tu hapo Jirani,

ELIMU ninayotolewa na shule ya Serikali, umma Toka msingi ni Bora kuliko shule za binafsi,

Kule wazazi wanapigana vikumbo kupata nafasi kupeleka watoto wao shule za Serikali,

Huku viongozi wanaruhusu shule binafsi kuzidi ubora shule za umma!!

Ilboru, tabora boys mbona zilikuwa juu enzi ya Nyerere?

Tusikubali Hali hii!!
 
Wananchi tuendelee kujiunga mkono Serikali Hadi lini ilhali wanamaliza shule za msingi watoto wasiojua hata kuandika barua ya maombi ya KAZI?

Output hiyo, itajiajiri vipi kusaidia Serikali kupata Kodi ya kutosha kuhudumia wananchi,

Mimi nikifika hapo,

Naona tunaenda kuwa watumwa wa vinchi vidogo tulivyovisaidia kujitawala mfano randa nk nk.
Pole,
Ondoa fikra za kua mtumwa mahali popote duniani kutoka Tanzania. Hilo halitatokea CCM ikiwa Madarakani.

Serikali makini ipo kazini,
hivi sasa kilimo na masoko ya mazao ya kilimo vimeimarika mno, vijana wengi wasomi kwa wasio wasomi wanachangamkia fursa hiyo muhimu ya ajira, vipato vyao vimeongezeka, maisha yao ni mazuri na yanasonga mbele kwelikweli.
Serikali pia inafanya makubwa katika kila halmashauri kuwapesha vijana mabajaji, matrekta na fedha kwajili ya biashara n.k
vyote hivi vinafanyika kuwainua vijana kiuchumi na kubiresha maisha ya kila mtanzania.
Asant
 
Hizo laptop wanaenda nazo home au zinabakia shuleni cost ya bando watamudu je shule zote Zina umeme.
Maeneo yote Yana network.
Pana vijiji mtandao pekee ni halotel mnara mmoja Tena wa solar jua likizama hakuna network
 
Ikiwa Mwl Nyerere aliweza kuhakikisha tunapata chakula mashuleni,

Tulipasa Awamu ya SITA shule za kata wanafunzi wawe na laptop kama kitendea KAZI katika ujifunzaji!!
Nyerere alikua na akiba ya pesa za kutosha alizoachiwa na wakoloni
 
Salaam, Shalom!!

Nimewahi kuandika Thread isomekayo,

Ushauri: Chakula Bure mashuleni kirudishwe Ili kuboresha uelewa wa wanafunzi.

Katika mada hiyo, Nimeshauri Serikali kuhakikisha inaweka mfumo Nchi nzima utakaosaidia wanafunzi shule za msingi angalau wapate kikombe Cha uji wawapo mashuleni.

Ikiwa jambo hili dogo halijatekelezwa Hadi sasa,

Je itachukua miaka mingapi Serikali ya CCM kuweza kuhakikisha Shule za msingi zinaunganishwa na Nishati ya umeme au solar Kila Kijiji, Ili Kila mwanafunzi aweze kupata na kutumia LAPTOP?

Ikiwa Nchi ndogo ya Rwanda imeweza,

Tujue, katika Nchi yetu chini ya utawala wa CCM itatuchukua muda Gani kama nchi kufika huko?

Ikiwa viongozi waliopo hawana MAONO hayo, tuchukue hatua Gani wananchi?

Karibuni.🙏

Amen.
Madawati tu yamewashinda, laptop itakua ndoto
 
Pole,
Ondoa fikra za kua mtumwa mahali popote duniani kutoka Tanzania. Hilo halitatokea CCM ikiwa Madarakani.

Serikali makini ipo kazini,
hivi sasa kilimo na masoko ya mazao ya kilimo vimeimarika mno, vijana wengi wasomi kwa wasio wasomi wanachangamkia fursa hiyo muhimu ya ajira, vipato vyao vimeongezeka, maisha yao ni mazuri na yanasonga mbele kwelikweli.
Serikali pia inafanya makubwa katika kila halmashauri kuwapesha vijana mabajaji, matrekta na fedha kwajili ya biashara n.k
vyote hivi vinafanyika kuwainua vijana kiuchumi na kubiresha maisha ya kila mtanzania.
Asant
Mimi sitaki mwanangu amalize st kayumba akakopeshwa bodaboda.

Nataka ELIMU ya Shule za kata nchini zitoe Elimu Bora kuliko Elimu inayotolewa Feza international.

Enzi za Nyerere ilikuwa hivyo.

Ikiwa viongozi waliopo hawalioni Hilo,

Wanaruhusu Kenya wameiga alichofanya Nyerere ,shule zao sasa za umma zinatoa Elimu Bora kuliko binafsi.

Nataka mwanangu aje awe waziri akitokea Saint Kayumba!!
 
Back
Top Bottom