Ni lini Serikali ya CCM itanunua laptop kwa kila mwanafunzi kuanzia shule za kata?

Ndo nasema, uongozi ni vitendo Si maneno.

Ndugu tlaatlaa anadai Yeye ni Waziri aliyetokea shule za kata.

Ni vizuri tukawalazimisha wabunge kutunga SHERIA, viongozi wote wa umma wapeleke watoto wao shule za kata.
Ogopa sana kumpa mtu kazi/cheo katika field fulani kisa yeye ni mmoja kapitia hizo changamoto, mfano umpe mtu wizara ya kilimo kisa amkulia na kuishi kijijini katika familia ya wakulima yani huwa wanajisahau sana wanajipambani kwanza na hawana dira ya kutatua changamoto zaidi ya paper work yakutosha kuliko field work [emoji706]
 
sio ufagio tu,
akiagizwa jembe, kuni, maji ya kumwagilia maua na miti ya shule, majani kwajili ya kujengea vyoo vya walimu na kuezekea majiko ya walimu,
mwanangu anakwenda kuyasaka porini na anakwendra nayo shule kama wanafunzi wengine.
Hajaendraa nayo anaadhibiwa vizur tu...
Mbali na Magufuli,

Hivi Kuna kiongozi wa Umma katika mawaziri ambaye mtoto wake anasoma St Kayumba?

Naona unaingiza Siasa kwenye ELIMU yetu ndugu Waziri Tlaatlaah!!
 
Mfumo gani huo
Kuanzia kwenye level ya ELIMU ya kuajiri walimu,

Minimum iwe degree second upper.

Mfumo wa kupeleka Fedha mashuleni.

Mfumo wa makazi Bora ya walimu.

Vitendea KAZI, posho za walimu na marupurupu,

In short uwekezaji uwe Bora zaidi.
 
Hiyo tu ingetosha kuinua hii sekta ya elimu na ingeheshimika na tungevuna graduates bora na sio bora graduates
 
Mbali na Magufuli,

Hivi Kuna kiongozi wa Umma katika mawaziri ambaye mtoto wake anasoma St Kayumba?

Naona unaingiza Siasa kwenye ELIMU yetu ndugu Waziri Tlaatlaah!!
Mimi mwanangu anasoma huko unako paita st.kayumba ingawa mimi silipendi jina hilo.

Lakini tulikua mawaziri kadhaa kwenye shule hizo mathalani waziri wa Maji tena huyu alitoka mazingira magumu Zaidi,

Enzi izo yeboyebo ndio zilikua zimetoka basi yeye alikua nazo za njano zimeisha upande moja kwenye kisigino, hadi huruma 4yrs haindi likizo anabaki shule coz hakua na uwezo wa kifedha, alivumilia na ustahimilivu na bidii vyake huko shule ndivyo vinamgarisha leo yeye na mimi.

Hivi ninavyoandika wanae na wanangu wanasoma hizo shule unazoita st kayumba na wanafanya Vizuri tu.

Tembelea huko mavyuoni utakuta wanaofanya Vizuri wengine wametoka st kayumba hao wengine huweskia wala kuwaona waking'aa vyuoni .

Wengine singependa niwataje Lakini wapo wamejaa serikali na wametoka huko kayumba..
 
Takwimu haidanganyi, ni shule chache zinafanya vizuri lakini kwa bidii ya mwanafunzi tofauti kama mazingira yangekua vyema yangebeba ubora zaidi wa mwanafunzi,

Tusiseme hiv vile ukweli ni kwamba hizi shule zinahitaji sana msada mkubww tena sio kwa kupepesa macho, hizii shule ni nyingi zinaweza kuinua hii sekta ya elimu zikiboreshwa
 
Ndo nasema, uongozi ni vitendo Si maneno.

Ndugu tlaatlaa anadai Yeye ni Waziri aliyetokea shule za kata.

Ni vizuri tukawalazimisha wabunge kutunga SHERIA, viongozi wote wa umma wapeleke watoto wao shule za kata.
watoto wa viongozi wengi wanao wanasoma hizo shule mnaziita kayumba hili mbona liko wazi.
Kwani kiongozi ni nani?,

uongozi ni dhamana, leo unateuliwa kesho unatenguliwa, sasa unapata wapi uhakika wa kumpeleka mwanao kwenye hizo shule ambazo mnaziona bora hali ya kua hata kuteuliwa kwenyewe huna uhakika wa kutenguliwa ?

Mnatusingizia kisicho cha kweli.
Serikali inaboresha shule za kata na sisi viongozi tunaridhishwa na hayo maboresho na matokeo mazuri na wenetu wanasoma huko na Maendeleo yao yanaridhisha sana.

Nawapongeza walimu wote wa shule za kata nchini, kwa namna wanavyofanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa.
Asant.
 
Mimi mwanangu anasoma huko unako paita st.kayumba ingawa mimi silipendi jina hilo.

Lakini tulikua mawaziri kadhaa kwenye shule hizo mathalani waziri wa Maji tena huyu alitoka mazingira magumu Zaidi,

Enzi izo yeboyebo ndio zilikua zimetoka basi yeye alikua nazo za njano zimeisha upande moja kwenye kisigino, hadi huruma 4yrs haindi likizo anabaki shule coz hakua na uwezo wa kifedha, alivumilia na ustahimilivu na bidii vyake huko shule ndivyo vinamgarisha leo yeye na mimi.

Hivi ninavyoandika wanae na wanangu wanasoma hizo shule unazoita st kayumba na wanafanya Vizuri tu.

Tembelea huko mavyuoni utakuta wanaofanya Vizuri wengine wametoka st kayumba hao wengine huweskia wala kuwaona waking'aa vyuoni .

Wengine singependa niwataje Lakini wapo wamejaa serikali na wametoka huko kayumba..
Kiukweli,

Wananchi tunaposikia kuwa pesa za umma zinaibwa Kwa mabilioni,

Halafu mzazi maskini asiye na uwezo wa kulipa ada ya 20,000 Kwa mwaka Kwa mwanae,

Hapohapo anafuatwa achangie nusu gunia la mahindi Ili chakula kipikwe shuleni ni mtihani.

Serikali ipunguze matumizi yake yasiyo na TIJA Ili kuwekeza kwenye ELIMU.

Ubinafsi utaliangamiza Taifa letu zuri Tanzania.
 
watoto wa viongozi wengi wanao wanasoma hizo shule mnaziita kayumba hili mbona liko wazi.
Kwani kiongozi ni nani?,

uongozi ni dhamana, leo unateuliwa kesho unatenguliwa, sasa unapata wapi uhakika wa kumpeleka mwanao kwenye hizo shule ambazo mnaziona bora hali ya kua hata kuteuliwa kwenyewe huna uhakika wa kutenguliwa ?

Mnatusingizia kisicho cha kweli.
Serikali inaboresha shule za kata na sisi viongozi tunaridhishwa na hayo maboresho na matokeo mazuri na wenetu wanasoma huko na Maendeleo yao yanaridhisha sana.

Nawapongeza walimu wote wa shule za kata nchini, kwa namna wanavyofanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa.
Asant.
Pia ni vizuri ikiwa u kiongozi husika kwenye sekta ya KILIMO au Elimu Kwa level ya WAZIRI,

Ungeomba Verified Identity Ili kujibu HOJA ya wananchi.

Maana viongozi ni watumishi wa wananchi, Si vizuri kujificha nyuma ya I'd fake kama chawa wanaosumbua Kila kukicha kina Choice variable na Lucas mwashambwa!!
 
Takwimu haidanganyi, ni shule chache zinafanya vizuri lakini kwa bidii ya mwanafunzi tofauti kama mazingira yangekua vyema yangebeba ubora zaidi wa mwanafunzi,

Tusiseme hiv vile ukweli ni kwamba hizi shule zinahitaji sana msada mkubww tena sio kwa kupepesa macho, hizii shule ni nyingi zinaweza kuinua hii sekta ya elimu zikiboreshwa
nashukuru nawe unakiri kwamba shule hizi za kata zinaweza kuinua sekta hii ya Elimu.
Rejea matokeo ya darasa la saba, form 4 na 6, miaka miwili hii ya sasa na miaka miwili ya nyuma zaidi utangundua ubora na kiwango cha Elimu nchini unavyo kua na kuimarika kwa kasi nchini.

Hivi sasa kila kata ina shule yake,
Serikali inafanya kazi kubwa kuhakikisha shule zote zinakua na walimu wa kutosha, maabara zilizokamilika, viwanja vya michezo, mabweni, chakula n.k

Yote haya yanahitaji fedha nyingi, muda, mipango, na ustahimilivu.
Na serikali inafanya kila liwezekanalo yote kwa pamoja yafanyike.
 
Salaam, Shalom!!

Nimewahi kuandika Thread isomekayo,

Ushauri: Chakula Bure mashuleni kirudishwe Ili kuboresha uelewa wa wanafunzi.

Katika mada hiyo, Nimeshauri Serikali kuhakikisha inaweka mfumo Nchi nzima utakaosaidia wanafunzi shule za msingi angalau wapate kikombe Cha uji wawapo mashuleni.

Ikiwa jambo hili dogo halijatekelezwa Hadi sasa,

Je itachukua miaka mingapi Serikali ya CCM kuweza kuhakikisha Shule za msingi zinaunganishwa na Nishati ya umeme au solar Kila Kijiji, Ili Kila mwanafunzi aweze kupata na kutumia LAPTOP?

Ikiwa Nchi ndogo ya Rwanda imeweza,

Tujue, katika Nchi yetu chini ya utawala wa CCM itatuchukua muda Gani kama nchi kufika huko?

Ikiwa viongozi waliopo hawana MAONO hayo, tuchukue hatua Gani wananchi?

Karibuni.🙏

Amen.

ndugu mie wa kwanza kupinga hizo habar ya comouter shulen mwa kata,, yaani hizo shule za kata darasa moja watoto 80 kwasababu hakuna madarasa, hakuna vyakula mchana, hakuna walimu wa kutosha, hakuna vitabu, hakuna umeme, hakuna madawati.. kisha upeleke laptop shulen.. yaan kwenye matatizo yote wewe hili umeona tatizo?
 
Kiukweli,

Wananchi tunaposikia kuwa pesa za umma zinaibwa Kwa mabilioni,

Halafu mzazi maskini asiye na uwezo wa kulipa ada ya 20,000 Kwa mwaka Kwa mwanae,

Hapohapo anafuatwa achangie nusu gunia la mahindi Ili chakula kipikwe shuleni ni mtihani.

Serikali ipunguze matumizi yake yasiyo na TIJA Ili kuwekeza kwenye ELIMU.

Ubinafsi utaliangamiza Taifa letu zuri Tanzania.
Pole sana,
Swala la ubadhirifu mali ya uma na Rushwa linabaki binafsi kwa muhisika na vyombo vya uchunguzi.

Tutashughulika pia na Elimu ya Rushwa kama somo kwenye maboresho ya mitaala yajayo
 
Salaam, Shalom!!

Nimewahi kuandika Thread isomekayo,

Ushauri: Chakula Bure mashuleni kirudishwe Ili kuboresha uelewa wa wanafunzi.

Katika mada hiyo, Nimeshauri Serikali kuhakikisha inaweka mfumo Nchi nzima utakaosaidia wanafunzi shule za msingi angalau wapate kikombe Cha uji wawapo mashuleni.

Ikiwa jambo hili dogo halijatekelezwa Hadi sasa,

Je itachukua miaka mingapi Serikali ya CCM kuweza kuhakikisha Shule za msingi zinaunganishwa na Nishati ya umeme au solar Kila Kijiji, Ili Kila mwanafunzi aweze kupata na kutumia LAPTOP?

Ikiwa Nchi ndogo ya Rwanda imeweza,

Tujue, katika Nchi yetu chini ya utawala wa CCM itatuchukua muda Gani kama nchi kufika huko?

Ikiwa viongozi waliopo hawana MAONO hayo, tuchukue hatua Gani wananchi?

Karibuni.[emoji120]

Amen.
Viongoz wenyew njaa tupu, wezi mixer vibaka kila sekta wao kuminya tu roho za ubinafc wao ztakapokoma ndio itawezekana kutimiza hayo
 
Pole sana,
Swala la ubadhirifu mali ya uma na Rushwa linabaki binafsi kwa muhisika na vyombo vya uchunguzi.

Tutashughulika pia na Elimu ya Rushwa kama somo kwenye maboresho ya mitaala yajayo
Pia ni vizuri mkakubali issue ya KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi,

Ni Kwa maslah mapana ya nchi yetu.
 
ndugu mie wa kwanza kupinga hizo habar ya comouter shulen mwa kata,, yaani hizo shule za kata darasa moja watoto 80 kwasababu hakuna madarasa, hakuna vyakula mchana, hakuna walimu wa kutosha, hakuna vitabu, hakuna umeme, hakuna madawati.. kisha upeleke laptop shulen.. yaan kwenye matatizo yote wewe hili umeona tatizo?
Soma thread hii:

Ushauri: Chakula Bure mashuleni kirudishwe Ili kuboresha uelewa wa wanafunzi.- Rabbon.

Niliandika thread hiyo purposely kuikumbusha Serikali kuongeza uwekezaji kwenye ELIMU.
 
Kuna siku niliumia nilikuwa naangalia documentary moja Kenya,kuna dogo yupo Primary lakini anajua issues za "Coding" vibaya mno.
Alafu sisi tupo na hiki chama cha Majangili tunadanganyana!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Kuna wenye degree za coding wamemaliza vyuo vikuu.hizo nchi kazi hawana

Na Tanzania tunao wenye degree coding zote wanajua kazi hawana na hata wakitaka kujiajiri soko la wahitaji hizo huduma nchini hawapo
 
Wananchi tuendelee kujiunga mkono Serikali Hadi lini ilhali wanamaliza shule za msingi watoto wasiojua hata kuandika barua ya maombi ya KAZI?
Kujua kuandika barua ya kuomba kazi ni kuelimika?
Kwanini mtoto asiandaliwe kujiajiri ili tuepukane na hili janga la vijana kukosa ajira na maarifa.
 
Ikiwa Mwl Nyerere aliweza kuhakikisha tunapata chakula mashuleni,
Wakati uke shule za msingi zilikuwa mbali sana na nyumbani kwa mtoto

Sasa hivi shule za msingi ziko jirani tu na makazi ya mtoto
 
Back
Top Bottom