serikali haijawahi kuacha kufanyia kazi masuala yenye maslahi mapana ya nchi.
naomba muelewe kwamba watoto wa viongozi walio wengi wanasoma shule za kata na wanamaendeleo mazuri sana.
pelekeni watoto wenu huko kata, pamenoga.
masuala yote ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiutamadudi, sayansi na tekinolojia yataendelea kuboreshwa kwa mipango, awamu na kadiri ya upatikanaji wa fedha.
wito wangu kwenu wananchi wenzangu, tuipe nafasi serikali, tujitahidi kulipa kodi kwa wakati bila kukwepa, tuiunge mkono ccm na serikali yake, ili hatimae masuala muhimu ikiwemo hili la katiba yaweze kufanyiwa kazi kwa wakati muafaka na kwa hatua na kuweza kuimarisha, Amani, umoja, mshikamano na utangamano miongoni mwa Watanzania.