Ni lini umewahi kumsikia Rais Samia Suluhu Hassan akizungumzia mambo haya?


mkuu tulipigwa!!!!

Nyerere ndiye aliyetuletea Muungano hewa. Maana ugombea-wenza alibebwa na anakotokea tu na sio kinginecho.

endeleeni kukopa
 
Hakuna Rais hapa ni Bomu tena la kienyeji
 
Mbona anaongea na kusema hakopi kununua sare za harusi!
Anaongea sana, huenda mkuu 'Allen' kapitiwa tu.
Mambo ya "Kufungua nchi" mara hii tumeyasahau. Bandari na mapori yetu kugawiwa , hayo siyo uchumi?

Yeye kila siku anaimba "wawekezaji" waje hapa kwa wingi kutuletea maendeleo; hata haya mkuu 'Allen' hajawahi kumsikia akiyazungumzia? Anaamini waTanzania, hasa waTanganyika hawana uwezo wowote wa kujiletea maendeleo, kwa hiyo njia bora iliyopo ni kuwafanya watwana tu wa hawa watu toka nje. Hawa ndio watakaokuwa wamiliki wetu wapya katika dira ya mama kwa taifa letu.

Kilimo kamkabidhi Msomali, anayemwamini kwamba hakuna mwingine yeyote anayeweza kuiongoza wizara hiyo bila ya huyo Msomali; ambaye yeye kwa upande wake anaona Wizarani mahali pa kugawa ardhi yetu kwa watu maalum wanaotambuliwa na CCM, vijana wa CCM. Kama wewe au mwanao hana koneksheni na CCM, ukoo wako wote utabaki kuwa maskini milele.

Yapo mengi sana aliyofanya na anayofanya mama kuhakikisha kuwa nchi hii inatawaliwa tena kinamna. jaribu tu kutuliza akili zako utaona kazi kubwa anayo ifanya kufikia malengo hayo.
Sasa subiri uone miujiza hapo baada ya Oktoba, baada ya kujichukulia madaraka kwa nguvu. Nina hakika hutapata tena fursa ya kukuna kichwa kutambua atakayo yafanya; kwani atakuwa hana kizuizi tena au nongwa ya kuambiwa yeye hakuchaguliwa kuongoza taifa hili.
 
Bila shaka sasa umechanganyikiwa au ni kipofu wa akili na macho. Hayo mambo yamezungumzwa na yamekuwa yakizungumzwa sana na Mheshimiwa Rais. Nami nimeyaleta sana humu jukwaani yale ambayo Mheshimiwa Rais amekuwa akiyazungumza kuhusu mambo hayo yote
 
Tangu aingie huyo mama yenu nchi imepoteza uelekeo kwa kiwango cha kutisha.Kila mhuni na nyang'au kwenye nafasi yake anafanya atakavyo.Wizi,udhalimu,uzembe,kutojali n.k. yote haya yameshika hatamu
 
one cannot diverge from nature. Kama asili yake si kuzungumzia masuala uliyoainisha hata weza.kuzungumzia mpaka atakapomaliza utawala wake.

Umeona hata ajenda ya nishati mbadala ni kama ameandikiwa kameza halafu ndio anaizungumza kunakuwa hakuna msisimko wa hoja sababu sio genuine.
 
Ndio maana nina shaka wanaccm wenye kujitambua hawataenda kupiga kura mwaka huu. Watapenda ccm ishinde kwa mategemeo mbeleni wataweza kuja pata fursa kuchagua mgombea anayebeba vema itikadi ya ccm ya ujamaa na kujitegemea.
 
Yeye kipaumbele chake ni kuwa Rais tena hata kwa kumwaga damu
 
Unataka kina cha aina ipi?
Kwa mfano sisi kama Taifa sera yetu kuhusu Afrika na Afrika ya Mashariki ikoje.

Kwa Afrika ya Mashariki tunafanya biashara na nchi ipi na maslahi yetu ni nini?

Ajira kwa vijana ikoje. Serikali inafanya nini kwa kusudia kuongeza ajira na kupanua wigo wa ajira na kuongeza uwezo wa sekta binafsi kuajiri.

Serikali inatoa nafuu kiasi gani ya Kodi (Tax incentives) kwa biashara zinazoanzishwa na wazawa? Na biashara za wazawa zinalindwa vipi na Serikali?
 
Mbona hivyo vitu vimeelezwa sana na Mheshimiwa Rais? Tena kwa kina sanaa? Mimi sitaki kuanza kurudia hapa maana inaonyesha una matatizo ya kupoteza kumbukumbu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…