Kuna tatizo la utoaji wa habari za kinachosainiwa. Kwenye mradi huu wa ujenzi wa bomba la mafuta, kuna mikataba mingi inayosainiwa, wananchi hatuambiwi jumla ya mikataba na kinachosainiwa ni nini. Wanadhani alichosaini JPM ni kile kile alichosaini Samia, na Samia alipokwenda kusaini Kampala ndio kile kile kilichosainiwa hapa Dar.
Kwenye hii mikataba iko ya intergovermental, na host goverment. Intergoverment ni mikataba ya serikali za Uganda na Tanzania, ambayo imesainiwa pande zote. Host government ni mkataba wa sisi Tanzania ni host tuu wa bomba la mafuta. Mwenye mafuta ni Uganda, mchimbaji ni Total, ndie mwenye bomba. Tanzania tunapitisha tuu. Mfano ule mkataba wetu wa asilimia 16% ya free carried shares kati ya Tanzania na Barrick, imesainiwa mikataba 12!.
Hivyo hata baada ya kisainiwa mikataba iliyopo, bado kuna mingine itafuata.
Problem ni information.