Ni mara ya 6 tunashuhudia utiaji saini bomba la mafuta Hoima - Tanga

Ni mara ya 6 tunashuhudia utiaji saini bomba la mafuta Hoima - Tanga

Dah, hili jambo na mimi nilikuwa naliwazia. Wanatuhadaa ila faida za hii kitu kwa Tanzania zitakuwa ni sifuri, zero. Tutakachopata kutoka kwenye hili bomba ni ubadhilifu na kashfa tu za rushwa.
 
Pamoja na hayo mbona mbwembwe kwenye hili bomba zimezidi huwa hatuzioni kwenye mikataba mingine ya aina hii, ukweli ni kwamba pesa hakuna wafadhili Total na Tullow bado hawajaewana.
Ukweli ni kwamba hujui kitu chochote..kaa kwa kutulia mama afanye kazi..usiishi kwa mazoea. #NAKAZIIENDELEE
 
Acha tu, bado wakasaini ngorongoro crater na serengeti! 🤐
 
....Inawezekana mkataba una kurasa nyingi za kusaini!
Na hiyo mikurasa mingi ndiyo Wazungu wanatupigia humo, maana wanajua Nani ataka asome hayo maandishi mengi,na kawaida Watanzania wengi hatupendi kusoma Maandishi marefu!!
 
Pamoja na hayo mbona mbwembwe kwenye hili bomba zimezidi huwa hatuzioni kwenye mikataba mingine ya aina hii, ukweli ni kwamba pesa hakuna wafadhili Total na Tullow bado hawajaewana.
Changa la macho kwa kwenda mbele , hawasemi ukweli watu wa mazingira wameukataa mradi .
 
Aug 5. 2017 Museveni alikuja Tanga kuweka jiwe la msingi, baadaye JPM alienda Uganda kusaini, September 2020 Museveni alikuja Dar kutia saini, Museveni akaja tena Chato kusaini, April 11, 2021 Rais Samia akaenda Uganda kusaini, jana Mseveni kaja tena Dar kusaini. Dah!

Kazi iendelee.
===============
Ukweli ni kwamba.....
===============
Ukiona hivyo ujue hakuna mradi wowote watu wanatiana moyo tu.
 
JPM alienda Uganda kusaini, Museveni akaja Dar kusaini, MusevenI akaja tena Chato kusaini, Samia akaenda Uganda kusaini, Museven kaja Dar kusaini. Wanachofanya hawa viongozi ni kuwapiga wananchi changa la macho. Huwa wanaamini kuwa wananchi ni wajinga kama wao.
Usipofuatulia habari ni kitu gani wanachotia sahihi, utafikiri ni kijinga. Lakini ukufuatilia, unaweza kushangaa tu mbona kuna watu wanaotumia kompyuta na intaneti na bado hawajui kusoma habari na kufanya uchunguzi kidogo kama wamesahau habari...
Haikuwa siri...
 
Kuna tatizo la utoaji wa habari za kinachosainiwa. Kwenye mradi huu wa ujenzi wa bomba la mafuta, kuna mikataba mingi inayosainiwa, wananchi hatuambiwi jumla ya mikataba na kinachosainiwa ni nini. Wanadhani alichosaini JPM ni kile kile alichosaini Samia, na Samia alipokwenda kusaini Kampala ndio kile kile kilichosainiwa hapa Dar.

Kwenye hii mikataba iko ya intergovermental, na host goverment. Intergoverment ni mikataba ya serikali za Uganda na Tanzania, ambayo imesainiwa pande zote. Host government ni mkataba wa sisi Tanzania ni host tuu wa bomba la mafuta. Mwenye mafuta ni Uganda, mchimbaji ni Total, ndie mwenye bomba. Tanzania tunapitisha tuu. Mfano ule mkataba wetu wa asilimia 16% ya free carried shares kati ya Tanzania na Barrick, imesainiwa mikataba 12!.

Hivyo hata baada ya kisainiwa mikataba iliyopo, bado kuna mingine itafuata.

Problem ni information.
Umefafanua vyema sana Brother, unafaa kuwa "Msemaji Mkuu wa Serikali". Information kama hii ilipaswa kutoka Serikalini kwenda kwa Wananchi ili waelewe.
Sijui kwanini Madam SSH hakuoni akupe japo kauteuzi katika Serikali yake.
 
Kuna tatizo la utoaji wa habari za kinachosainiwa. Kwenye mradi huu wa ujenzi wa bomba la mafuta, kuna mikataba mingi inayosainiwa, wananchi hatuambiwi jumla ya mikataba na kinachosainiwa ni nini. Wanadhani alichosaini JPM ni kile kile alichosaini Samia, na Samia alipokwenda kusaini Kampala ndio kile kile kilichosainiwa hapa Dar.

Kwenye hii mikataba iko ya intergovermental, na host goverment. Intergoverment ni mikataba ya serikali za Uganda na Tanzania, ambayo imesainiwa pande zote. Host government ni mkataba wa sisi Tanzania ni host tuu wa bomba la mafuta. Mwenye mafuta ni Uganda, mchimbaji ni Total, ndie mwenye bomba. Tanzania tunapitisha tuu. Mfano ule mkataba wetu wa asilimia 16% ya free carried shares kati ya Tanzania na Barrick, imesainiwa mikataba 12!.

Hivyo hata baada ya kisainiwa mikataba iliyopo, bado kuna mingine itafuata.

Problem ni information.
Huwa tunaambiwa mikataba ni Siri,huenda hata hii ni Siri pia.
 
Aug 5. 2017 Museveni alikuja Tanga kuweka jiwe la msingi, baadaye JPM alienda Uganda kusaini, September 2020 Museveni alikuja Dar kutia saini, Museveni akaja tena Chato kusaini, April 11, 2021 Rais Samia akaenda Uganda kusaini, jana Mseveni kaja tena Dar kusaini. Dah!

Kazi iendelee.
===============
Ukweli ni kwamba.....
===============
Huu mradi hautafanyika kamwe kwa wanaojua kwanini wanajua.
 
Back
Top Bottom