Ni mara ya 6 tunashuhudia utiaji saini bomba la mafuta Hoima - Tanga

Movie zinaendelea!
Hakuna mradi hapo..
Wanaharakati na watetezi wa mazingira washafungua kesi kibao huko kuzuia huu mradi sababu sehemu kubwa ya huu mradi athari za mazingira hazijaangaliwa..
Barclays UK ni one of the banks/financier wa hii project ameshajitoa na kuna Bank ya Ufaransa pia imeshanyoosha mikono pia.
 
Wafadhili walikuwa hawamtaki dikteta Magufuli John ila sasa japo wamemuondoa lakini ni kama bado hawana imani na Samia.

Kadri ccm watakavyoendelea kung'ang'ania madaraka ndivyo watanzania tutakavyozidi kukosa mambo mengi tofauti na kama wangekuwa wameondoka madarakani. Ni sawa tu na Zanu PF kule Zimbabwe.
 
Believe me hakuna cha Bomba la mafuta wala nini , Wanangu wa lasaba waliokimbilia Tanga kutega uvibarua kwenye hlo igizo la Bomba la mafuta nawasihi warudi makwao wasije wakakuta wake zao washazalishwa
Mu7 anacheka tu manake anajua ataendelea kusaini na marais tofauti tofauti wa TZ yeye akiwa yuleyule miaka yote ijayo
 
Inashangaza kwa kweli.
Mikataba ya iptl,dowans,aggreko,makampuni ya uchimbaji madini ,gas,nk saini Mara moja klia kitu kimeenda!lol

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mhhh hata Mimi nikajisemea huwa kinasainiwa nn kila siku watu wanasign wanasign tangu Ruge Mutahaba na Mengi wako hai bado linasainiwa tu...Mzee wetu amgekuwepo ungesikia "jamani perekeni pendekezo tusaign vitu vyote pamoja sign nazo zimekuwa nyingi mno watani zangu Waganda nasema uongo ndugu zangu? Ili Pesa za kusafiri safiri tuzifanyizie kazi nyingine....tusaign kila kitu pamoja Museven akikubali fedha tutajenga daraja rire linaunganisha kagera na Uganda iri wanaume wa Tz nao wakachumbie huko na kandarasi tutatoa bure kabisa kutoka Tz au Jeshi letu kabisa kwaajili ya kujenga . daraja.....just joking life is too short...Rip genius.
 
Though sina taarifa za uhakika ila nashawishika kuamini kuwa ujenzi unafanywa kwa phases na unafanywa na makampuni tofauti,hivyo kila mjenzi anapopatikana contract inasainiwa
 
Sasa muulize musaidiwe kuelewa huwa wanasign nini?
 
....Inawezekana mkataba una kurasa nyingi za kusaini!
 

Pia vyombo vya habari wakikutana na waziri wa Nishati , Waziri wa Mambo ya Nje au Mkurugenzi Mkuu wa TPDC huwa wanakuwa wasikilizaji tu, hawaulizi maswali ya kutaka ufafanuzi, mikakati n.k

Tutegemee waandishi wa habari watakuwa wadadisi kama wanaJF na kutumia uzi huu wa comment hii ya Paschal Mayalla kama 'framework' ya uandishi wao na pia 'yardstick' ya kutumia kuwahoji wakubwa iwe ni kwa Prof. Palamagamba Kabudi kuhusu 'mahabusu wa kisiasa' au Dr. Medard Kalemani kuhusu 'Luku' au Dr. Dorothy Gwajina na covid-19 n.k
 
Leo naona umerudi 2017, hongera sn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…