Ni mara ya 6 tunashuhudia utiaji saini bomba la mafuta Hoima - Tanga

😁😁😁 wanasaini tu, mimi pia sielewi.
Nakumbuka kauli iliyotoka "... sasa tuache maneno bomba lijengwe..." nukuu isiyo rasmi. Nadhani sasa litajengwa ila mwanzo ilikuwa ni maneno tu...
 
Dah, hili jambo na mimi nilikuwa naliwazia. Wanatuhadaa ila faida za hii kitu kwa Tanzania zitakuwa ni sifuri, zero. Tutakachopata kutoka kwenye hili bomba ni ubadhilifu na kashfa tu za rushwa.
 
Pamoja na hayo mbona mbwembwe kwenye hili bomba zimezidi huwa hatuzioni kwenye mikataba mingine ya aina hii, ukweli ni kwamba pesa hakuna wafadhili Total na Tullow bado hawajaewana.
Ukweli ni kwamba hujui kitu chochote..kaa kwa kutulia mama afanye kazi..usiishi kwa mazoea. #NAKAZIIENDELEE
 
Acha tu, bado wakasaini ngorongoro crater na serengeti! 🤐
 
....Inawezekana mkataba una kurasa nyingi za kusaini!
Na hiyo mikurasa mingi ndiyo Wazungu wanatupigia humo, maana wanajua Nani ataka asome hayo maandishi mengi,na kawaida Watanzania wengi hatupendi kusoma Maandishi marefu!!
 
Pamoja na hayo mbona mbwembwe kwenye hili bomba zimezidi huwa hatuzioni kwenye mikataba mingine ya aina hii, ukweli ni kwamba pesa hakuna wafadhili Total na Tullow bado hawajaewana.
Changa la macho kwa kwenda mbele , hawasemi ukweli watu wa mazingira wameukataa mradi .
 
Ukiona hivyo ujue hakuna mradi wowote watu wanatiana moyo tu.
 
Usipofuatulia habari ni kitu gani wanachotia sahihi, utafikiri ni kijinga. Lakini ukufuatilia, unaweza kushangaa tu mbona kuna watu wanaotumia kompyuta na intaneti na bado hawajui kusoma habari na kufanya uchunguzi kidogo kama wamesahau habari...
Haikuwa siri...
 
Umefafanua vyema sana Brother, unafaa kuwa "Msemaji Mkuu wa Serikali". Information kama hii ilipaswa kutoka Serikalini kwenda kwa Wananchi ili waelewe.
Sijui kwanini Madam SSH hakuoni akupe japo kauteuzi katika Serikali yake.
 
Huwa tunaambiwa mikataba ni Siri,huenda hata hii ni Siri pia.
 
Huu mradi hautafanyika kamwe kwa wanaojua kwanini wanajua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…