Ni maswali gani unahisi hayajibiki duniani?

Ni maswali gani unahisi hayajibiki duniani?

Mfano
1. Kuna nini kinaendelea baada ya kifo.?
2. Mwenyezi Mungu alitokea wapi?
1. Ni maisha in another dimension tofauti na physical world so kufa sio kupotea na kinachokufa na mwili maana vitu vyenye asili ya physical world huwa vinatabia ya kutokudumu milele ila wewe ni Nafsi hai inayoishi ndani ya nyumba inaitwa mwili.
2. God has neither begining nor end kwa sababu hata time ni part ya creation yake, so physical things are the ones which are limited by time.
 
roho ikoje?
Roho ni nguvu au nishati (energy) inayovipa uhai vitu visivyo na uhai, so it's just nguvu haina umbo ingawa inaweza kuchukua umbo lolote, mfano moto au maji vinaumbo gani? Ila vinaweza kuchukua umbo la chochote kutegemea viko wapi, ila roho ikiwa na nafsi, ndio tunapata Nafsi hai yenye utashi mawazo maamuzi hisia tabia elimu na makolokolo yote ambayo yapo kwenye nafsi au yanayounda nafsi, kwa hiyo roho kama roho yenyewe ni nguvu isiyo na utashi maamuzi tabia elimu hisia na Nafsi bila roho haiwezi kuonesha hizo sifa zake ingawa zipo lakini bila roho zinakuwa zimekufa ni sawa na simu nzuri sana yenyewe kila kitu miziki social Networks operating system bila betri hakuna kila kitu.
 
Mungu hashindwi chochote? Kama ndiyo; basi mungu anaweza kutengeneza jiwe kubwa ambalo hawezi kulibeba?
Why jiwe, na alibebe anapeleka wapi anampelekea nani na kwanini, ukitafakari kwa makini utafahamu kuwa kila kitu kinafanyika kwa sababu na makusudi maalum kama ipo sababu na kusudi na umuhimu wa kufanya hivyo hakuna cha kumzuia kutimiza matakwa yake, kama lengo lake ni asiweze kulibeba bado hashindwi kufanya hivyo.
 
Hahahahahahaha, kama alivyomtengeneza shetani akashindwa kumcontrol
Ndivyo unavyojidanganya shetani kaachwa kimkakati na kwa sababu, ni sawa na kusema majeshi ya UN kushindwa kumaliza waasi Congo ila wanaachwa tu kimkakati na kwa sababu za wakulu [emoji16] ila anytime wakiamua kuwafuta ni swala dogo sana
 
1.Nani ni mmiliki wa logo ya copy right?
2.Ukiwa mwezini ukiangalia juu unaona nini?
Anga ya mwezini ni giza tu haijalishi kuwe na jua au hamna ni kwa sababu hamna atmosphere (collection of different gases) it's vacuum to some extent
 
Kwani yale maswali ya kiranga yalishajibiwa? Yangejibiwa kwanza yale ndo maswali mengine yafuate.
 
Kabla ya kuzaliwa na kuuvaa huu mwili ulikuwa wapi?
 
Kuna mtu humu aliuliza hvi mtu ukimiliki ardhi ni unaimiliki had tu the core yaani kiini cha dunia?

Week kadhaa nilipata nafasi ya kufanya kazi ya kupima viwanja. Nilipata nafasi ya kumuuliza hili swali afisa ardhi alijibu NDIYO!

ndio maana unaruhusiwa hata kuchimba kisima futi uzitakazo ilmradi uyakute maji.
Akanitania kwa kusema ila kama ardhi yako ina madini basi serikali hufanya yake.
 
Yapo mambo ambayo Mungu hawezi fanya au kutenda inagawa anaweza yote .
1.Hawezi kutenda dhambi.
2.Hawezi kwenda kinyume na sheria alizoziweka mwenyewe hata Kama anayo nguvu na mamlaka.
3.Hawezi kusema uongo.
4.Hawezi kuhacha kutunza na kutekeleza maagano.
 
Hakuna swali lisilojibika duniani sema tu tumelimitiwa tu ,tufahamu haya na mengne tusijue,kwa manufaa ya wajanja wachache
 
Back
Top Bottom