Ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?

Ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?

Binafsi mimi mtu ambae nilimshuhudia akipitia maumivu.

Huyu dada alikuwa hospitali akiumwa saratani ya titi,

Titi lake lilikuwa limeoza kwa upande wa kwapa huku.
Huyu dada dawa ya kuzuia maumivu ilikuwa ikiisha nguvu alikuwa analia sana.
Alikuwa anaumia sana.
Inasikitisha sana.
Hii mwaka 2015 Magomeni,mimi nilimshuhudia huyu dada/mama kwa kumkadiria umri alikuwa na 44/46 akiwa kwenye hatua za mwisho.

Nasema hatua za mwisho kwa sababu tulipoenda kumuona ilikuwa saa mbili usiku akawa amekaa kitandani lakini hawezi kusema chochote huku anapiga kwikwi kali ile isiyoachia tulikuwa na mtu mzima mmoja akasema huyu kesho saa sita hafiki kweli siku iliyofuata saa nne nikasikia amefariki,uchungu mkubwa sana tulipoenda tulimkuta na mama yake dada yake na wanae wawili yaani walikuwa hawana cha kufanya zaidi ya kusubiri hatma.

Mungu awapumzishe kwa amani wote na awape afueni wanaokutana na mtihani huu.
 
Wakuu habari za humu ndani.
Hivi ni maumivu gani makali zaidi ya mwili wa binadamu ushawahi ku experience au uliona mtu anapitia ukaona kabisa ni maumivu makali kwa binadamu.

Kwangu mimi ni maumivu ya tumbo,kuna siku niliwahi changanya pilipili kichaa na vitunguu swaumu nikabrend then nikanywa aisee maumivu niliyoyapata sitakuja kusahau.Niliona Israel huyu hapa kaja kunisalimia.Tumbo linauma asikuambie mtu.

Je ni ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?
Maumivu ambayo nmewah ku experience a, ni MAUMIVU YA KIPANDE USO , MBELE YA PAJA LA USO,. Asee maumivu yake nmakali mno unakuwa unatamani hata kujitoboa damu itoke, ukisogeza hata mkono au kitu chochte karbia na uso panauma, ukiinama panauma, hata ukifanya movement yoyte panauma zaidi, asee sisemi mengi ila walioptia hii changamoto wanajua 🙏.
 
Chukua pilipili kichaa zilizokomaa vyema ziponde / twanga kwenye kinu kisha loweka kwenye mafuta ya taa halafu weka juani kwa muda wa lisaa. Chovya kitambaa kwenye huo mchanganyiko halafu pangusa kwa namna ya kupakaa kwenye eneo linalouma (paji la uso) kisha kaa sehemu yenye utulivu kwa masaa walau manne kabla hujaenda kuosha uso wako.

Binti yangu alisumbuka sana na kadhia hiyo ,katika kuhangaika nikaelekezwa tiba hiyo ,asante Mola ilisaidia na hakuwahi kuumwa tena.

NB: kuwa makini mchanganyiko wako usiingie machoni wakati wa kupakaa
Ahsante sana kwa maelezo ya Tiba,
Nateseka sana kwa kweli.
 
Acha nimeuguza mtu wa namna hii usiombee, anakwambia uchungu anaosikia ni kama wa kuzaa lakini Bora wa kuzaa mtu anategemea kupata mtoto unakuwa ni uchungu wa furaha lakini sio wa maumivu wa vidonda vya saratani hatari sana....
Pole na hongera kwa ustahimilivu na moyo wa kuuguza.
 
Kuna lile chango wanapita linaumaga hata usipokuwa Mp Yani [emoji23][emoji23][emoji23]nilikuwa natambaa tu [emoji23][emoji23] na kulala nimebinua Tako juu[emoji23][emoji23][emoji23] majirani walicheka badae nilivopona
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Poleee aunt, hukwenda kwa mtaalamu?
 
Mwaka 2018 mlango ulijibamiza ukanipiga kwenye kidole cha shahada,kumbuka mlango wa mninga halafu ni mkubwa,ilitakiwa uwe dabo, basi aisee kidole siku ya tatu yake kilivimba kikawa kinapwita balaa, nikaenda Rabbinnisia hospitl chumba cha upasuaji,kufika nawambia madaktari naitaji kukikata hiki kidole inaghalimu sh. Ngapi!? Aisee walicheka sana
 
Back
Top Bottom