Ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?

Ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?

nimeumwa jino, sikio, tumbo,.......nadiriki kusema bado maumivu yake hayafikii kwenye haya,....

1)-kupasuliwa korodani (nimeshuhudia kwa macho yangu , jamaa akipasuliwa)
2)-kuungua moto (from experience)
3)-kuvunjika mfupa....(nimeuguza mgonjwa)

nadiriki kusema hayo maumivu omba yakupitie mbali kabisa,....
Alipasuliwa pumbu kwa sababu gani mkuu🙌🙌
 
Hakuna maumivu yanayozidi KUFILISIKA KIUCHUMI, hayo mengine yote mwili unaweza kupambana...
 
Mgonjwa cancer ya tezidume anaposhindwa kukojoa anapowekewa ule mpira wa mkojo. Aisee usiombe kuona, ule mrija(catheter) una urefu zaidi ya futi moja, unene kama kalamu ya speedo unapenyezwa kwenye tundu la mboo hadi ufike kwenye kibofu cha mkojo. Narudia kusema usiombe kushuhudia ama yakukute.
Kuna shem wangu mmoja anapitia hapa baada ya kufanyiwa operation mbili ndo anauguza kidonda ili pasizibe
 
Kuna shem wangu mmoja anapitia hapa baada ya kufanyiwa operation mbili ndo anauguza kidonda ili pasizibe
Mungu amjalie uponyaji salama na mapema Mkuu. Kwanza maumivu ni anaposhindwa kukojoa baada ya tezi kuziba urethra na kuzuia mkojo usitoke nje. Mtu anabanwa na mkojo lkn hawez kukojoa, mkojo unaunguza kibofu ndani kwa ndani. Wanaume na wadau wa afya tunatakiwa kuelekeza jitihada za kukabiliana na changamoto ya tezi dume. Ana umri gani shem wako?
 
Mungu amjalie uponyaji salama na mapema Mkuu. Kwanza maumivu ni anaposhindwa kukojoa baada ya tezi kuziba urethra na kuzuia mkojo usitoke nje. Mtu anabanwa na mkojo lkn hawez kukojoa, mkojo unaunguza kibofu ndani kwa ndani. Wanaume na wadau wa afya tunatakiwa kuelekeza jitihada za kukabiliana na changamoto ya tezi dume. Ana umri gani shem wako?
65 i think. Amina kwa dua
 
Maumivu ya kuongozwa na wapumbavu wa sisiemu na yule mjalaana wao haya ni hatari sana hadi unakubali kuwa kufa ni kufa tu
 
Kila kiungo kinauma sana,ni kulingana tu na wakati gani umeumwa nini zaidi,
Ila tumbo kiboko
 
Wakuu habari za humu ndani.
Hivi ni maumivu gani makali zaidi ya mwili wa binadamu ushawahi ku experience au uliona mtu anapitia ukaona kabisa ni maumivu makali kwa binadamu.

Kwangu mimi ni maumivu ya tumbo,kuna siku niliwahi changanya pilipili kichaa na vitunguu swaumu nikabrend then nikanywa aisee maumivu niliyoyapata sitakuja kusahau.Niliona Israel huyu hapa kaja kunisalimia.Tumbo linauma asikuambie mtu.

Je ni ni maumivu gani makali zaidi ya mwili?
JINO
aisee hii nilishihudia kwa mwingine lakini aaah acha nilimuonea huruma huku nikishindwa kujizuia kucheka.

KUTEGUKA BEGA
Yale maumivu sitamani kuyakumbuka aisee, ilikuwa ukilala kuamka ni kipengele lazima utafute pozi la kuamka nalo ambalo angalau litapunguza uchungu wa maumivu. Nafikiri joint za bega ndo joint zinazoongoza kuwa na movement mwilini, usiombe maumivu yake.
 
Nilimshuhudia mume wangu akiumwa saratani ya ini maumivu aliyokuwa akiyapitia hayaelezeki ilifikia hatua hata dawa za maumivu hazifanyi kazi ni analia muda wote huu ugonjwa usikie tu usibishe hodi kwenye familia yako
Duuh polee sanaa mummy..

Vipi bro alipona?
 
Back
Top Bottom