Ni michezo gani ya hatari uliwahi kufanya ili utoboe kimaisha?

Kwa hizi code ulizotoa ni rahisi kudakwa labda kama uko nje ya nchi lakini mamlaka zikiamua hutoboi kama ulitumia majina yako halali ni rahisi kuku trace kupitia NIDA na I'd nyingine hata tu transaction za kibank wakizipiga pin ukienda TAWI lolote kuulizia kwanini account zangu ziko pinned jamaa wataitwa fasta kuja kukunyakua Sasa una ulinzi gani wa kutodakwa? Maana hata hao wenzako walioko ndani Kwa hayo mabilioni wakiminywa watakutaja tu mkuu.
 
We ni nyokoo kabisaa master unapiga mulemule kwenye government..
 
Nimeandika mara nne nikafuta. Ngoja nikae kimya tu mambo yasiwe mengi nikaja kupewa Economic case. Ila itoshe tu kusema uhaba wa maji Dar Es Salaam ulikuwa FURSA kubwa sana kwangu miaka ya 2011-2013.
 
Masamaki au?
 
hahahahaha nimecheka sana
 
Ndio nyie mlikua mnacheza na efd machine mnatoa risiti feki?
 
Mimi nilipewa kitengo cha logistics kwenye kampuni ninayokuwa nafanyia kazi. Muhindi aliniamini sana kwenye kutafuta bei nzuri ya kusafirisha mizigo za mazao kwenda Dar. Basi ukawa mwanya kwangu! Uzuri mzigo ulikuwa mwingi, niliwatafuta ma -transporter nikawapanga na kuongeza 300k kila gari bila muhindi kushtuka. Msimu ule tulisafirisha gari zaidi ya 100+ na kufanikiwa kupata 30M chapchap. Msimu ulifuata nikacheza tena nikabutua 24M. Msimu wa tatu wambea wakanichoma nikashtukiwa na kufukuzwa kazi.
Scenerio ya pili;
Niliajiriwa kama branch manager kanda za juu kusini. Basi nilikuwa mimi na mlinzi tu kwenye hiyo ofisi. Nikaanza kutengeneza majina ya vibarua hewa ili nipate pesa. Kama unavyojua vibarua wa less than 200k kwa mwezi hawaingii kwenye payrol hivyo nikawa nawalipia kupitia pettycash. Kila mwezi. Kila mwezi nikawa sikosi 1m mbali na mipigo mingine. Nilipata hiyo hela kwa miaka mitatu mfululizo baadaye nikaletewa watu kutoka makao makuu kama wasaidizi na mchongo ukafa. Ila hiyo hela ilinisaidia kujenga nyumba ninayoishi kwa sasa.

Baada ya mianya kubana nilihamia kwenye uwekezaji UTT then Hisa ndo mpaka saivi nipo huko. Dili haram zilikata so ziebaki ndogondogo za nadra.
 
We ndo mwanaume sasa 🙌 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…