Ni mkoa gani mzuri kwa kuanzia maisha from Zero?

Ni mkoa gani mzuri kwa kuanzia maisha from Zero?

Room30-40 fursa zipo nyingii kuuza matunda&mbogamboga, kuchukua mchele&chenga kyela&mbarali na kuuza town, kuna mishe za kuchoma viazi,nyama,kuna mishe za kuuza mitumba mwanjelwa kuna mishe za kulima mahindi&mpunga.
Shukrani sana kaka. Nimevutiwa
 
Mkuu, Dar kuna chumba cha bei hiyo? Mbona nilisikia maisha ni ghali sana huko?!
Maisha ya Dar yapo size tofauti.

Yapo ya ghali kweli kweli ushuani na yapo ya wa hali ya chini. Maeneo ya hali ya chini ndio yatakufaa kujibanza mkuu room zipo mpaka za 30 inategemea ni wapi tu aidha Mbagala, Tandale au Temeke
 
Maisha ya Dar yapo size tofauti.

Yapo ya ghali kweli kweli ushuani na yapo ya wa hali ya chini. Maeneo ya hali ya chini ndio yatakufaa kujibanza mkuu room zipo mpaka za 30 inategemea ni wapi tu aidha Mbagala, Tandale au Temeke
Ahsante kaka
 
mwezi ulopita nilikuwa mkoani Iringa , nilipita maeneo mengi ya mjini na baadhi ya vijiji wilayani kilolo nikaanza kushawishika kuishi huko kutokana na mandhari na fursa tofauti tofauti zilizopo , kwanza kabisa ukifika maeneo ya iringa mjini utaona kuwa kuna hakuna wafanya biashara wengi kama ilivyo mikoa mingine ,pili hata wafanya biashara walokuwepo maeneo tofauti tofauti wanafanya biashara zinazofanana

Niliona baadhi ya mitaa ambyo ni maarufu ikiwa na watu wengi wakitembea kutafuta mahitaji maeneo yao.nilianza kushawishika zaidi kufanya biashaa ya mavazi ,chakula na vinywaji kwa baadhi ya maeneo lakini pia niliona Iringa panafaa sana kwa mtu anaetafutamaisha au yule anaweanza kujitegemea .maana bei za nyumba za kupangani rahisi,bei za vyakula ni rahisi bei za mavazi zipo juu kidogo tofauti na dsm .

Binafsi nitarudi tena iringa nikiwa kama raia wa huko nikijishughulisha na biashara ndogo ndogo au hata biashara kubwa pia maana ukifika maeneo ya ilula unakaribishwa na matenga ya nyanya yakiuzwa kwa bei rahisi mno lakini cha ajabu ukiwa mjini nyanya unazipata soko kuu tu na wala huoni watu wakiuza bidhaa hiyo barabarani kama dsm ,ukifika mtela bwawani utakutana na wateja na wauzaji wa samaki wakitoa bwawani hapo wakisafirisha toka iringa kwenda mikoa mingine hapa tz,imani yangu ni kwamba ukiwa kwenye CHAIN VALUE ya hii biasharaya samaki hata ukiwa na tsh 50000 unatoboa , na pia ukipita barabara ya Iringa Dodoma utaona maeneo mengi na vijiji tofaiti tofauti lakini huwezi ona mtu auze soda ,maji au hata leso japo kuna maeneo mabasi na malori yanasimama kwa muda mrefu

nakushauri utembeehuko uone kama kutakufaa au jaribu kwenda mkoa mwingine na wa nyumbani kwako
 
Back
Top Bottom