mwezi ulopita nilikuwa mkoani Iringa , nilipita maeneo mengi ya mjini na baadhi ya vijiji wilayani kilolo nikaanza kushawishika kuishi huko kutokana na mandhari na fursa tofauti tofauti zilizopo , kwanza kabisa ukifika maeneo ya iringa mjini utaona kuwa kuna hakuna wafanya biashara wengi kama ilivyo mikoa mingine ,pili hata wafanya biashara walokuwepo maeneo tofauti tofauti wanafanya biashara zinazofanana
Niliona baadhi ya mitaa ambyo ni maarufu ikiwa na watu wengi wakitembea kutafuta mahitaji maeneo yao.nilianza kushawishika zaidi kufanya biashaa ya mavazi ,chakula na vinywaji kwa baadhi ya maeneo lakini pia niliona Iringa panafaa sana kwa mtu anaetafutamaisha au yule anaweanza kujitegemea .maana bei za nyumba za kupangani rahisi,bei za vyakula ni rahisi bei za mavazi zipo juu kidogo tofauti na dsm .
Binafsi nitarudi tena iringa nikiwa kama raia wa huko nikijishughulisha na biashara ndogo ndogo au hata biashara kubwa pia maana ukifika maeneo ya ilula unakaribishwa na matenga ya nyanya yakiuzwa kwa bei rahisi mno lakini cha ajabu ukiwa mjini nyanya unazipata soko kuu tu na wala huoni watu wakiuza bidhaa hiyo barabarani kama dsm ,ukifika mtela bwawani utakutana na wateja na wauzaji wa samaki wakitoa bwawani hapo wakisafirisha toka iringa kwenda mikoa mingine hapa tz,imani yangu ni kwamba ukiwa kwenye CHAIN VALUE ya hii biasharaya samaki hata ukiwa na tsh 50000 unatoboa , na pia ukipita barabara ya Iringa Dodoma utaona maeneo mengi na vijiji tofaiti tofauti lakini huwezi ona mtu auze soda ,maji au hata leso japo kuna maeneo mabasi na malori yanasimama kwa muda mrefu
nakushauri utembeehuko uone kama kutakufaa au jaribu kwenda mkoa mwingine na wa nyumbani kwako