Ni mkoa gani mzuri kwa kuanzia maisha from Zero?

Ni mkoa gani mzuri kwa kuanzia maisha from Zero?

Mwaka fulani mjini Morogoro alikuja jamaa mmoja toka Uganda, alivyo kuja mpaka kufika sijui.
Ila alikuja sehemu fulani kwenye mafundi wengi wa seremala, alipokelewa akawa anapewa kazi ya kupiga msasa furniture.
Alifanya shughuli hiyo kwa muda kidogo lakini akiwa na malengo, mpaka sasa ana maduka kadhaa ya kawaida na showroom ya Feniture.

Unaweza kwenda kwenye mji wowote ukatafuta hao mafundi, au hata mafundi ujenzi, mwanzoni itakua na changamoto kidogo lakini ukisha kaa sawa ndio inakua jumla.

Alie kushauri uende dar nami namuunga mkono.
Kila la heri.
 
Room za kaeaida( za hustlers) shingapi?! Na kwa mtaji huo naweza kudaka fursa gani?!
Chumba giza elf 20.Kwa wajanja wa mji uhitaji kupanga machimbo ni mengi box lako tu.But kupanga ni salama zaidi.
Fursa kwa mtaji huo unaweza laza elf 10 hadi 20 kwa siku kupitia biashara ndogo zinazodharaulika.Kuuza
Mishikaki,mahindi choma,kahawa,chai na tangawizi,machungwa,karanga,nk
 
Chumba giza elf 20.Kwa wajanja wa mji uhitaji kupanga machimbo ni mengi box lako tu.But kupanga ni salama zaidi.
Fursa kwa mtaji huo unaweza laza elf 10 hadi 20 kwa siku kupitia biashara ndogo zinazodharaulika.Kuuza
Mishikaki,mahindi choma,kahawa,chai na tangawizi,machungwa,karanga,nk
Shukrani sana mkuu
 
Wakuu habari za muda huu!

Baada ya kukaa nyumbani muda mrefu nikifanya kilimo cha kutegemea mvua, mwaka huu kilimo kimeniangusha sana na hata miaka iliyopita mara zote mavuno yalikuwa tofauti na matarajio hivyo nimeamua kuachana na kilimo kwani sioni hatima ya maisha yangu ikiwa tofauti na ya sasa. Unakuta mwaka wenye unafuu katika mavuno napata 160,000 nikiuza ( jasho la mwaka mzima ndiyo hilo).

Nimewaza nikaamua niende mjini nikajitume huwenda mambo yakawa nafuu baadaye.

Naomba ushauri wa mkoa mzuri wa kuanzia maisha from Zero. nina mtaji wa 200,000 na ni tofauti na nauli endapo nitapata uelekeo wa kwenda.

Pia naomba mchanganuo kwa mtaji huu naweza kufanya biashara gani japo sina uzoefu wa kufanya biashara yeyote au kwa mwenye kazi za kutumia nguvu naomba anipe. Tafadhali naombeni Msaada kwa hili na ahsanteni.
Nenda kiranjeranje lindi, panga chumba, nunua mbuzi 2 Anza biashara ya supu asbh na jioni,

Kisha uje na mrejesho
 
Room30-40 fursa zipo nyingii kuuza matunda&mbogamboga, kuchukua mchele&chenga kyela&mbarali na kuuza town, kuna mishe za kuchoma viazi,nyama,kuna mishe za kuuza mitumba mwanjelwa kuna mishe za kulima mahindi&mpunga.
Samahani mkuu. Ni wilaya gani kwa Mbeya inafanya vizuri kwenye kilimo?!
 
mwezi ulopita nilikuwa mkoani Iringa , nilipita maeneo mengi ya mjini na baadhi ya vijiji wilayani kilolo nikaanza kushawishika kuishi huko kutokana na mandhari na fursa tofauti tofauti zilizopo , kwanza kabisa ukifika maeneo ya iringa mjini utaona kuwa kuna hakuna wafanya biashara wengi kama ilivyo mikoa mingine ,pili hata wafanya biashara walokuwepo maeneo tofauti tofauti wanafanya biashara zinazofanana

Niliona baadhi ya mitaa ambyo ni maarufu ikiwa na watu wengi wakitembea kutafuta mahitaji maeneo yao.nilianza kushawishika zaidi kufanya biashaa ya mavazi ,chakula na vinywaji kwa baadhi ya maeneo lakini pia niliona Iringa panafaa sana kwa mtu anaetafutamaisha au yule anaweanza kujitegemea .maana bei za nyumba za kupangani rahisi,bei za vyakula ni rahisi bei za mavazi zipo juu kidogo tofauti na dsm .

Binafsi nitarudi tena iringa nikiwa kama raia wa huko nikijishughulisha na biashara ndogo ndogo au hata biashara kubwa pia maana ukifika maeneo ya ilula unakaribishwa na matenga ya nyanya yakiuzwa kwa bei rahisi mno lakini cha ajabu ukiwa mjini nyanya unazipata soko kuu tu na wala huoni watu wakiuza bidhaa hiyo barabarani kama dsm ,ukifika mtela bwawani utakutana na wateja na wauzaji wa samaki wakitoa bwawani hapo wakisafirisha toka iringa kwenda mikoa mingine hapa tz,imani yangu ni kwamba ukiwa kwenye CHAIN VALUE ya hii biasharaya samaki hata ukiwa na tsh 50000 unatoboa , na pia ukipita barabara ya Iringa Dodoma utaona maeneo mengi na vijiji tofaiti tofauti lakini huwezi ona mtu auze soda ,maji au hata leso japo kuna maeneo mabasi na malori yanasimama kwa muda mrefu

nakushauri utembeehuko uone kama kutakufaa au jaribu kwenda mkoa mwingine na wa nyumbani kwako
Ukiona hivyo jua shilingi ni ngumu kuipata.
 
Nenda kaisho mbeya hautakufa kwa njaa vyakula vya kimaskini bei chee sana, kama unaanza maisha pana kufaa, pesa yote unayo utaiwazia maendeleo tu hauta waza kula na pakulala kwa sababu kuna vyumba mpaka vya 20k [emoji15]
 
Nenda kaisho mbeya hautakufa kwa njaa vyakula vya kimaskini bei chee sana, kama unaanza maisha pana kufaa, pesa yote unayo utaiwazia maendeleo tu hauta waza kula na pakulala kwa sababu kuna vyumba mpaka vya 20k [emoji15]
Ahsante. Wilaya gani kwa mfano
 
Njoo arusha ukamate skygo nyekundu ni mwendo wa hesabu tu.
 
Back
Top Bottom