Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakuu habari za muda huu!
Baada ya kukaa nyumbani muda mrefu nikifanya kilimo cha kutegemea mvua, mwaka huu kilimo kimeniangusha sana na hata miaka iliyopita mara zote mavuno yalikuwa tofauti na matarajio hivyo nimeamua kuachana na kilimo kwani sioni hatima ya maisha yangu ikiwa tofauti na ya sasa. Unakuta mwaka wenye unafuu katika mavuno napata 160,000 nikiuza ( jasho la mwaka mzima ndiyo hilo).
Nimewaza nikaamua niende mjini nikajitume huwenda mambo yakawa nafuu baadaye.
Naomba ushauri wa mkoa mzuri wa kuanzia maisha from Zero. nina mtaji wa 200,000 na ni tofauti na nauli endapo nitapata uelekeo wa kwenda.
Pia naomba mchanganuo kwa mtaji huu naweza kufanya biashara gani japo sina uzoefu wa kufanya biashara yeyote au kwa mwenye kazi za kutumia nguvu naomba anipe. Tafadhali naombeni Msaada kwa hili na ahsanteni.
Shukrani sana mkuuNenda Dar, specific Mbagala stand au Temeke stereo tafuta connection na wasukuma toroli za mizigo zile ndogo. Tengeneza toroli kwa bajeti ya pesa yako. Endeleza harakati.
Nenda kwenye majiji yenye msongamano,
Dar (Mbagala, Temeke, K/koo), Mbeya (Mwanjelwa, Kabwe etc), Mwanza, Dodoma nk.
Nunua trey tatu za mayai hapa gharama kwa tray 7000 - 10000 kutegemea na msimu, sufuria kubwa yenye uwezo wa kuchemsha mayai mkaa, chumvi kisha ingia mtaani kuuza mayai ya kuchemsha. Ukizoea mji tafuta vijana wengine wasiojiongeza wabebeshe tray kadhaa na wewe utaanza kuwa muajiri.
All the best
Mkuu, Dar kuna chumba cha bei hiyo? Mbona nilisikia maisha ni ghali sana huko?!
Hakuna wezi kweli..?!
Same Sehem gan mkuu?Same
Popote utakapoamua unaweza kutoboa maisha hayana formula kikubwa imani usitegemee watu kukupa opinion za kweli kuhusu mji sahihi kutafuta maisha akili yako inapokwambia ndio hukohuko wish all the best
Dodoma kuna fursa gani mkuuMkuu njoo dodoma ujaribu bahati yako
Chumba cha 20k huku mburahati au manzese midiziniChumba mimi nimepanga nalipa kodi 20000 kwa mwezi.
Vyumba vipo kuanzia 15000 +
Anayesema eti maoni yangu ni "dagaa mchele" hajui kitu.
Wakati nafika mjini Nilipewa kazi ya kuhudumia kitimoto (napenda sana).
Kurunzi
Si huwa mnasemaga chsi kila uziNakumbuka uzi wako mi nilikuwa najua ni jokes tu za kujaza server za JF kumbe ilikuwa kweli big up sana
Kigamboni KibadaChumba cha 20k huku mburahati au manzese midizini