Ni mkoa gani mzuri kwa kuanzia maisha from Zero?

Mimi nakushauri njoo dar.
Mimi nimekuja mjini hapa na nauli tu, nimeshuka pale kwenye treni sina hata mia mbovu mfukoni,
Mbaya zaidi sikuwa na mwenyeji wa kunipokea au sehemu ya kufikia.
Ila kwa sasa nimepanga chumba changu fresh maisha yanaenda.
Nakukubali sana mwanangu...😜
 
tukutane kesho saa mbili asb kwa mkuu wa wilaya nilishanunua pete miaka miwili iliyopita we njoo na suti tu
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Wacha niende Karume kesho kulokota Esuti kwa Disii itakuwa keshokutwa sasa
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Wacha niende Karume kesho kulokota Esuti kwa Disii itakuwa keshokutwa sasa
Mkuu kesho kutwa mbali sana unaweza kubadilisha mawazo nitumie vipimo vyako naenda Kwa fundi sasa hivi
 
Iringa mjini maisha ni ghali kuliko dar
Amini usiamini

Afu hakuna fursa hapo labda ufanye biashara inayolenga wateja wanachuo coz kuna vyuo vingi sana

Ila vyuo vikifungwa iringa ni kama lindi tuu dadek
 
Nenda Mbeya kaishi Simike, Sokomatola au Ghana kwa wajane.

Kama ni Moshi kaishi Njoro.

Kama ni Dar Tandika, Vingunguti au Buguruni.

Iringa kaishi Kitanzini, Makorongoni. Frelimo au Kihodombi.

HIZO SEHEMU HATA VYUMBA VYA ELFU 7,10 AU 15 UNAPATA.
 
Sasa masta hapo, inabid uzungushe vitu mkononi, manake ununue vitu kwa wachina/ wahindi uzungushe... otherwise kutobos ni kipande sana kwa hiyo capital mzee...
Sasa usijeuliza ni vitu gani...
Mkoa unaweza chagua
1.Dar..japo mahitaji si mengi kivile
2.Tabora
3.Singida..vijijini... kama manyoni nk unaweza pambana

Kila la kher
 
Nakumbuka uzi wako mi nilikuwa najua ni jokes tu za kujaza server za JF kumbe ilikuwa kweli big up sana
Ile haikuwa Jokes hata kidogo mkuu.
watu wengi walijua mimi ni tapeli.
ila wachache walijitosa kunisaidia bila hata kunijua nitokako hasa.
walinisaidia freshi tu mpaka leo nalisukuma gurudumu la mihangaiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…