Ni msanii gani wa muziki Bongo ambaye tangu uanze kumsikia hujawahi muelewa kabisa?

Ni msanii gani wa muziki Bongo ambaye tangu uanze kumsikia hujawahi muelewa kabisa?

Duh! Ni vile naheshimu msimamo wako. Ila kumkataa AY inabidi uwe kauzu kama kitu gani sijui.

Ova
Nadhani kwa sababu AY huwa hatoi hits kwa muda mrefu tofauti na FA ambaye kila akirudi anasimamisha mji..

Ila AY nina nyimbo nyingi tu nazikubali, toka Raha tu, yule hadi point ya Zigo
 
Hii ni 10 bora ya watu ambao hawakupaswa kujihusisha na muziki kwa sababu ya kukosa vipaji;
1. Jux
2. Shilole
3. Wakazi
4. Queen Darlin
5. Madee
6. AY
7. Babalevo
8. Ali Kiba
9. Tundaman
10. Best Naso.
Mkuu dili na siasa mziki tuachie sisi vijana yaani unasema alikiba hakupaswa kujihusisha na mziki umekosea sana yaani sana
 
Kabisa umri unachangia hali hiyo sana uwezi kuwa unamuelewa lesi wanyika, msondo ngoma kama mzee wetu Grahams alafu uwaelewe fresh boys, billnas, kondeboy na wengineo.
Umewataja Les Wanyika pamoja na Msondo Ngoma Baba ya Muziki, umefanya nichukue miwani yangu niangalie mara mbili mbili picha ya mrembo mmoja niliyekutana naye Nairobi Mwaka 47 wakati tumeenda Disko (Club) kuziona hizo Bendi mbili 🤗

Those were days 🤗🙌
 
Mimi labda ninatatizo ila kiukweli AY sijawahi kumuelewa kabisa. Tangu nimeanza kumsikiliza wayback hajawahi kutoa ngoma nikaielewa kabisa. Labda ile Yuleee, nampenda sana jinsi alivyooo.... nayo kwa mbaali sana. Hata nikikutana nayo kwenye playlist ntaiskip tu.
Yule, changa la macho, ile ngoma aliimba na sauti soul wako jangwani, genda okole na yule mganda, ile ngoma ya raha tu na marehemu complex, inategemea na mtu aisee mkuu zama hizo usimwelewe AY kweli?
Mimi simwelewi young lunya nadhani si generation yangu, simwelewi sijui yamy, siwaelewi wasanii wengi kwa kweli maana wote wana taste the same
 
Hii ni 10 bora ya watu ambao hawakupaswa kujihusisha na muziki kwa sababu ya kukosa vipaji;
1. Jux
2. Shilole
3. Wakazi
4. Queen Darlin
5. Madee
6. AY
7. Babalevo
8. Ali Kiba
9. Tundaman
10. Best Naso.
Wewe utakuwa ni kijana wa miaka ya 70
 
Best naso hapana kwakweli, hizo hela anapeleka studio bora angekua anakula nyama choma ajenge shavu
😃😃😃😃😃😃😃Ila wasanii wa zamani kila mtu alikuwa na staili yake ya kipekee.
Kuna Crazy Gk,D knob,Kali P na yule mwingine jina nimemsahau aliimba nyimbo ya Nampenda bibi kikongwe hawa jamaa ilikuwa nikisikiliza nyimbo zao nilikuwa nacheka sana hadi nikawa addicted nazo bila ya kutarajia
 
2. D Voice & Mac Voice
Huyu bwana mi kuna wimbo wake mmoja tu ule kaimba singeli ndio ulivutia, tena sio wimbo wote, ni kakipande tu anaimba
"Haya dadaa tikisa kalio kalio kalio kariakooooo.
Wasio kua nalo na wenye ngongingo warushe rohoo"
😅😅😅.

NB
Mnisamehe kidogo, maana mi kuna time huwa napendaga vitu vya kijinga kijinga
 
Back
Top Bottom