Ni msanii gani wa muziki Bongo ambaye tangu uanze kumsikia hujawahi muelewa kabisa?

Ni msanii gani wa muziki Bongo ambaye tangu uanze kumsikia hujawahi muelewa kabisa?

Kuna yule mmoja alikuwa wateule na kina J moo na Mchizi mox.
Alikuwa anatoka na Shyrose Banji, aysee jamaa alikuwa hajui hadi anakera,

Unamzungumzia Jaffarai. Yule alikua anafanya kujifurahisha tu sio kwa ajili ya mafans.
 
😂 kwa umri huo bado unageuka? Sasa unageukia nini au ndio uzee mwisho ukipishana na wanaume.
Tangu tupewe maelekezo pale Eden kwamba Wanawake ni mapambo ya Dunia, siachi kuwaangalia

Mwana FA aliwahi kusema "Mimi na Mabinti damu damu...*

Baadaye Wazee tukatunga ule wimbo rangi ya chungwa kuendelea kusifu uumbaji 🤗
 
Tangu tupewe maelekezo pale Eden kwamba Wanawake ni mapambo ya Dunia, siachi kuwaangalia

Mwana FA aliwahi kusema "Mimi na Mabinti damu damu...*

Baadaye Wazee tukatunga ule wimbo rangi ya chungwa kuendelea kusifu uumbaji 🤗
Mkaimba na mapambio kabisa basi ndio maana wazee mnatuzidi kete vijana, maana kasi ya mabinti kupenda wazee ni kubwa mno.
 
😃😃😃😃😃😃😃Ila wasanii wa zamani kila mtu alikuwa na staili yake ya kipekee.
Kuna Crazy Gk,D knob,Kali P na yule mwingine jina nimemsahau aliimba nyimbo ya Nampenda bibi kikongwe hawa jamaa ilikuwa nikisikiliza nyimbo zao nilikuwa nacheka sana hadi nikawa addicted nazo bila ya kutarajia
GK nililipenda sana Goma lake Ntakufaje. Hadi leo nikilisikia linaclick medula.
D knob na sauti ya Gharama
Kali P na imekaa vibaya
Picco wa kikongwe ndo sikumuelewaga kabisa.
 
Nadhani kwa sababu AY huwa hatoi hits kwa muda mrefu tofauti na FA ambaye kila akirudi anasimamisha mji..

Ila AY nina nyimbo nyingi tu nazikubali, toka Raha tu, yule hadi point ya Zigo
There's something about FA aisee, binafsi sio shabiki yake, personality and stuff. ila nazipenda nyimbo zake zote, hata zile alizotoa nikiwa bado mdogo. Mi ni shabiki wa music wake at large.

Na ameonesha consistency kwenye hili, kila akiingia studio lazima atoe kitu kiende mjini!
 
GK nililipenda sana Goma lake Ntakufaje. Hadi leo nikilisikia linaclick medula.
D knob na sauti ya Gharama
Kali P na imekaa vibaya
Picco wa kikongwe ndo sikumuelewaga kabisa.
Hata mimi nilikuwa nazipenda hizo nyimbo na nyingine ya Gk inaitwa Ama zangu ama zao kuna mstari mmoja ilikuwa nikiusikia lazima nitabasamu huo mstari unasema"Watoto wadogo mkitoa nyimbo moja mnajiona wakina Pdiddy,pombe na nyinyi,mademu kibao" In king crazy Gk's voice😀😀😀
Pia kali p kwenye nyimbo yake ya imekaa vibaya hata sasa hivi niko nayo kwenye simu yangu kuna mistari yake miwili huwa nikiisikia naburudika sana na inachekesha anasema"Ilikaa vibaya ile siku tulivyomkamata mchina anayecheza kareti,hu ha master,mimi na yule polisi mwenzangu tukatoka nduki,kuanzia leo mie sio polisi tena,nimekuwa bwanyenye ona sasa watoto wananitania,salimia kiafande,aisee wewe,aisee wewe"in Kali P's voice😀😀😀😀😀
Huyo Piko hata mimi nilikuwa simuelewi sema tu ilikuwa nikisikia nyimbo yake inanitafakarisha tu na kujiuliza aliwaza nini kumpenda bibi kikongwe na wakati vijana wa umri wake wapo.
 
Back
Top Bottom