Ni kweli kabisa si kila ndoto ni ya kusimulia hasa hizi zenye maono,,na mfano mzuri tunaupata katika vitabu vitakatifu pale Yusuphu rehema na amani ziwe juu yake alipomwambia baba yake kuwa nimeota nyota 11 na mwezi vikinisujudia,baba yake akamwambia usiwaambie ndugu zako kwani shetani ataleta uadui kati yenu
Kwahiyo hayo mambo yapo,,na nyengine ni za maono
Binafsi huko nyuma nilikuwa sio mtu wa ibada,siku moja niliota malaika wamekuja kuchukua roho yangu ingawa sikuwaona lkn nilihisi uwepo wao karibu yangu,nikajuta sana na kutamani ningefanya ibada,wakachukua roho yangu na ikawa inapaa kwenda mbinguni,najiona kabisa napaa kwenda mara nikashtuka,nilitafakari sana na ukawa mwanzo wa kujikurubisha kufanya ibada,,,na kwa mujibu wa quran roho ikitoka kwanza chap inaenda kwa muumba kisha inarejeshwa kwa mhusika kaburini,kwahiyo nami niliota hivyo hivyo ndoto ikienda mbinguni,na ni sahihi sikuwaona malaika kwasababu ukifa ndio utawaona live kabisa