Ni muda sasa sijawahi kumbuka ndoto yoyote niliyoota

Ni muda sasa sijawahi kumbuka ndoto yoyote niliyoota

mi kila nachoota lazima kitokee napata taarifa na maelekezo kupitia ndoto
Hiyo ni kweli kabisa mkuu, hata mimiWakati wa nyuma nilikuwa na baadhi ya ndoto ambazo huwa kweli, ila sasa sijui nini kimetokea mpaka sikumbuki tena.
 
Iambie hakili yako.iache kisahau ndoto na itakuwa hivyo

Binafsi nikiota kitu lazima nikumbuke na lazima kitokee
 
Hiyo ni kweli kabisa mkuu, hata mimiWakati wa nyuma nilikuwa na baadhi ya ndoto ambazo huwa kweli, ila sasa sijui nini kimetokea mpaka sikumbuki tena.
hapo ndugu ushachezewa na wazee wa kamati sali sana upone kiroho
 
Last week kwa siku 2 mfululizo, nimeota niko mahala ,nina huzuni sana , nafanya maombi huku nalia kwa uchungu sana, nikashtuka ndotoni,ilikua saa 8 usiku, macho yamejaa machozi,moyo wangu mzito sana. Siku 2 mfululizo ndoto hii ya aina moja.
SIjui hii ina maana gani et Rabboni ?
Kwa muda huo ulioota kuna jambo linakwenda kukukuta, mida hiyo ndoto nyingi huwa za kweli... ongeza ibada kwa wingi na utoe swadaka sana!
 
Habari za asubuhi wadau

Kama kichwa cha habari kinavyo sema. Nina uhakika kila siku naota ndoto nikiwa usingizini, lakini cha ajabu ni kwamba nikiamka tu asubuhi sikumbuki ndoto hata moja.

Ni muda mrefu sina kumbukumbu ya ndoto yoyote ile, naota ndoto zaidi ya tatu lakini asubuhi ifikapo nikijaribu kukumbuka nashindwa.

Hili ni tatizo au ni hali ya kawaida tu? Ni zaidi ya miaka mitatu sasa nimekuwa na hali hii. Nifanye nini?
Kitendo cha kuota na kusahau, usikumbuke ulichoota wataalam wanasema ni dalili mbaya. Huenda watu wameshakuchezea muda mrefu... Kuna wataalam wa kuchungulia na kujua kesho yako itakuwa tamu kama kisheti, wakakumaliza mapema. Dalili ya kwanza ni kutokujua umeota nini, kupoteza kumbukumbu na kuhisi uzito kwenye kifua, pindi unavuta na kutoa pumzi, maumivu ya kichwa kwa mbali na kuhisi mwili hovyohovyo. Kama unaumwaumwa hivi...

Wanayajua hayo wakitambua vitu vichache binafsi kuhusu maisha yako, vifuatavyo:- "Tarehe ya kuzaliwa, mwezi na mwaka, siku uliyozaliwa, Jina la Mama, aina ya nyota na wakipata vitu muhimu kama kucha, nywele, unyayo na damu"

Watoto wetu huaribiwa mapema sana hasa na ndugu au watu wetu wa karibu utotoni mwao maana wanawawahi kuwachungulia mapema hasa wakiwa na akili angali wadogo, hasa performance ikiwa kali darasani. Unashangaa mtoto anashuka na kuishia kuwa teja... Mnaishia kulaumiana ni malezi au michezo, kumbe binadamu nao walishiriki kwenye counter-attack ya maisha ya mtoto.

Binadamu ni hatari sana!
 
Back
Top Bottom