Ndoto nyingi ni yale mambo unayoishi nayo kila wakati. Japo wengi wanazichukulia serious,lakini hata pale wanapozichukulia serious kwamba alichokiota kitatokea,hiyo inakuwa nadharia tu wakati hakitokei hata nusu yake,japo InabaKi kwenye Imani ya mhusika kwamba itatokea,mpaka anasahau kwamba imetokea au haijatokea.
Ukitaka kuikumbuka ndoto uliyoota ni rahisi tu ni kama vile unavyostuka mkojo ukikubana,basi unaweza kujitafuta kila wakati ukiota jilazimishe kuamka. Ukiweza kuamka kila wakati,usiamke kwa kama unastuka. Amka soft tu anza kuwaza ulivyokuwa usingizini ilazimishe akili ivute kumbukumbuku ndoto yako. Anza na tukio kubwa kubwa lililojirudia rudia kwenye ndoto yako. Mwisho utaweza kukumbuka ndoto zako. Japo sio muhimu. Mimi huwa nikiota ndoto mbaya najilazimisha sana niamke hata katikati ya ndoto. Ukija kulala huwezi kuota tena ile ile ndoto.