Ni muda sasa sijawahi kumbuka ndoto yoyote niliyoota

Mimi niliwahi kuota ndoto mara mbili, nikiwa kwenye ndoto nikajua kuwa hii ni ndoto dah nilifanya mambo ya ajabu ndotoni.!
 
Kwa muda huo ulioota kuna jambo linakwenda kukukuta, mida hiyo ndoto nyingi huwa za kweli... ongeza ibada kwa wingi na utoe swadaka sana!
JApo ningetaman unisaidie kufafanu zaid, lakin usimacho kinaweza kikawa kwel, maana siku ya 3 yake, nikashtuka tena usiku moyo/roho inauma sanaa, kesho yake ikatokea ile ajali ya mbeya (hii ya juzi hapa) and my blood brother alikua mmoja wapo wa waliokuwepo kwenye ajali ile, hali yake badi si nzuri yuko icu mpaka sasa.
Sina uhakika kama kuna connection na those 3 days of dreaming
 
Wewe Mungu amekuita katika utumishi muda sasa ila unakwepa kwepa,

Mungu anatutaka uingie katika shamba lake uvune Roho zilizopotea.

Hiyo ni huzuni ya Mungu Roho mtakatifu, huzuni ya kuwahurumia watenda dhambi Ili warudi kundini baada ya kutubu.

Kuhubiri INJILI ni KAZI yenye thamani kuliko KAZI yoyote duniani

UbarikiweπŸ™
 
Tatizo mimi nilishakengeuka, niliacha ibada kabisa. Nabak kusikiliza tu online preachers hii sijaacha.
 
Tatizo mimi nilishakengeuka, niliacha ibada kabisa. Nabak kusikiliza tu online preachers hii sijaacha.
Wala usijihukumu,

Mwana mpotevu pia alimwambia hivyo pia baba yake, kwamba sifai kuwa mwanao,

Mungu anapenda watu wa aina Yako wenye kujishusha na kujua kuwa wametenda dhambi na kupungukiwa utukufu,

Usijihukumu, tubu na Amini Mungu amekusamehe.

Mungu akubariki, endelea na kusoma neno, kuomba na kuabudu usiache Hadi utakapo sikia maelekezo ya wito.

Amen
 
Hii ilitokea kwa marehemu babu yangu.

Wakati akinipa wosia akaniambia: ... 'Mjukuu wangu siku zangu zimekaribia maana hata ndoto sioti siku hizi, na hii ni ishara kubwa ya kuukaribia umauti'... .

Sikumdadisi sana jambo hilo, ingawa kweli hakuchelewa kuaga dunia.

Jambo nisilolielewa ni kama kweli alikuwa haoti au alikuwa akiota na kusahau?
 
.....Sasa umejuaje uliota, na huku unasema hukumbuki?
Mfalme Nebuchadnezzar alitoa ndoto na kuisahau, akakumbuka kuwa alitoa ndoto ila kukumbuka ndio hakumbuki.

Ilibidi amtafute Daniel, akamwomba Mungu Kisha Ndoto Daniel akaambiwa ndoto aliyoota mfalme na tafsiri yake.
 
Nimetoa nimepoteza viatu,, yaani ndoto mbaya hii usiwah omba kuota
Kupoteza viatu ni kupoteza au kucheleweshwa hatua za kiuchumi, kiimani, kimahusiano nk nk

Omba Kwa bidii zaidi na zaidi Ili hatua zako ziongozwe na Mungu. Asiwepo mwenye kuzizuia.
 
Dah, mkuu sasa hapo unasababisha nikose amani kabisa
 
Kutokuota ndoto au kusahau ni hatua tata sana.

Si ya kupuuza.
 
Dah, mkuu sasa hapo unasababisha nikose amani kabisa
Kuwa na amani.
Babu yangu alikuwa ni kizee sana karibia miaka 100.

Wee bado kijana, yaweza kuwa ni fatique mwili unachoka saazingine kutokana na mazingira pamoja na kazi.

Tafuta ushauri kwa wataalamu wa saikolojia ama madaktari wa afya ya akili.
 
Mungu ni above all,

Huwezi muwekea mipaka. Unawezaje kujizuia kuvuta Pumzi ya uhai?

Ndio unaweza kumkataa asikuongoze, ila Bado atakuwepo kukupa kupumua Pumzi yake ya uhai Bure.
 
Anayedharau ndoto namuona hana maana kabisa,ndoto zina ujumbe,mke wangu mimi hawezi zini bila ya mimi kujua hadi mwenyewe anajishitukia,hawezi fanya chochote chenye mashaka kwangu bila ya mimi kujua,na hakuna jambo linakuja kwangu bila ya mimi kuliona kabla. Wife amewahi kutongozwa na jamaa wawili tofauti nikamwambia hadi na namba zao hakuamini wakati alifanya siri ,asante mungu wangu kwa hiki kipawa.


Mtoa mada njoo inbox nitakuelekeza dawa ya kienyeji ya kuoga kwa maji moto hali yako itarudi,hii ni bure sikuombi hata kumi.

Ila uwe usukumani,huku ndo inapatikana hiyo dawa

Bob Manson
 
Mkuu kwanza nashukuru kwa maelezo mazuri, nimejifunza kitu kutokana na uliyo yasema hapo Lakni sasa Mimi sipo usukumani nipo huku kwa wazaramo.
 
Kupoteza viatu ni kupoteza au kucheleweshwa hatua za kiuchumi, kiimani, kimahusiano nk nk

Omba Kwa bidii zaidi na zaidi Ili hatua zako ziongozwe na Mungu. Asiwepo mwenye kuzizuia.
na ndo imetokea patashika leo kazin aseeeee πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎ
 
πŸ˜‚πŸ˜‚Yan unaamka unatoka jasho na unauhakika ulikua kwenye varangati ila ndo hukumbuki kivipi ,,moyo upo mbio mbio yan
Hahaha hatari saana.
 
Mkuu kwanza nashukuru kwa maelezo mazuri, nimejifunza kitu kutokana na uliyo yasema hapo Lakni sasa Mimi sipo usukumani nipo huku kwa wazaramo.
Hakuna mabanda ya wale wauza dawa za kienyeji huko Darisalama yanayosimamiwa na wasukuma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…