Ni muda wa kuambiana ukweli. Sisi watu weusi hapa duniani tatizo letu ni nini?

Mambo ni mengi ila kwa kuweka kifupi katika mfumo ya nukta ni :

  • Ulemavu wa kushindwa kufikiri, ulemavu wa kuhoji,
  • ulemavu wa kutafuta suluhisho la jambo,
  • ulemavu wa kutegemea hisani / fadhila,
  • ulemavu wa kudhani matatizo yetu yatatatuliwa na wageni kutoka mabara ulaya, Mashariki ya kati, Marekani ya Kaskazini na Mashariki ya Mbali
  • na mwisho ulemavu wa kulilia kupendwa na wageni wa mabara mageni hapo juu.
  • Tutaweza kukubali maandamano kupinga uonevu, ukandamizaji na anasa za watawala
  • Sheria na katiba sahihi
  • N.k
Tukiweza kuondokana na upetevu huo hapo juu basi tutaweza kujenga reli wenyewe na miundo-mbinu mingine, tunaweza kuzuia mito ya maji kula kingo zake hivyo nyumba zetu zisibimoke, mipango miji / makazi itawezekana badala ya vichochoro na miji ya mabanda, tutauza magari yote ya viongozi wa taasisi za umma kama ma V8 yote ya vigogo kununua vifaa-tiba na kuanzia mfuko wa bima ya afya .....


Picha hapa chini kingo za mto mkubwa wa usiokauka mto Siene katika jiji la Paris unaopitisha meli za cruise


Picha hapa chini za kingo za mto mdogo tena wa msimu wa mto Gide kitongoji cha Ubungo jijini Dar es Salaam


Wanafunzi wa kitivo cha uhandisi chuo kikuu tajwa kongwe UDSM kwa kushirikiana na halmashauri ya Ubungo TAMISEMI wangeweza kutumia kodi za wananchi vizuri na wanafunzi wa UDSM kujifunza kwa vitendo kujenga kingo hatimaye majina yao kuingia ktk rekodi kumbukizi tukuka kuwa elimu imewezesha kutatua changamoto katika jamii .


Kifusi cha mchanga uliosombwa toka kingo za mto Msimbazi kikiwa kimechotwa na kuwekwa kando eneo la Jangwani DSM


Picha chini ufukwe wa Ocean Road barabara ya Barrack Obama jijini Dar es Salaam wenye mawimbi makubwa toka bahari ya Hindi yanayotishia kusababisha kumomonyoka kwa ardhi na barabara pembezoni mwa bahari ukiimarishwa na kunakishiwa vibaraza vya kutembelea

 
Hatari
 
Shida yetu ni tabia tu hakuna kingine. Hatupendi kazi na kujituma. Pia tuna wawazia wezetu mabaya zaidi kuliko mazuri
 
Wachina kiuchumi wameanza kupiga hatua kubwa juzi tu hapa baada ya Deng Xiaoping kuwafungua macho.

Na hata baada ya Deng Xiaoping, unaangalia mafanikio ya China mijini tu, China ni kubwa sana na ina watu wengi sana masikini, hata kama wengine wengi wametolewa kwenye umasikini.

Let's look at GDP per capita for perspective.

GDP per capita ya China ni $12,556 (2021)

Kwa mwaka huo Seychelles ilikuwa na GDP per capita ya $14,653 . Maana yake Seychelles nchi ya Afrika iliipita China kwenye GDP per capita as recently as 2021.

Mchina aligundua njia za kuja Africa kabla ya Mreno, na angeweza kufaidika kwa kufanya hata biashara tu, kama si utumwa.

Ila, Mfalme wa China akakataza watu wa China kutoka nje. Kwa falsafa hizo hizo za kujiona wao ndio zaidi na wao wana maadili zaidi.

Biashara yenye faida kubwa haiendani na maadili, inabidi uchague biashara yenye faida kubwa au maadili.
 
Uchawa ni moja ya kitu cha hovyo kinachokua kwa kasi sana
 
Sawa
 
Haya ni matatizo yetu kwa asilimia kubwa
 
Shida yetu ni tabia tu hakuna kingine. Hatupendi kazi na kujituma. Pia tuna wawazia wezetu mabaya zaidi kuliko mazuri
Ni kweli sisi hatufanyi kazi au kuna shida nyingine zaidi
 
Waafrika wacha tuendelee kuwa wangese tu sababu nchi kama tz sasa hivi mitandao inajadili mimba ya dada anayeitwa Paula,
Achilia mbali watoto wa shule wanatangaziwa kesho hakuna masomo wote muelekee sehemu fulan kumlaki kiongozi kuweka shazi mkutanoni,
Mtoa mada unataka ujilinganishe na binadam wa bara lipi?
 
Ni mazingira tunayoishi
Cha ajabu huyo mtu mweusi akienda kuishi mazingira ya watu weupe, na hii nimeiona Ulaya na US, simaanishi kwenda tu kuishi sehemu yeyeto, bali kuishi kwenye neighbourhood zilizojaa wazungu tu(wa hali ya kati sio wale masikini) wanabadilika, hata watoto wanatasoma shule kwa bidii kutokana nna shule watazoenda, japo kutakuwa na changamoto ya ubaguzi, lakini watoto wata thrive sana kimaendeleo yao binafsi kulinganisha kama wakienda kuishi neighbourhood zilizojaa foreigners wenzao( Mexican, Blacks, Indian and so so).
 
Ki uchumi wote hatuwezi kuwa wajanja uchumi utayumba inabidi wawepo wajanja wachache na mafala wengi
 
Sidhani maadili ya wachina kwa kiasi kikubwa yamebadilika maana hadi leo hawapendi kujihusisha na migogoro na masuala ya mataifa mengine zaidi ya China yao.

Wachina ni watu wanaojitazama wao zaidi na hali zao na wanajihukumu kwa historia yao wenyewe ni watu ambao historia yao ya jamii yao ndio inayo waendesha sio foreign influence.

Na kipindi hicho mchina anapuuzia biashara ya utumwa pwani ya Afrika mashariki na kuondoka zake licha ya kuwa mtu wa mwanzo hakuwa taifa masikini alikuwa moja ya taifa tajiri duniani na aliushika uchumi wa dunia kwa asilimia zake China kaja kunyong'onyea huku baadae kabisa ndipo akavamiwa.

Tamaduni hizo za wachina hazijaweza kuwa kizuizi wao kukanyaga hatua kubwa tena ukiongeza na ukomunisti unao onekana ni kama mfumo fulani wa kizembe lakini kwa China haikua hivyo.

China limekuwa taifa la kiviwanda kwa kiasi kikubwa chini ya ukomunisti wa Mao huku kwetu ilifeli na viwanda kufa, China chini ya ukomunisti wa Mao walienda mchakamchaka haswa pasipo kujali madhara ya baadhi ya sera kufail.

So, China utamaduni na ukomunisti wao kwao haujawa mzigo kwao ila kwetu imeonekana mzigo why
 
Inasikitisha
 
Watu weusi wanaoishi marekani ndio walijazana magerezani wale ni watu wa hovyo kupindukia
 
Tatizo la Afrika ni viongozi. Wengi ni wabinafsi kupindukia hawana maono yoyote ya kukwamua nchi zao ndiyo maana hakuna kinachofanikiwa kusini mwa jangwa la sahara
 
Unaangalia chumi kutoka kwa relativistic lens.

China kaanza kugundua mabaruti na marisasi na ma silaha, mashine za kuandika miaka mingi sana kabla ya Ulaya.

Kwa hivyo, China ndiye alitakiwa kutawala dunia nzima, yani unavyoona huu ufalme wa Uingereza na Marekani katika biashara ya dunia, kama China asingekuwa na hizo qualms, China ndiye alitakiwa awe kinara wao wote hao kiuchumi. Na dunia nzima badala ya kuongea Kiingerwza tungekuwa tunaongea Kichina.

Kwanza wao wengi, pili wana utamaduni mrefu wa ugunduzi na teknolojia.

Ila, utamaduni wa maadili yao ya kutoingilia watu wa nje ndio uliowaharibia nafasi ya kuongoza biashara.

Yani wao waliijua njia ya biashara kabla ya wazungu, wakaja Africa wakachukua wanyama, wakapeleka China. Halafu Mfalme wao akapiga stop watu kutoka nje.

Yani hayo mafanikio ya China unayoyaona leo ukiyapigia mahesabu yalivyotakiwa kuwa kama wasingekuwa na hayo maadili ya Confucianism, yalitakiwa kuwa mara nyingi sana kupita mafanikio yao ya leo.

Na hata hayo mafanikio yao ya leo unayaangalia kwa udogo tu, kama nilivyosema awali, kiuchumi China haijaifikia hata Seychelles kwenye GDP per capita.

Tuongee namba, si hisia.

Kuna wachumi wanakwambia kama hujafikisha GDP per capita ya $25,000 bado nchi yako ni kati ya nchi zinazoendelea, si zilizoendelea.

IMF bado inaiita China an "emergind and developing country" as opposed to "developed country".

 
Viongozi hawataki demokrasia Africa tutaendelea vipi? zaidi ya kuibiana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…