Unaandika kama vike "watu weusi" wa Marekani wameachiwa tu waendelee wanavyotaka.
"Watu weusi" wa Marekani wana historia ndefu iliyo complicated. Naona mara nyingi kuwalaumu bila nuance ni "blaming the victim".
Kuna mfumo ulikaa rasmi kukandamiza watu weusi wowote watakaoanza kuendelea pamoja kama kundi la watu Marekani
Kuna "watu weusi" waligundua mafuta huko Tulsa Oklahoma, wazungu wabaguzi wakaja kuwawekea nongwa na kuwaharibia biashara zao.
Sasa hao naonutasema ni wa ovyo?
Kuna kina Martin Luther King na Malcolm X walikuwa wanapigania haki za watu weusi, wakaukiwa. Hao nao utasema ni watu wa ovyo?
Sisemi kwamba hakuna "watu weusi" wa ovyo, hao wapo kila sehemu. Tatizo tukija kwa weusi tuna generalize sana.
Soma historia ya Tulsa race massacre.
en.wikipedia.org