Nje ya mitandao ya kijamii na baadhi ya wasomi, Magufuli anakubalika na wengi nvhini, hasa vijijini ambako kura nyingi ndiko zinakotoka. Waathirika wa sera za Magufuli ni elites pekee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jisomee kidogo Historia na vitendo vya madikteta wote duniani. Huwa wanajificha kwenye kivuli cha kutetea wanyonge na maskini lakini ndani yao wote ni mashetani kabisa. Soma adolf Hitler alivyofanya na makuli na kuwashiriksha kwenye jeshi. Idd Amin Dada Nduli aliwagawia maskini maduka ya wahindi. Na huyu unamuonaje?
 
Upo sahihi lakini kwa maoni yangu niliona CDM wenyewe hawawezi kufanya hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Who told you serikali inaungwa mkono na watu wengi ? And then stop your Hippocratic unachambua wazi Uko upande wa serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Deep down kila mtu mwenye akili timamu anajua ni nani wanahusika. Hata wauaji wenyewe wajijua.
 
Spot on, Sir.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wale waliotaka kumuua Dk. Ulimboka walijulikana? Ingawa siamini kama walitaka kumuua bali kumyamazisha na wamefanikawa.

Huenda hata kwa Lisu ni kwa kusudi la kumnyamazisha tu, je watafanikiwa? Will Lisu bow?

Vv
 
Point nzuri sana.

Lissu ameshambuliwa saa 7 mchana. Hivi simu zote hizi mitaani hakuna hata mtu mmoja aliepata picha kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wengi watamchagua basi atashinda hata kama elites watamuona dikteta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taifa liko katika mapito makali ya vita ya kiuchumi.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania yuko katika mapambano makali dhidi ya wezi na wahujumu uchumi,vita hivi ni ndani ya chama chake,ndani ya nchi yake,ndani ya washindani wa nchi za maziwa makuu na kwa upekee yupo kwenye vita na mabepari na wakoloni wa zamani na wakoloni mamboleo.

Wakati akipokea ripoti za wizi unaotokea kwenye makanikia mheshimiwa Rais alitahadharisha juu ya ugumu wa vita hii.

Ukiacha kutahadharisha juu ya usalama wa wajumbe wa kamati Mh Rais alitsahadharisha kuhusu usalama wake mwenyewe na of course usalama wa watanzania wazalendo.

Katika mapokeo ya tukio lililomkumba ndugu yetu na mtanzania mwenzetu ni vyema tukawa na mapokeo ya aina zote ambayo kati ya hayo moja tu ndio litakuwa sahihi baada ya uchunguzi.

Huu sio wakati wa kutukana,kuhemuka,kulaumu au kujiapiza bali ni wakati ambao watanzania wote bila kujali itikadi kutulia na kutafakari kwa kina sana.

Zipo conspirancy theiories kadhaa ambazo inatakiwa tuzimulike kabla ya kuja na misimamo mikali ambayo haitasaidia kujua ukweli wa jambo hili na hataonesha upendo au majonzi yetu ya dhati kwa Mh Lissu.

1-Tundu lissu alikuwa ni maarufu kwa kupinga sera za Rais Magufuli na CCM na ameingia kwenye migongano kadhaa iliyoko mahakamani dhidi ya Serikali ya CCM pengine hata kabla Magufuli hajaingia madarakani.

2-Tundu lissu alikuwa ni mwanaharakati wa mazingira haswa katika uharibufu wa mazingira katika maeneo ya migodini na ameandika articles nyingi dhidi ya wachimbaji wa madini wa kutoka ughaibuni.

3-Tundu lissu ni mwanasheria kitaaluma na amesaidia wengi katika kesi mbalimbali na amewaumiza wengi kwa maana hii katika kesi mbalimbali.

4-Tundu lissu kwa weledi wake katika sheria anaweza kuwa ni asset muhimu ya serikali kitaifa na kimataifa kama leo tulivyoelezwa na mheshimiwa Rais kuhusu professa Mruma.

5-Tundu lissu ni mwanaChadema 'asili' ambaye potentially angeweza kuwa mgombea urais 2015 au hata 2020.pia anaweza kuwa bado ni mkereketwa halisi wa vita dhidi ya ufisadi na aliyeamua kupingana na ufisadi ndani ya Chama chake.

6-Tundu lissu kwa weledi wake anaweza kuwa ni muajiriwa wa makampuni ya uwekezaji katika madini ambayo kwa sasa yapo kwenye mgogoro mkubwa na Serikali au pengine yako kwenye mgogoro au ushindani mkubwa kati yao wenyewe.

7-Tundu lissu ni mwanafamilia ambaye ana mke na watoto na hivyo huwezi kumuondoa kwenye migogoro ya kawaida ya kifamilia.

8-Tundu lissu ni mbunge ambaye kwa level za kibongo ni tajiri kwa kiasi chake kiasi cha kuvutia majambazi wanaoweza kuhotaji mali zake.

9-Tanzania ni nchi salama na thabiti kisiasa ambayo inaweza kuwa under attack ili tu ionekane hakuna amani nchini mwetu.

10-Tundu lissu sio exceptional kwa vichaa tu wenye hamu za kuchukua uhai wa watu hasa hasa watu maarufu kwa sababu za kuwapendezesha watu hao.

Kwa ufupi zipo theories nyingi zinazoweza kutujulusha kwa nini shambulio hili kwa mheshimiwa lissu limetokea .

Tujadili kitaalamu kwa kila mwanaJF na utaalamu wake wakati tukisubiri ripoti za vyombo vya ulinzi na usalama.

Mada hii ijadiliwe kwa weledi zaidi kuliko mohemuko au itikadi zetu za kisiasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…