Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act)

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.

1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu

Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.
Umechambua vzr na kwa weledi, nimefikiri zaidi namba 4

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1)Mtoto kumdanganya mtoto mwenzie tunasema mtoto anacheza
2)mtoto kumdanganya mtu mzima tunasema mtoto anakua
3)Lakini mtu mzima kumdanganya mtu mzma mwenzake kuna walakini
 
Kwa tukio hili la leo naamini kabisa hata wabaya wake ndani ya chama chake WANAWEZA kushiriki uovu huu.
Tayari imasemekana kuna makundi yanayomuona mjaruhiwa kama tishio ndani ya chama kwa chaguzi zijazo 2020 na 2025.

Tusubiri uchunguzi unaoendelea.
Acheni siasa uchwara,pambaneni na aibu hii.Msifikiri wa TZ wa leo ni wa miaka ya 60s.watu wanajielewa.Unafkiri unaweza kutuokota kibashite namna hii?..Idiot.

In this world,It doesn't matter who you are,But what you do to Survive.
 
Hivi si alisema kuna watu walikuwa wanamfuatilia na gari Toyota Premio akawakaba na kisha akamuonya IGP? Huko Dodoma ameshindwa kuwakaba? au Wanaume wale wa Dar ndio waliwezekana na Wa Mikoani kawashindwa?
 
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act)

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.

1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.
Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.
Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.
Mkuu habari za siku!,
Kwa kiasi kikubwa nakubaliana na ww ila pia naomba kupingana na ww!.
Dhana zote zinaweza kuwa valid na zikawa invalid.

Me naomba kuangalia dhana ya serikali.
Toka mwaka unaanza kumekuwa na matukio mengi ya serikali au vyombo vyake kuonekana kwenye makashi kashi ya uharifu na siraha ki ujumla
Mifano ni mingi,tukianzia kwa clauds fm watu wameingia na siraha na mpk leo clouds wanasema ila haikuwa social visit,Nape kutolewa bastola,office za IMMA kuvamiwa na watu wenye mavazi ya askari,akina roma kutekwa. Na mengine mengi ila kwa kiwango kikubwa hao waharifu they manage to get away with it!.
Kipindi cha nyuma akina Ulimboka na hao watu hawakupatikana

Kwa ambao wanafahamu uwezo wa jeshi au usalama kwenye kukusanya habari na ku deal na uharifu mkubwa au organized crime we are real good.na tunaheshimika saana huko kwenye jamii ya inteligency, ila kwa matukio ya uhalifu wa siku hizi kuna external force na watu wanaweza to get away with it!.

Kuna kitu ambacho huwa kina hamasisha jamii kuwa ya kiharifu.na haya matukio yakiendelea yatasababisha mafia au waharifu wa kimataifa kuona kumbe TZ unaweza l
Kufanya uharifu na ku get away with it!.
Neo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa tukio hili la leo naamini kabisa hata wabaya wake ndani ya chama chake WANAWEZA kushiriki uovu huu.
Tayari imasemekana kuna makundi yanayomuona mjaruhiwa kama tishio ndani ya chama kwa chaguzi zijazo 2020 na 2025.

Tusubiri uchunguzi unaoendelea.
Tundu lisu hana mbaya wake ndani ya chama.mawazo hayo mnatakakumkingia bwana Faru
 
Hakuna sababu yoyote inayoweza ku-justify kupigwa risasi Lissu!! huu Ni unyama wa hali ya juu!!
 
Nje ya mitandao ya kijamii na baadhi ya wasomi, Magufuli anakubalika na wengi nvhini, hasa vijijini ambako kura nyingi ndiko zinakotoka. Waathirika wa sera za Magufuli ni elites pekee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua kabisa kuwa unailazimisha na kuidanganya nafsi yako kuwa anapendwa na majority ya wapigakura hasa wa vijijini! Haiyumkini wewe ndio twaweza na tafiti zile zisizokuwa na sampling ni zako. Jibu unalo sasa kuwa wewe na wateule wenzako ndii mmebaki upande huo japo wengi wenu mmebakizwa na matumbo yenu yasiyojaa!
Na kwa hoja hii my instinct never lies to me kuwa you know something but unataka kujua kama kuna anayejua zaidi yako? Psychologically written ideas can lead to the facts alizonazo mtu. And you lead us to the truth and facts na eti unatuuliza swali ambalo majibu yake unayo na wahusika unawajua! Tuambie ni kwanini leo na sio juzi wala jana?
 
I will also go for no 2 ila kauli za mkulu dhidi ya TL zinaweza kuwa precipitating factor. Kunasehemu nimeandika kwamba very likely kuna kikundi kinachofanya huu uhalifu nje ya awareness ya serikali wakidhani wanasaidia serikali iliyopo. Kumbuka bomu ofisi za IMMA, bomu nyumbani kwa shehe, na pengine hata uvamiz clouds fm. Are they Tanzanians, Tanzanians + foreigners, imported foreigners? ??
Nadhan ni watu wa wabaya tuu pengine ni private contractors,deep state,au renegade unit ina operate nje ya kamandi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada naona una rukia kuwashutumu hao uliowaita "maadui" Wa Lissu!
Lakini nikukumbushe kwamba kwenye siasa za Dunia hii lolote laweza kutokea!! Hata Marafiki wake, nao Ni wa kuwachunguza!!
Rafiki wakati mwingine ana nafasi kubwa ya kufanya maovu halafu akanyooshewa vidole adui ambaye hakuhusika!! Hii ipo sana kwenye siasa za dunia hii!!
 
Hakuna sababu yoyote inayoweza ku-justify kupigwa risasi Lissu!! huu Ni unyama wa hali ya juu!!

TL amejiitahidi sana kufundiisha somo la UDIKTETA........!!!
Baada ya tukio hili nina hakika somo linaziidi kueleweka na kupendwa na Wanafunzi...!!!
 
Back
Top Bottom