Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
Ungeweka na 5. Inawezekana washambuliaji wakatoka cdm yenyewe katika mpambano wa kugombea mgombea urais wao 2020.
6. Washambuliaji kutoka huko huko cdm ili kuichonganisha serikali na wananchi?
Hili suala ni gumu sana linachohitaji ni kusubiri uchunguzi wa vyombo vya usalama tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unasema ni gumu but at the same time unapiga ramli chonganishi eti ni cdm.
 
Get well soon mh. Lisu. Wewe mtoa mada unapaswa isaidie upelelezi, hoja yako inautetezi mwepesi mno ktk dhana mojawapo . Unaleta propaganda hasi.
 
Nimefuatilia maoni ya watu mbalimbali katika mitandao yakijamii kunabaadhi ya watu tayari wameshajitwika mzigo wa vyombo vya dola. Wanatoa kauli za ajabu Sana ebu watanzania tuviachie vyombo vya usalama vifanye kazi yake. Pia niwasihi watanzania wenzangu tuache kutumia mitandao ya kijamii vibaya. Utakuta mtu mwingine anatoa maneno ya ajabu utafikiri Kama wale Jamaa wanaotukana huku wakiwa ng'ambo Ni vitu hatari Sana.
 
Kuna kiongozi mmoja mkubwa kipindi anakabidhiwa report fulani aliongelea kwamba kuna adui anatakiwa kupewa adhabu ya kifo.

Sent from my Priceless H40-D00 using JamiiForums mobile app
 
Hivi si alisema kuna watu walikuwa wanamfuatilia na gari Toyota Premio akawakaba na kisha akamuonya IGP? Huko Dodoma ameshindwa kuwakaba? au Wanaume wale wa Dar ndio waliwezekana na Wa Mikoani kawashindwa?
Huu ulikuwa ni mpango uliosukwa (conspiracy).

Nadhani unahusisha mtandao hatari sana. Ningekuwa na madaraka watu kama Mbowe, Mdee, Bulaya, Msigwa, na wengineo wangepatiwa ulinzi mkali mpaka hiki kijulikane.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kadri muda unavyozd kwenda waelewa tunazd kupata majibu
..haiwezeakani Ccm hili swala mlivalie kibwebwe namna hiiiii....
Ni kama wanajishtukia hivi..Mara rais,Mara pole pole ajikanyage ktk barua pa pole ya August,na mabango ya kujitetea mengi mitandaoni kote...
Watu washaelewa ukweli na kupitia hili nimepata jibu kuwa watanzania wanawapenda wapinzani kwa dhati...maana TZ nzima imezzma na watu wamesikitishwa sana na tukio hili...kwa dhati na si fos za watu....
Wito wangu kwa watanzania ni tushikamane hivi hivi mpaka 2020 tuking'oe hiki kidubwana uchwara na ccm yake
 
Nimefuatilia maoni ya watu mbalimbali katika mitandao yakijamii kunabaadhi ya watu tayari wameshajitwika mzigo wa vyombo vya dola. Wanatoa kauli za ajabu Sana ebu watanzania tuviachie vyombo vya usalama vifanye kazi yake. Pia niwasihi watanzania wenzangu tuache kutumia mitandao ya kijamii vibaya. Utakuta mtu mwingine anatoa maneno ya ajabu utafikiri Kama wale Jamaa wanaotukana huku wakiwa ng'ambo Ni vitu hatari Sana.
Huna sababu ya maana kuanzisha uzi huu. Unatupotezea muda tu. Mengi yameshasemwa kupitia mada zingine.
 
Nje ya mitandao ya kijamii na baadhi ya wasomi, Magufuli anakubalika na wengi nvhini, hasa vijijini ambako kura nyingi ndiko zinakotoka. Waathirika wa sera za Magufuli ni elites pekee.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndugu acha kudanganya watu humu....

Mimi niko kijijini kabisa huku Shinyanga tena kwa wasukuma wenzake huyu Magufuli wako.....

Kama unabisha uliza vijiji vya Tinde, Mwakitolyo, Busanda Mwamashimba, Kizumbi nk viko wapi....

Ukikuta watu kumi, ni mmoja ama wawili pekee ndiyo wanamuunga mkono Rais wako tena kwa kigezo cha ukabila tu (msukuma mwenzao) ni si kwa sbb nyingine iwayo yoyote !!

So, you are just deceiving yourself..... Unaandika tu ukiwa umejifungia kwenye chumba cha kujifichia hapo Lumumba badala ya kwenda kijijini kweli ukafanye utafiti......
 
Lissu ana maadui wengi, tuondoe dhana ya kusema kuwa ccm ndiyo ilitaka kumuua. Siasa ni mchezo mchafu, usikute kabisa ni marafiki zake wanaomchukia ama wabunge wenzake wa chadema wasiompenda Lissu. Pia inaweza kabisa kuwa hata mawakili wenzake wanao ona kuwa wanafunikwa na kick azipatazo. In short, Lissu alijijengea maadui ndani ya chama chake, serikali, na wananchi kwa ujumla. Anything is possible na I am not pointing fingers at anyone ila najuwa fika kuwa....waliotaka kumuua Lissu wanaweza kuwa watu wa karibu sana wenye chuki naye au tu walihamua kumsaliti ili afutike kwa maslahi yao wenyewe because hakuna mtu anafanya kitu bila kuwa na valid reason.
 
Huwezi kumzuia binadamu kuhisi jambo, na kila binadamu huwa na hisia. Hisia huletwa na ishara au dalili. Na hisia za kweli huzaa ukweli.

Mleta mada wewe una hisi nani anahusika?
Unadhani kwa nini watu wengi wanahisi mhusika ni yuleee?
 
Mkuu habari za siku!,
Kwa kiasi kikubwa nakubaliana na ww ila pia naomba kupingana na ww!.
Dhana zote zinaweza kuwa valid na zikawa invalid.

Me naomba kuangalia dhana ya serikali.
Toka mwaka unaanza kumekuwa na matukio mengi ya serikali au vyombo vyake kuonekana kwenye makashi kashi ya uharifu na siraha ki ujumla
Mifano ni mingi,tukianzia kwa clauds fm watu wameingia na siraha na mpk leo clouds wanasema ila haikuwa social visit,Nape kutolewa bastola,office za IMMA kuvamiwa na watu wenye mavazi ya askari,akina roma kutekwa. Na mengine mengi ila kwa kiwango kikubwa hao waharifu they manage to get away with it!.
Kipindi cha nyuma akina Ulimboka na hao watu hawakupatikana

Kwa ambao wanafahamu uwezo wa jeshi au usalama kwenye kukusanya habari na ku deal na uharifu mkubwa au organized crime we are real good.na tunaheshimika saana huko kwenye jamii ya inteligency, ila kwa matukio ya uhalifu wa siku hizi kuna external force na watu wanaweza to get away with it!.

Kuna kitu ambacho huwa kina hamasisha jamii kuwa ya kiharifu.na haya matukio yakiendelea yatasababisha mafia au waharifu wa kimataifa kuona kumbe TZ unaweza l
Kufanya uharifu na ku get away with it!.
Neo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari za siku nzuri mkuu. Tutakutana si muda mrefu kwenye jukwaa letu lisilokuwa na mizengwe.

Wazo la serikali kuhusika lilinijia kwanza. Lakini baada ya kufikiria kidogo nikaona halileti maana. Wakifanya hivyo watakuwa wamewapa ushindi wa kirahisi CDM ifikapo 2020. They will have shot themselves in the foot. They are not that dumb.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lissu ana maadui wengi, tuondoe dhana ya kusema kuwa ccm ndiyo ilitaka kumuua. Siasa ni mchezo mchafu, usikute kabisa ni marafiki zake wanaomchukia ama wabunge wenzake wa chadema wasiompenda Lissu. Pia inaweza kabisa kuwa hata mawakili wenzake wanao ona kuwa wanafunikwa na kick azipatazo. In short, Lissu alijijengea maadui ndani ya chama chake, serikali, na wananchi kwa ujumla. Anything is possible na I am not pointing fingers at anyone ila najuwa fika kuwa....waliotaka kumuua Lissu wanaweza kuwa watu wa karibu sana wenye chuki naye au tu walihamua kumsaliti ili afutike kwa maslahi yao wenyewe because hakuna mtu anafanya kitu bila kuwa na valid reason.
ondoa hilo neno "valid"
 
Huu ulikuwa ni mpango uliosukwa (conspiracy).

Nadhani unahusisha mtandao hatari sana. Ningekuwa na madaraka watu kama Mbowe, Mdee, Bulaya, Msigwa, na wengineo wangepatiwa ulinzi mkali mpaka hiki kijulikane.

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana ni wale Wastaafu nini? they knew kwamba wao ni next Target ya Magu na Tundu ndio anachokonoa balaa kama moto wa BOMU la Bwana Kiduku
 
Wanaowindwa kwa risasi, ni wengi sana kuliko wawindaji. Siku wanaowindwa watasema basi imetosha, ndio mtajua kuwa nguvu ya umma haijawahi kushindwa hapa duniani. Tumefikia hata mkusanyiko wa watu hospitali nao unakatazwa watu wasimjulie hali Tundu Lissu? Wakati utajibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom