Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act)

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.


1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.
Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.
Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.

None of the above! Ni vita ya uchumi!!! Mind u
 
Unajua kabisa kuwa unailazimisha na kuidanganya nafsi yako kuwa anapendwa na majority ya wapigakura hasa wa vijijini! Haiyumkini wewe ndio twaweza na tafiti zile zisizokuwa na sampling ni zako. Jibu unalo sasa kuwa wewe na wateule wenzako ndii mmebaki upande huo japo wengi wenu mmebakizwa na matumbo yenu yasiyojaa!
Na kwa hoja hii my instinct never lies to me kuwa you know something but unataka kujua kama kuna anayejua zaidi yako? Psychologically written ideas can lead to the facts alizonazo mtu. And you lead us to the truth and facts na eti unatuuliza swali ambalo majibu yake unayo na wahusika unawajua! Tuambie ni kwanini leo na sio juzi wala jana?
You are giving me too much credit than I deserve. I am very shallow.

Kama Magufuli hapendwi na wengi basi upinzani hawana cha kuhofu, 2020 inanukia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivyo vyombo husika lini vilikuja na majibu sahihi kuhusu matukio ya upinzani ukweli inaujua ila unaamua kujitilisha huruma tu
 
Hivi how come Taifa Zima linasikiliza habari za wizi wa Almasi, halafu ghafla bin vuup linatokea tukio la kutaka kumuassasinste kiongozi maarufu, hivi hii haiwezi kuwa ni Strategy ya Mabepari wa Almasi kujaribu kuzuia mjadala wa wizi wa Almasi usiende viral, na pia vyombo vya kimataifa visiripoti move ya serikali kuhusu madini hayo ili kulinda shares za Makampuni yao zisishuke.
Yaani Hii assasination attempt how possible can it be a coincidence na Ripoti ya Almasi kusomwa mbele ya president?

Mabepari yana mbinu nyingi za kublackmail serikali mbalimbali, au hata kutengeneza mazingira serikali zichukiwe na kisha ziangushwe kama zisipotii matakwa yao!!
 
Nimefuatilia maoni ya watu mbalimbali katika mitandao yakijamii kunabaadhi ya watu tayari wameshajitwika mzigo wa vyombo vya dola. Wanatoa kauli za ajabu Sana ebu watanzania tuviachie vyombo vya usalama vifanye kazi yake. Pia niwasihi watanzania wenzangu tuache kutumia mitandao ya kijamii vibaya. Utakuta mtu mwingine anatoa maneno ya ajabu utafikiri Kama wale Jamaa wanaotukana huku wakiwa ng'ambo Ni vitu hatari Sana.

Bensanane yuko wapi????

Waliomwagia tindikali kubenea wako wapi??

Waliomngoa kucha na meno Ulimboka wako wapi??

Walimteka mzee wa zimbabwe wako wapi??

Walioshambulia Absalom kibanda wako wapi???

Waliomua dr... Wako wapi??

Walio mtishia Nape Bastola wako wapi???

Walioshambulia CUF buguruni wako wapi??

Huu ni mchezo unaopangwa na watu wenye nia yao.
 
Uchambuzi wako na hypothesis zako ni nzuri sana, ila umesahau kitu kimoja tu, je silaha zilizotumika kumshambulia ni za aina gani? Je hao raia wa kawaida wanaruhusiwa kua nazo? Je Lissu ni wa kwanza kua mwiba kwa serikali? Je umaarufu wake kwa kuisumbua serikali unazidi wa Mrema na Dr. Slaa?
Asante kwa mchango wako.

Kuhusu silaha unaweza kusema majambazi wengi tu siku hizi wanazo SMG/AK47.

Lakini hizo points nyingine ni nzuri sana na sikuziainisha. Nisaidie basi mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
You are giving me too much credit than I deserve. I am very shallow.

Kama Magufuli hapendwi na wengi basi upinzani hawana cha kuhofu, 2020 inanukia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes you're too low. Kwasababu wao hawana cha kupoteza hivyo mwenye cha kupoteza ana hofu ya kupotelewa ndio maana anakilinda kwa mitutu! Uacheni uwanja huru na refa huru muone mtakavyopoteana dimbani na hapo ndipo utakapojua maana ya elite bila kamusi!
Waswahili husema, " ukiufunga sana mlango utalala nje "! Usemi huu upo karibu kutimia.
 
Yaani Hii assasination attempt how possible can it be a coincidence na Ripoti ya Almasi kusomwa mbele ya president?

Mabepari yana mbinu nyingi za kublackmail serikali mbalimbali, au hata kutengeneza mazingira serikali zichukiwe na kisha ziangushwe kama zisipotii matakwa yao!!

Kazi mojawapo ya idara ya Usalama wa Taifa ni kudetect na kuprevent threat to our national security.

Haihitaji mtu kuwa na akili sana kuelewa kwa hali ya siasa ya sasa ikitokea Lisu akashambuliwa watu watainyooshea vidole Serikali.

Hii ni kwa sababu Lisu ashasema idara hii inamfuatilia na inataka kumdhuru. Pia, anakwaruzana na Magufuli openly. Hii ni sababu nyingine kwa nini jambo lolote lile likitokea juu yake Serikali inanyooshewa vidole.

Sasa Rais anapotangaza kwamba yupo kwenye vita ya uchumi, vyombo vya usalama vinapaswa kuhakikisha hakuna "mzungu" anayekuja kumdhuru Lisu ili kuichonganisha Serikali.

Hivyo alipaswa kuwa chini ya uangalizi. Isitoshe kama mzungu anatoka nje na kuweza kufanya hili basi hatupo salama. Hii inaonyesha failure kwa vyombo vyetu.

Failure hii si mara moja bali mara mbili. Kushindwa kutambua hatari na pia kushindwa kuzuia hatari.

Jambo lingine unalohoji kuhusu hii coincidence ya kusoma ripoti na Lisu kupigwa risasi. Unasahau hizi ripoti si tu zinawachafua hawa wazungu bali hata serikali zilizopita.

Je, inawezekana watu kutoka hizi Serikali zilizopita hawapendi kuchafuliwa na sasa wameamua kuhamisha upepo? Hii pia ni moja ya scenario.

Lakini haya matokeo ya kuteka watu na kutolea bastola watu si mapya sasa.

Kabla ya kunyooshea vidole hao wazungu tujiangalie na sisi kwanza kama tu wasafi.
 
..hakuna jambazi wala kibaka atakayetaka kumuua Lissu usiku hata akiwa anatembea...achilia mbali mchana kweupe.....maana yeye ni mtetezi wa wote hawa....waliotaka kumuua Lissu wametumwa...jambo la kujiuliza ni nani waliwatuma???.....tuanze na ujambazi wa bashite Dar uliopita bila kuadhibiwa....ama wale waliomtolea silaha nape...ama kumteka roma....tuanzie hapa....jibu ndipo lilipo....kama watu wanatishia wenzao silaha bila kuadhibiwa...kwanini tusifikiri ndio waliomchapa risasi lissu???
 
Back
Top Bottom