Kote ulikuwa unavuta the main points zako

Umejaribu kuzungukaa weee kumbe sababu kubwa ni dhana namba 5
 
Mkuu kumbe BAVICHA walipeleka baruwa kwa IGP na DCI kuripoti kutishiwa kwa Lissu tarehe 24 Aug., 2017.

Hii ni kufuatia taarifa ya mkutano wao wa hadhara. Soma uzi huu.

IGP aanikwa kumbe Lissu aliripoti kuwindwa, Walinzi waliondolewa, askari wanaolinda spika na mawaziri walijifungia
 
Kote ulikuwa unavuta the main points zako

Umejaribu kuzungukaa weee kumbe sababu kubwa ni dhana namba 5
Unapoweka dhana (theories) unapaswa kuwa mkamilifu (exhaustive).

Unapaswa kuweka kila kitu hata kama utakuja kikanusha baadae, kama ilivyokuwa kwa dhana namba 1.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hili la lissu wahusika wanajulikana kama uchunguzi utafanyika huru.....
 
Kwahiyo ndio upo kwenye utafiti su umetuletea mrejesho wa utafiti wako?
Hapana.

Nilichofanya ni kuorodhesha makundi yote ambayo yangetaka kumuua Lissu. Katika kila dhana nimetoa maoni yangu kama kundi linahusika au la. Haya maoni yangu yalikuwa kama chachu tu. Nilitegemea wachangiaji wafanye yafuatayo:

1. Kuongeza dhana nyingine nilizozisahau.

2. Kupanua zaidi au kuponda maoni niliyoyaainisha.

3. Kutoa maelezo yao ya kina kuhusu dhana zote.

Mpaka sasa ninaweza kutoa muhtasari kama ifuatavyo kutokana na maoni ya wachangiaji. Sitajumuisha matusi, kejeli, na utoto uliomwagwa:

(a) Kuna wengi wanafikiri serikali imehusika (dhana no. 3) na shambulio la Lissu.

Kwa maoni yangu hawa watu wenye mawazo haya wanaonekana kuwa na mihemuko zaidi na hawatoi maelezo ya kimatiki (logical reasoning) kwa nini Serikali ilitaka Lissu afe. Hawakuorodhesha faida au hasara kwa Serikali kama Lissu akifa.

(b) Kundi kubwa la pili ni la wale wanaodhani watu wanaoichukia serikali wanahusika. Kwamba wanataka Lissu afe, serikali ishutumiwe na mauwaji hayo ili waweze kumuondoa Magufuli ifikapo 2020.

Hawa wachangiaji wanajumuisha dhana no. 4 na 5. Kiukweli huwezi kutofautisha sana kati ya dhana no. 4 na no. 5. Hii ndio maana niliamua kuiorodhesha dhana no. 5 kirefu. Hili kundi linaonekana kutoa sababu za msingi na zinazoweza kuaminika kwa nini dhana no. 4 au 5 zina mashiko.

(c) Kundi la mwisho na dogo zaidi ni wale wanaodhani wapenzi wa serikali (sio serikali yenyewe) wanaomchukia Lissu wamehusika na hili shambulizi. Hii ni dhana no. 2.

Ukiniuliza mimi nipo wapi basi nipo kundi la pili (b). Hasa nalalia dhana no. 4 lakini sitashangaa kama dhana no. 5 inahusika.

Sijui kama nimekujibu.
 
Kuripoti tishio la kuuawa hawawezi kuripoti BAVICHA; anaripoti mhusika. Kila ukiripoti ni lazima polisi wakuulize unamtilia shaka nani? BAVICHA hawawezi kujibu hilo swali itakuwa ni heresay. Je, kwa nini Lissu mwenyewe hakuripoti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli sina majibu ya maswali yako. Mimi nilileta taarifa zilizowekwa kwenye bandiko lingine nikitumaini zitasaidia mjadala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchambuzi wako ni wa kisiasa zaidi, mojakwamoja umeegemea upande wawashika dola, kifupi hujachambua ila umekuja kutudhihirishia unasema nini, kwanz umeonesha ni mwanasiasa moja kwa moja tena wa
 
Serikali hii haipendwi na watanzania bali watu wanaidshi kwa Uoga wanaogopa visasi kukomoana kubambikiana kesi, serikali ya CCM hawajawahi kujibu hoja kwa hoja za Lisu bali hutumia polisiccm kumtisha kumnyanyasa kumsachi nyumbani kwake, kutaka kumpima mkojo ili abambikiwe kesi za unga nk, nyie CCM na serikali yenu humukuwa mkifahamu watanzania wanampenda Lisu kiasi hiki, mlidhani Lisu hana watu lakini baada ya jaribio la kumuua kukwama mmetambua kuwa wapo watanzania wengi pamoja na mataifa mengi yanamuunga mkono na huko kenya anapotibiwa amepewa Ulinzi mkubwa na matibabu bora chini ya uangalizi mkubwa sana, kwa taarifa yako ingawa umekuja na story ndefu sana mtuhumiwa namba mija ni Bashite, Le mutuz na wenzako kadhaa hilo halina ubishi na wananchi wengi ndivyo wanajua.
 
Uchambuzi wako ni wa kisiasa zaidi, mojakwamoja umeegemea upande wawashika dola, kifupi hujachambua ila umekuja kutudhihirishia unasema nini, kwanz umeonesha ni mwanasiasa moja kwa moja tena wa
Nimeweka maoni yangu kama chachu na sio neno la mwisho.

Lengo hapa ni kuwa watu kama wewe mje mkosoe au muunge mkono maoni yangu. Lakini hasa nilitegemea wachambuzi walete dhana mbadala na kuelezea kwa nini wanafikiria dhana zao zina mashiko. Hii ndio ilikuwa dhamira ya bandiko langu.

Kwa mfano, sikuitetea serikali katika dhana no.3 bali nimeeleza sababu zangu kwa nini nilifikiri dhana ile ni potofu. Nilitegemea mtu mwengine aje atoe mdahalo wake unaoelezea kwa nini serikali ilitaka kumuua Lissu.

Mijadala ya Great-Thinkers ndivyo inavyoendeshwa hivi. Ni malumbano na kila mmoja anatoa hoja zake. Mimi nikisema hoja hii ndio sahihi ni lazima nitoe maelezo ya kuwashawishi wengine. Asiekubaliana na mimi nae anakuja na hoja zake mbadala mpaka tunakubaliana au tunakubaliana kutokukubaliana.

Samahani kama ulifikiri mimi ndie mwenye majibu yote. Ningemjua aliefanya unyama huu ningekimbilia polisi badala ya kuja JF.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana ni kweli hakwenda polisi kuomba ulinzi, badala yake akaitisha press conference na kijipigia debe la kisiasa.
Polisi ndiyo wanatumika kuwabambikia kesi chadema kila siku nani aombe Ulinzi wao?
 
mada ndefu huwa ngumu wengi kuzisoma, kwa kifupi tambua kuwa serikali hii ya kibabe kidikteta huwa haipendi kukosolewa ama kuonyeshwa udhaifu wake wa kiutendaji imekuwa ikimunyanyasa Lisu kupitia Polisiccm pindi akiwakosoa kila mtanzania analijua hilo.
 
Mimi sina chama bali ninaunga mkono juhudi za serikali hii. Hapo nyuma nilimshambulia sana Lissu kwa hoja zake potofu dhidi ya serikali hii. Hoja zote za Lissu dhidi ya serikali hii ni nyepesi sana na zinajibika kirahisi. Serikali haina haja ya kumuua kwa sababu hana hoja nzito. Nitarudia tena hapa:

Lete hoja yoyote ile ya Lissu dhidi ya serikali hii na nitaijibu hapa, sasa hivi.

Na kwa taarifa yako mimi sio msemaji au muajiriwa wa serikali.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ukosoaji gani wa Lissu kwa serikali unaotaka niuelezee kwa nini haukufuatwa. Lete hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja zipo nyingi na si nyepesi hivyo labda ujibu kwa kudhani unavyofikiri ndilo jibu, Zipo wapi zile bilion 251 zilipotea wizara ya ujenzi kwa kuwalipa makandarasi hewa? Vipo wapi vyeti vya Bashite mshauri mkuu wa Mtukufu? Yupo wapi Ben sanane aliyehoji PhD feki ya mtukufu, ? Ujenzi wa uwanja wa ndege chato, ununuzi wa ndege kwa cash vilibalikiwa na Bunge? Tenda za ununuzi na ujenzi zilitangazwa wapi? Na bei ya ndege ni bei halisi? Zipo wapi zile nyumba za serikali alizojiuzia Mtukufu akagawa kwa mdogo wake na ingine kwa hawala yake ambao hawakuwa watumishi wa umma? Nakupa hayo machche kwanza maana Hoja ni nyingi na maswali ni mengi sana.
 
Ni ukosoaji gani wa Lissu kwa serikali unaotaka niuelezee kwa nini haukufuatwa. Lete hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
tokea 1998 lisu alipiga kelele juu ya mikataba mibovu ya uwekaji na Mtukufu alikuwa waziri kipindi hicho na wabunge wa CCM wakapitisha mikataba hiyo leo hii Mtukufu anajidai kupiga kelele kana kwamba hakuwa sehemu ya waliopitisha mikataba mibovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…