herikipaji
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 1,198
- 1,369
Tunakumbuka September 7, 2017 ndugu Tundu Lissu akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge alipigwa risasi nyingi na kujeruhiwa vibaya.
Tukio lile la kikatili na kimafia lazima kuendelea kulikemea na kulaani vikali kwa kila binadamu mwenye akili timamu.
Lakini kulaani na kukemea tu kwa maneno matupu au kuandika tu mitandaoni haitoshi, ili kuepuka kujirudia rudia kwa matukio kama haya ni lazima wale wahusika wajulikane na kuletwa kwenye hukumu ya haki ili kuwajibika.
Haya matukio yanajirudia rudia baada ya muda fulani sababu tu hakuna anayepata kuwajibika na yataendelea kutokea sana yani watu watazidi kuumia na kuteseka bila kuwadhibiti watesi.
Hao watesi wanajua vizuri na wengine walishazungumza waziwazi ati Watanzania wengi ni "malofa na wapumbavu" na huu umekua mtaji wao mkubwa.
Tuko na kazi ya kuwathibitishia sisi Watanzania siyo wajinga kama wanavyofikiri.
Sasa naomba turudi September 7, 2017 tujiulize ni nani aliyempiga risasi Tundu Lissu?
Ni vizuri kama unapatikana ushahidi hii yote ni kueza kuwafamu wahusika wa matukio na mauaji ya waso hatia.