Ni nani alitaka kumuua Tundu Lissu?
Wameipata ile gari iliyopaki viwanja vya bunge kisha kumfuatilia Lissu na kumshambulia?

Maswali yako yana arrogance ile ile ya "kurara nao mbere"

Sasa huoni kama watakuomba uwasaidie kuipata hiyo gari ambayo hadi sasa haijulikani ilipo pamoja na udogo wa Dodoma?
 
Kumbe na wewe una ubongo wa kuku!

Bora wa kuku hali wa hauwi vifaranga wake anawatunza kwa upendo.

Kuliko ubongo wa baba yako anauwa ma-genius wote wa Taifa hili libaki la malofa, wajinga na wapumbafu kama wewe...kila jambo ndiyooooooo
 
Unaongea mambo ya kuchonganisha na UCHOCHEZI.Je Ikiwa leo wewe utakamatwa na Polisi na wakuulize UWASASAIDIE katika upelelezi WAO ili UUDHIBITISHIE Umma kuwa Mh Rais Magufuli ALIHUSIKA.Nina maswali mawili:
1.Je UTABITISHA?
Maana hamna mtu aliye na RUHUSA awe ni nani ya kutoa uhai wa mtu mwingine.
2. Je Polisi Wakikukamata ili KUKUHOJI utasema WAMEKUONEA?

ACHA kutuletea mambo ya vijiweni na uongo wa MITANDAONI.
Tuviachieni vyombo vya dola vifanye upelelezi wake ili GARI husika LIKAMATWE na wahusika WAKAMATWE. Hata kama ni NANI?

Magufuli HAJATUMA watu WAMTETEE yeye kwa KUVUNJA sheria za nchi na kuua watu.
Waliofanya hayo ni WAHALIFU wakubwa sana.
Kila mtu ABEBE MSALABA wake.
Message ndiyo hiyo kila mtu mitaani anajua hivyo, nyie mrukeruke tu lakini ndio kuiva kwa 'maharage' wenye akili watajua nilichomaanisha.
 
Kama hoja za TL zinaweza kujibika bila risasi, je, ni hoja ngapi alizozitoa dhidi ya serikali zilizojibiwa bila kutumia maguvu?
 
Vyovyote vile mtakavyolazimisha ila ukweli utatamalaki, always ukweli huwa haulazimishwi kama mnavyolazimisha uongo kuwa ukweli, mtashindwa kama mlivyoshindwa jaribio lenu la kumuua Lissu.
mtanyooka tu na kufuata msitari taratibu!
 
I believe your pics where misplaced, The topic was about a fellow Tanzanian who was gunned down by Terrorists. While we all grieving the last thing anyone here wanted to see is pictures of someone boarding helicopters.

Mind we are also proud to see a fellow Tanzanian offering a helping in a distant land, but that should have been in separate post, where by we could be congradualatimg you for a good deed.

.

On the issue of the names you have been called should never bother you . You are what u are , and nobody can change that, hiyo jitihada uliyofanya mpaka kufika hapo ulipo inaonyesha uhodari, umakini na juhudi ya kutaka kujiendeleza

Sent using Jamii Forums mobile app

Correction I am a US Citizen not a Tanzanian, Nilizaliwa Tanzania
 
Nasema "alietaka kumuua" kwa sababu ukiangalia yale matundu ya risasi upande wake wa gari utajua kuwa hawa watu hawakutaka kumtishia tu. Walidhamiria kumuua.

Niungane na Watanzania wenzangu kumuombea Tundu Lissu dua/sala ili apone kikamilifu, Amin.

Nimejiuliza maswali mengi kuhusu shambulio hili la kipekee kwa mbunge (sijui kama kulikwishatokea shambulio jingine kama hili), hapa Tanzania.

Yafuatayo ni malumbano ya kifikra ndani ya nafsi yangu kuwa ni nani hawa waliotaka Tundu Lissu afe. Maoni yako yanahusika, tafadhal.

Nimefikiria wahusika katika dhana 4. Nitazichambua hizi dhana moja moja.

Dhana zenyewe ni hizi. Washambuliaji ni:

1. Vichaa fulani tu. (Random act)

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.

3. Serikali yenyewe

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.


1. Vichaa fulani tu. (Random act)
Hii inawezekana lakini inakinzana na taarifa za kuwa Lissu alikuwa anafuatiliwa na magari kwa kipindi kirefu. Huu mpango ulisukwa na pia walijua wanaemtaka hadi kumfuata mpaka nyumbani kwake. Sidhani hii ilikuwa ni Random Act. Dhana hii ni potofu.

2. Raia wenye chuki na Lissu kwa kuikalia kooni serikali.
Hii inawezekana kabisa. Wengi walimshutumu Lissu kwa kupinga sera zote za serikali (mimi nikiwa mmojawao). Kuna watu walikwenda mbali zaidi na kusema wanataka serikali iwaruhusu wamuue. Ndio maana kuna umuhimu wa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu hawa.

Katika demokrasia watu tunashambuliana vikali kwa hoja na sio kwa kuumizana au kuuana. Kama hii itathibitika, basi kuna umuhimu wa kuwapatia ulinzi wanasiasa machachari wanaoibua hisia kali.

Kuna uwezekano mkubwa dhana hii ni sahihi.

3. Serikali yenyewe
Kuna watu mitandaoni wanadhani ni serikali yenyewe ndio imeunda hii mbinu ya kumuua Lissu ili awaondolee kelele. Wengi wanasema Lissu amefichua siri nyingi za serikali kufikia kuwa tishio kwa hii serikali.

Kwa maoni yangu huu ni upuuzi. Serikali hii inakubaliwa na watanzania wengi. Hoja karibuni zote alizotoa Lissu dhidi ya serikali zinaweza kujibiwa kirahisi sana. In fact, baadhi ya shutuma za Lissu zinaipaisha serikali kwa Watanzania. Kelele za Lissu zinaweza kuwa baraka (blessing) kwa CCM ifikapo 2020. Kumuua Lissu kutajenga hisia za uonevu na kuwaonea huruma CDM ifikapo uchaguzi mkuu. Serikali haiwezi kufanya kosa hilo.

Kwa hiyo dhana hii ni potofu

4. Watu wenye chuki na serikali (false-flag attack) ili waisingizie serikali uovu huu.
Hii dhana inahusisha watu wanaoichukia serikali (sio lazima wapinzani, inaweza kuwa watu wa nje) wanaotaka kumuondoa Rais Magufuli madarakani ifikapo 2020 kwa kuihusisha serikali yake na mauaji ya Lissu.

Serikali ya Magufuli imeathiri maslahi ya watu wengi sana wa ndani na wa nje. Akiendelea hivi hivi ana uhakika kabisa wa kupita ifikapo 2020. Sasa utaitoaje hii serikali madarakani ifikapo 2020. Jenga chuki kwayo.

Kama nilivyoeleza kwenye dhana namba 3, watu wakiamini kuwa serikali imemuua Lissu kinyama basi watawaonea huruma CDM na kuichukia CCM. CDM watachukua dola ifikapo 2020.

Je ni nani hawa wanaotaka kufanya unyama kama huu na kuisingizia serikali ya CCM (false-flag attack)?

Nina dhana nyingine 2 au 3 hivi (mfano, internal politics within CDM) lakini ni za pembeni sana na uwezekano wake ni karibu na sifuri. Kwa sasa hayo ndio malumbano yanayoendelea kichwani mwangu.

Please tell me I am not crazy.

This is how Criminals are pinned, they like to Go out of their way to explain, distance themselves from the crime n by doing so they further incriminate themselves!
 
article-2150824-134775C2000005DC-452_472x325.jpg

Kama kuna kitu kinatia wasi wasi katika jamii hivi sasa, ni awa "Watu wasiojulikana".
Hii ni murder squad, kwa hali yoyote ile.

Wasi wasi unaojitokeza ni kwamba , sasa msemo ule wa kisiasa unaohimiza mshikamano ati ya wananchi, unaelekea kufa rasmi.
Namkumbuka sana mzee Rashid Kawawa alivyokuwa akihimiza mshikamano.
bastola-520x245.jpg


Dalili za hawa watu wasiojulikana umeanza siku nyigi.
Lakini katika kutaka kushambuliwa Nape pale St Peter, na serikali bado haijampata yule "mtu asiyejulikana" akishika bastola , inatia shaka.
Ni dhahiri kila mtu anaye culprit moyoni, lakini serikali inabidi iwatie nguvuni hao " watu wasiojulikana" kabla taswira ya nchi haijachafuliwa Zaidi kwa kuendekeza hizi murder squads.
 
Eti "watu wasiojulikana" halafu wenye dhamana ya kuhakikisha wanakamatwa wamekaa tu maofisini na manishani na mabeji makubwa makubwa mabegani na vifuani! Kubali mmeshindwa kazi na mjipime sio kutuletea hadithi hizo hizo kila leo!
 
This is how Criminals are pinned, they like to Go out of their way to explain, distance themselves from the crime n by doing so they further incriminate themselves!
You worry about yourself, Sir. I wouldn't give advices to criminals in TZ if I were you. Just enjoy your life in the States.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm,bado napata ukakasi tu,lisu anaishi sehemu au karibu na naibu spika,vilevile ni jiran na mawaziri.hv eneo hili halina ulinz,hili ni swali la kwanza linalonipa shida,swali la pili,hawa waliofanya tukio hilo walikua wanajiamin nini,kufanya shambuliz kwenye eneo nyeti kama hilo wanaloishi viongoz.najua mlio wa risasi unanguvu sana na unaweza ukasafiri mita kadhaa,Mashaka yangu hapa,yaan inaanza kupingwa risasi ya kwanza,ya pili,ya tatu na kuendelea mpaka 32,taarifa zinakua hazijafika polisi tu,mpaka waharifu wanakimbia.na la mwisho intelijinsia ya polisi ikoje kama tundu lisu halishasema mbele ya uma kuna watu wanafatilia kwa wiki zaidi ya tatu.mwenye majibu naomba anisaidiae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uache upuuzi umetumwa na umejaribu kujificha lakini unaegememea upande waliokutuma kwenye mambo kama hayo hakuna kisichowezekana tanzania sio kisiwa na duniani haya hayajaanza leo WANASIASA MASHUHURI NA WAUPINZANI KUUWAWA NA ZINAZOSADIKIWA KUWA NI SERIKALI MI NAJUA YOTE YANAWEZEKANA ILA KUNA PROBABILITY YA ASILIMIA TOFAUTI KWA KILA KUNDI SASA KWA WEWE LILE ULILONYIM,A NAFASI NDIO KUBWA NA ULIOIPA NAFASI KUBWA NDIO NDOGO AU HAIWEZEKANI KABISA
Katika mada yangu sikuweka dhana hii ifuatayo.

Dhana:
Maadui wa ndani wa CDM walitaka kumuua Lissu ili watimize malengo 3 yafuatayo.

1. Lissu aondoe ushindani katika uchaguzi ujao wa mwenyekiti.

2. Lissu aondoe ushindani katika uteuzi ujao wa mgombea uraisi ifikapo 2020.

3. Lissu atumiwe kama kafara ili kuipa CDM mvuto kwa kuonewa huruma na kuichukia serikali katika uchaguzi wa 2020.

Sasa, kati ya dhana hii na ile ya kuwa Serikali inahusika ni ipi ina probability kubwa?

Tusianze kushutumu watu bila ya ushahidi. Tuache uchunguzi uendelee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom