Ni mtu hatari sana kuwepo ndani ya nchi.
Ila na sisi Watanzania tuna tatizo kubwa sana sana katika namna ya kukomesha mambo makubwa kama haya, iweje mjadala usiwe nani mtu huyu muuaji badala yake tuna fikia kutoa matamko nani kamsafirisha, nani kahudumia mgonjwa, idadi ya risasi ni 32 au 38 na mambo kama hayo.
Tunaelekeza nguvu kubwa kuzuia wachangia damu, sijui wasoma Albadili badala ya nguvu kujua nani muhusika. Kwa nchi makini kila lisemwalo kumuhusisha mtu basi mtu huyo anahojiwa. Jee Paulo Makonda katajwa kuwa alikuwa Dodoma sijui Morogoro na hajulikani alifuata nini, jee kuna gharama gani kumhoji na kupata ukweli ili kumsafisha kama hahusiki?
Mnadhani Lissu hana ndugu au wapenzi wake ambao wengine wana akili za visasi na kwamba wanaweza kufanya kisasi kwa mtu ambaye kumbe hahusiki? Tuendelee kuharibu nchi yetu kwa mauaji kutokana na mtu mmoja kuleta tabia yake ya mauaji kwa sababu tuu tunajikita kwenye ushabiki na kudharau mambo makubwa mabaya.
Tabia za kule Iraq, Somalia, Yemen nk za kuvaa mabomu na kwenda masokoni na makanisani au misikitini na kujilipua hazikushuka toka mbinguni bali zilianzishwa na mtu mmoja mmoja kichaa na jamii ikajikuta ipo ndani ya mwenendo huo.
Jee Tanzania ile ya kuitana NDUGU leo inaelekea wapi? Tu hakikishe huyo mtu mbaya ANATOKOMEZWA ili tuwe salama