Salaam, Shalom.
Ni wiki sasa, Mwanasheria msomi Tundu Lissu ametoa HOJA nzito kuhusiana na Muungano wetu, na anatoa HOJA Kwa kutumia Katiba ya nchi iliyopo.
Cha kushangaza wanaibuka viongozi tena wenye hadhi ya juu kabisa na kumjibu TUNDU Lissu kiujumla jumla tu. Anauliza swali Kwa kunukuu Katiba ya nchi, lakini anajibiwa Kwa kauli nyepesi za kisiasa bila ushahidi wowote au nukuu yoyote kisheria, imekaaje hii?
Jamani, HOJA hujibiwa Kwa HOJA,
Ikiwa wamekosekana viongozi wa Serikali wenye uwezo wa kumjibu TUNDU Lissu kisomi, ni Bora kunyamaza.
Swali linabaki kuwa, huko serikalini hawapo watu wenye capacity ya kumjibu TUNDU Lissu Kwa HOJA?
Karibuni🙏