Mkuu nakubaliana na wewe, kuna ndugu yangu mmoja baada ya kumaliza form 6 miaka mi3 iliyopita aligoma kabisa kuendelea na chuo, badala yake alinunua pikipik mpya na kuanza u-bodaboda ilikuwa ngumu mwanzoni maana wazee walimkalia sana vikao wakidai anadhalilisha familia (kutokana na asili ya kiarabu tuliyonayo)
Lakini jamaa aligoma kabisa kuwasikiliza na wazee wakafanya kama kumsusa maana alionekana hana adabu. Lakini hivi sasa ninavyokuambia ana bodaboda jumla 32 na yeye bado anapiga kazi, na ana mjengo wa maana na gari ya kutembelea kaiweka uani kwake. Ila still bado ni bodaboda.