Ni sababu ipi muhimu sisi wazazi tunakuwa na mtoto zaidi ya mmoja?

Wkt naanza maisha ya kujitegemea nilikutana na mzungu wa kike, ktk story ikaja issue ya idadi ya watoto wangapi ni nzuri kua nayo. Kwa haraka sana alipinga kua na mtoto mmoja na akatolea maelezo.
Kwao kazaliwa peke yake na wazazi wake ni wazee. Kuna siku baba yake aliugua sana na kulazwa hospital, mama kwa uzee wake hakuweza kumuhudumia baba kwahiyo yy akabeba jukumu lote na kwa siku zote mpaka alipotoka.
Anasema alitaabika sana sbb by that time alikua na mtoto mchanga akawa anawaza wangekua wawili angalau mzigo ungepungua kwake.
Anadai hata wazazi wake pia waliona mapungufu kuwa na mtoto mmoja kipindi mzee anaugua lkn ndo umri umemtupa.
Kwangu binafsi: Mimi naishi Arusha, mzee wangu yupo Dar aliugua mbaya najiuliza vp ningekua ndo mtoto pekee? Japo wanaume tupo wawili na madada 3 jumla 5 mzigo tumeudistribute vzr kwa wote kupunguza maumivu.
Kuna ndugu zangu kwao wako 11, ikitokea shida hata iwe kubwa kiasi gani jinsi inavyotatuliwa kirahisi mpaka raha.
All ni all kama upend watoto wengiiiiii basi angalau wawe wawili, peleka shule, lea vzr the rest muachie Mungu.
 
Suala la kuzaa watoto wangapi, au kutozaa kabisa, ni la utashi wa mtu binafsi. Ni haki ya mtu binafsi. Hapo hakuna mwanya wa haki hiyo kuingiliwa bila kuvunja haki za kikatiba na za kibinadamu za huyo mtu.

Ila.

Kuzaa kwa hesabu zozote za watoto kuja kukusaidia kwa namna yoyote baadaye ni aina fulani ya biashara, tena biashara ya utumwa.

Watu wanatakiwa wazae bila mategemeo yoyote ya kulipwa fadhila yoyote na watoto, hata ya kutunzwa uzeeni. Wajiwekee mipango yao wenyewe.

Kwa sababu.

Kwanza mtu hawezi kujua kwamba mtoto wake ataishi maisha marefu kumpita yeye. Inawezekana mtoto akafariki awali.

Pili, si maadili mema kuzaa kwa lengo la kibiashara. Kwamba mimi namzaa mtoto namtunza ili naye aje anitunze. Hiyo si familia, hiyo ni biashara ya kutunzana.

Vipi kama mtoto hana interest yoyote ya kutunza wazazi, yeye anataka kuishi kwa uhuru wake akae mbali akiendesha maisha yake? Hiyo ni haki yake. Utataka aache maisha yake amtunze mzazi?

Hiyo ni sababu moja ya kibinafsi kabisa ya kuzaa watoto.

Sisemi kwamba kumtunza mzazi ni kitu kibaya, nasema kwamba, mzazi kuweka mahesabu kwamba nazaa watoto wengi waje kunitunza vizuri baadaye ni kama kuwafanya wale watoto ni watumwa wake, kazaa watumwa wengi waje kumtumikia, kawekeza kibiashara, hajazaa kifamilia.
 
Punguza papara na stress zako, acha kupaniki.
Kama shida ni mzazi mwenzio kuwa mbali na Sasa unahisi unahitaji mtoto mwingine, usiulize watu humu maswali ya kutoto..!
Tafuta mwanamke mwingine weka Mimba.
Huyo mtoto wa Uingereza sio wako tena, tafuta mwingine.
 
Mkuu Kiranga umefika mbali sana huko but I salute ur comment though!!!!.
 
Umeandika nini sasa hapa
 
Siye tumezaliwa wawili nami nimezaa wawili.....mdogo wangu yupo mbali kidogo na home Mimi niliyekaribu na home ndo nimejua umuhimu wa watoto...mama kalazwa majuzi nilivyotingwa ni tofauti na tungekuwa wengi...mdogo wangu anafika mi nipo hoi.....lazima niongeze mtoto au watoto wawili
 
Sahihi Kabisa
 
Aisee
 
Mkuu wewe humu ni kama Senior sikutegemea kama ungemjibu maneno haya Tena mtoto wa kike.Kibaya zaidi una heshima kubwa humu mwenye thread kapotezea wewe ukaamua kununua kesi.Naamini sio Kiranga yule tunayemjua kama atakuwa ni yeye basi account Kuna wahuni wamehack.
 
Kuna mwingine dereva wa superfeo au newforce wakati anazikwa alikuwa 30 ana watoto 13 au 19.. Hadi mc akasema makofi kwake..
 
Italy wamepunguza population tena wana mpango wa kupungua zaidi.

Watu wengi wameshtuka dunia sio salama ,kuzaa watoto wachache hata kuchelewa kuzaa na wapo ambao hawazai kabisa.

Zamani mtoto kuishi ni rahisi ila sasa lazima uwe vizuri kiuchumi la sivyo utajuta
.
 
Idadi ya watoto mi nadhani na maamuzi ya mtu. Mtu azae idadi yoyote atakayo ilimradi tu anaweza kuwatunza. Niliwai kuwaza zamani niwe na wawili tu, ila sasa nna watatu ngoja nije kutafuta kengine kakufungia menopause [emoji1751][emoji1751][emoji1751]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…