Suala la kuzaa watoto wangapi, au kutozaa kabisa, ni la utashi wa mtu binafsi. Ni haki ya mtu binafsi. Hapo hakuna mwanya wa haki hiyo kuingiliwa bila kuvunja haki za kikatiba na za kibinadamu za huyo mtu.
Ila.
Kuzaa kwa hesabu zozote za watoto kuja kukusaidia kwa namna yoyote baadaye ni aina fulani ya biashara, tena biashara ya utumwa.
Watu wanatakiwa wazae bila mategemeo yoyote ya kulipwa fadhila yoyote na watoto, hata ya kutunzwa uzeeni. Wajiwekee mipango yao wenyewe.
Kwa sababu.
Kwanza mtu hawezi kujua kwamba mtoto wake ataishi maisha marefu kumpita yeye. Inawezekana mtoto akafariki awali.
Pili, si maadili mema kuzaa kwa lengo la kibiashara. Kwamba mimi namzaa mtoto namtunza ili naye aje anitunze. Hiyo si familia, hiyo ni biashara ya kutunzana.
Vipi kama mtoto hana interest yoyote ya kutunza wazazi, yeye anataka kuishi kwa uhuru wake akae mbali akiendesha maisha yake? Hiyo ni haki yake. Utataka aache maisha yake amtunze mzazi?
Hiyo ni sababu moja ya kibinafsi kabisa ya kuzaa watoto.
Sisemi kwamba kumtunza mzazi ni kitu kibaya, nasema kwamba, mzazi kuweka mahesabu kwamba nazaa watoto wengi waje kunitunza vizuri baadaye ni kama kuwafanya wale watoto ni watumwa wake, kazaa watumwa wengi waje kumtumikia, kawekeza kibiashara, hajazaa kifamilia.