Ni sababu ipi muhimu sisi wazazi tunakuwa na mtoto zaidi ya mmoja?

Ni sababu ipi muhimu sisi wazazi tunakuwa na mtoto zaidi ya mmoja?

Habari za muda huu ndugu zangu. Nimekaa, nikafikiria, Mimi ni mzazi wa mtoto mmoja wa kike.

Sasa issue kubwa nataka kufahamu nimeona kama nimeridhika au sina sababu maalumu ya kuongeza mtoto. Najiweza sana kiuchumi, mimi kijana mdogo ila mwanangu yupo anaishi na mama yake Uingereza (Mama mtanzania age 27) nilimpeleka mwenyewe. Anajiweza. Na pia sipo nae kimahusiano kwa sasa ila nina mtunza huyu binti.

(Nia nikutoa point za uchumi na uhusiano). Sasa sina Wazo lolote la kuongeza mtoto, yaani nina mapenzi yaliyopitiliza kwa huyu niliye nae.

Wazee sababu ipi inafanya mtu awe na watoto zaidi ya mmoja au wengine kupitiliza hadi watano. Nini sababu?

Au huwaga ni bahati mbaya tu, mimba hiyo?
Kuwa na mtoto zaidi ya mmoja sababu ni hizi;

1)Agizo kutoka kwa M/Mungu i.e Zaeni muongezeke mkaijaze dunia.

2)Unapanua ukoo/ jina.

3)Ukiwajengea msingi imara wa upendo watasaidiana wao kwa wao kuliko ukikazaa kamoja halafu ukafariki.

4)Ni raha kuwa na watoto angalau watatu au wanne na wawe jinsia tofauti (Ke na Me).Ke atabeba majukumu ya mama na Me atabeba majukumu ya baba.
 
Hapana,

Zaa unavyotaka. Au usizae unavyotaka.

Huo ni uamuzi wako.

Mimi ninachosema ni kwamba, moja ya hasara na matatizo ya kuzaa mtoto mmoja mmoja ni kwamba, watu wote wakizaa hivyo, idadi ya watu kwa kizazi itapungua kwa nusu kila kizazi, mpaka kizazi kitoweke kabisa.

Sijakwambia uzae au usizae vyovyote, siwezi kukupangia hilo jambo ambalo ni haki yako ya kikatiba na kibinadamu kuamua uzae au usizae unavyotaka.
Kuzaa mtoto mmoja hadi kizazi cha binadamu kitoweke kabisa inakadiriwa itachakua karibia miaka 1000 , ni mingi sana.
 
Wkt naanza maisha ya kujitegemea nilikutana na mzungu wa kike, ktk story ikaja issue ya idadi ya watoto wangapi ni nzuri kua nayo. Kwa haraka sana alipinga kua na mtoto mmoja na akatolea maelezo.
Kwao kazaliwa peke yake na wazazi wake ni wazee. Kuna siku baba yake aliugua sana na kulazwa hospital, mama kwa uzee wake hakuweza kumuhudumia baba kwahiyo yy akabeba jukumu lote na kwa siku zote mpaka alipotoka.
Anasema alitaabika sana sbb by that time alikua na mtoto mchanga akawa anawaza wangekua wawili angalau mzigo ungepungua kwake.
Anadai hata wazazi wake pia waliona mapungufu kuwa na mtoto mmoja kipindi mzee anaugua lkn ndo umri umemtupa.
Kwangu binafsi: Mimi naishi Arusha, mzee wangu yupo Dar aliugua mbaya najiuliza vp ningekua ndo mtoto pekee? Japo wanaume tupo wawili na madada 3 jumla 5 mzigo tumeudistribute vzr kwa wote kupunguza maumivu.
Kuna ndugu zangu kwao wako 11, ikitokea shida hata iwe kubwa kiasi gani jinsi inavyotatuliwa kirahisi mpaka raha.
All ni all kama upend watoto wengiiiiii basi angalau wawe wawili, peleka shule, lea vzr the rest muachie Mungu.
Hapa tatizo ni umaskini wa wazazi wala sio idadi chache ya watoto. Matajiri hata wasio na watoto wanaweza kuhudumiwa kwa huduma bora kabisa katika wakati wowote na hali yoyote.
 
Siye tumezaliwa wawili nami nimezaa wawili.....mdogo wangu yupo mbali kidogo na home Mimi niliyekaribu na home ndo nimejua umuhimu wa watoto...mama kalazwa majuzi nilivyotingwa ni tofauti na tungekuwa wengi...mdogo wangu anafika mi nipo hoi.....lazima niongeze mtoto au watoto wawili
Tatizo hapa ni umaskini, sio idadi ya watoto.
 
Siye tumezaliwa wawili nami nimezaa wawili.....mdogo wangu yupo mbali kidogo na home Mimi niliyekaribu na home ndo nimejua umuhimu wa watoto...mama kalazwa majuzi nilivyotingwa ni tofauti na tungekuwa wengi...mdogo wangu anafika mi nipo hoi.....lazima niongeze mtoto au watoto wawili
Tumezaliwa sita mpaka sasa mzee hana mtu anaydkaa nae karibu yaani kila mtu kala kona .. Mpaka nina mpango nihame kikazi nikawape tafu kidogo.

Mzee mmoja jirani ni muarabu ana wanae hajawahi kuwaona tangu mwaka 2000 mwanzo wapo Marekani , wengine oman ana watoto watatu...Mara ya mwisho walimletea coaster za abiria kama 3 hawajarudi tena hata mawasiliano hana kabisa ila wanakaa na mama yao maana waliachana na huyo mzee jirani
 
Kuzaa mtoto mmoja hadi kizazi cha binadamu kitoweke kabisa inakadiriwa itachakua karibia miaka 1000 , ni mingi sana.

Katika hesabu za maisha ya species kama watu, miaka 1,000 ni muda mdogo sana.

Yani, ukipiga hesabu kuwa watu wamekuwapo kwa miaka 200,000 iliyopita, hiyo miaka 1,000 ni 0.005% tu.

Yani, ukifanya hiyo historia ya miaka 200,000 iwe sawa na siku moja ya saa 24, hiyo miaka 1,000 ya mwisho ni sawa na dakika 7.2 za mwisho za siku.

Yani tumefikia saa tano na dakika 52 na sekunde 48 usiku, tunaelekea midnight, halafu wewe unasema hizo dakika chache zilizobakia ni nyingi sana.

Pia.

Hapo ni kabla ya kuweka hesabu za pandemic litakalokuja na kusaidia kufyeka idadi ya watu wengi sana.
 
Habari za muda huu ndugu zangu. Nimekaa, nikafikiria, Mimi ni mzazi wa mtoto mmoja wa kike.

Sasa issue kubwa nataka kufahamu nimeona kama nimeridhika au sina sababu maalumu ya kuongeza mtoto. Najiweza sana kiuchumi, mimi kijana mdogo ila mwanangu yupo anaishi na mama yake Uingereza (Mama mtanzania age 27) nilimpeleka mwenyewe. Anajiweza. Na pia sipo nae kimahusiano kwa sasa ila nina mtunza huyu binti.

(Nia nikutoa point za uchumi na uhusiano). Sasa sina Wazo lolote la kuongeza mtoto, yaani nina mapenzi yaliyopitiliza kwa huyu niliye nae.

Wazee sababu ipi inafanya mtu awe na watoto zaidi ya mmoja au wengine kupitiliza hadi watano. Nini sababu?

Au huwaga ni bahati mbaya tu, mimba hiyo?
Mi nanao wa nne ndani,wanna nje!
Bado nataka wanane wengine Toka nyumba ndogo!!
Mind set!
 
Aah, wewe unaweza kuona ukweli kumbe unatuletea shombo tu.

Mtu kauliza swali, hajakuuliza wewe.

Anapata michango ya watu wengine kumjibu.

Wewe kinachokuuma nini?

Kama hupendi hiyo mada kwa nini usiiruke tu uende kwenye mada unazopenda?

Ulitaka kumzalia mtoa mada mtoto wa pili akakukatalia, ndiyo maana unatuletea kisirani chako hapa?

Au uko mwezini unasumbuliwa na hormones?
Dah [emoji23][emoji23]
 
Katika hesabu za maisha ya species kama watu, miaka 1000 ni muda mdogo sana.

Yani, ukipiga hwsabu kuwa watu wamekuwapi kwa miaka 200,000 iliyopita, hiyo miaka 1,000 ni 0.005% tu.

Pia.

Hapo ni kabla ya kuweka hesabu za pandemic litakalokuja na kusaidia kufyeka idadi ya watu wengi sana.
Labda pia katika kipindi hicho zitatokea vumbuzi ambazo zitapunguza binadamu kuzeeka na kurefusha kiwango cha maisha ya binadamu kwa miaka mingi sana. Kuna wanasayansi wamejichimbia katika tafiti za immortality zinazofadhiliwa kwa mabilioni ya dola na matajiri.
 
Unapozaa mtoto mmoja lazima ujue duniani Kuna mengi , mfano Kuna kifo ambacho kinaweza kuchukua huyo mmoja na ukabaki mtupu.

Na madhara ya kukosa familiar huwa yanaonekana kipindi cha uzee wetu.
 
You are a despicable miscreant spewing pure excrement out of all your orifices.

Wewe huna unachoweza kujibizana na mimi zaidi ya logical fallacies kama hizi za ad hominem attack.

Ni wazi hujasoma, huelewi uhuru wa mtu binafsi ni nini, huelewi haki za kikatiba ni nini, huelewi haki za binadamu ni nini, huna ustaarabu hata chembe, huelewi ugumba ni nini, huelewi kuwa kuna watu ni wagumba kweli hawana watoto kabisa na wanatamani kuwa na watoto na kuwanyanyapaa kama unavyofanya kwa ugumba wao ni kitu kibaya.

Wewe ni kama guluguja asiye na ubongo wala uti wa mgongo, unabiringita kwa reflex action tu.

Mimi sina muda wa kujibizana na wewe.

You are not on my level.

Nakuongeza kwenye list yangu ya watu wajingawajinga nisiotaka kujibizana nao.

Nakupeleka ignore list, unakuwa mtu wa 164 kupoteza privilege ya kujibizana nami moja kwa moja.

Kuanzia hapa sitaona chochote utakachopost.
Nyenye nyenye nyenye mshamba mkubwa weeee, mnajikuta wazungu kisa ni wakoloni wao, nyie ni nyani tu mbele ya macho yao, kenge kama wewe ulokosa nguvu za kiume unataka kuwaaminisha ujinga wako mazumbukuku wenzio eti mtoto mmoja fyoko fyoko,

Pathetic.
 
Katika hesabu za maisha ya species kama watu, miaka 1,000 ni muda mdogo sana.

Yani, ukipiga hesabu kuwa watu wamekuwapo kwa miaka 200,000 iliyopita, hiyo miaka 1,000 ni 0.005% tu.

Yani, ukifanya hiyo historia ya miaka 200,000 iwe sawa na siku moja ya saa 24, hiyo miaka 1,000 ya mwisho ni sawa na dakika 7.2 za mwisho za siku.

Yani tumefikia saa tano na dakika 52 na sekunde 48 usiku, tunaelekea midnight, halafu wewe unasema hizo dakika chache zilizobakia ni nyingi sana.

Pia.

Hapo ni kabla ya kuweka hesabu za pandemic litakalokuja na kusaidia kufyeka idadi ya watu wengi sana.
Inaweza kujirudia watu wakaanza kuishi mamia ya miaka kama wa kwenye Biblia[emoji1787], labda miaka 900 hivi kama kina Methuselah wa Biblia.
 
Mm ninao watoto 3 wote wa kike maisha yangu ni ya kati yanayonifanya niweze kuwahudumia kwa kadiri hawa mabinti.

Katika fikra zangu za ujanani nilipenda sana niwe na mtoto 1 na nilikuwa nikitamani awe binti.

Hivyo nilipopata mtoto na akawa Binti nilifurahi na kuamini mawazo yangu yatatimia. Lkn sivyo alivyokuwa akiwaza mwenzangu.

Lkn leo hii NATAMKA WAZI, kama unayo Mali jenga BOMA kuwa na Mwanamke Zaidi ya 1 hata wakifika 10 zaa kadiri ya maandiko .

Inapendeza sana .
 
Labda pia katika kipindi hicho zitatokea vumbuzi ambazo zitapunguza binadamu kuzeeka na kurefusha kiwango cha maisha ya binadamu kwa miaka mingi sana. Kuna wanasayansi wamejichimbia katika tafiti za immortality zinazofadhiliwa kwa mabilioni ya dola na matajiri.

Yeah. Hatuwezi kutabiri sayansi na teknolojia itatupeleka wapi, mengi yatakayowezekana baafaye hata hatujaanza kuyaelewa vizuri sasa.

Kuna sayansi ya cryogenic ya ku freeze watu kwa miaka mingi mpaka uwezekano wa kuwafufua utakapopatikana.

It's a bit like mummifying the Paharaohs if you ask me.

Elon Musk anataka kufanya watu wawe "multi-planetary species". Yani tuwe tunaishi katika sayari zaidi ya moja.

Ili sayari hii, kwa mfano, ikipigwa na kimondo kikubwa na kupata "extinction level event" itakayomaliza maisha ya watu wote hapa duniani, kuwepo na watu walio katika sayari nyingine kuendeleza kizazi.

Kwa sasa wote tumekaa kwenye sayari moja, sayari ikipata daflao la kumaliza maisha ya watu wote, hatuna backup ya kuendeleza kizazi kwenye sayari nyingine.

Unaonaje huu mpango?

Una mantiki ya kutufaa au ni kupoteza mabilioni ya dola tu?
 
Back
Top Bottom