Kwa siku hizi utaambiwa kutaka kuishi miaka mingi sana ni ubinafsi na uharibifu wa mazingira.Inaweza kujirudia watu wakaanza kuishi mamia ya miaka kama wa kwenye Biblia[emoji1787], labda miaka 900 hivi kama kina Methuselah wa Biblia.
Sababu zipi zilikufanya uhitaji kupata mtoto huyo uliyenaye?Habari za muda huu ndugu zangu. Nimekaa, nikafikiria, Mimi ni mzazi wa mtoto mmoja wa kike.
Sasa issue kubwa nataka kufahamu nimeona kama nimeridhika au sina sababu maalumu ya kuongeza mtoto. Najiweza sana kiuchumi, mimi kijana mdogo ila mwanangu yupo anaishi na mama yake Uingereza (Mama mtanzania age 27) nilimpeleka mwenyewe. Anajiweza. Na pia sipo nae kimahusiano kwa sasa ila nina mtunza huyu binti.
(Nia nikutoa point za uchumi na uhusiano). Sasa sina Wazo lolote la kuongeza mtoto, yaani nina mapenzi yaliyopitiliza kwa huyu niliye nae.
Wazee sababu ipi inafanya mtu awe na watoto zaidi ya mmoja au wengine kupitiliza hadi watano. Nini sababu?
Au huwaga ni bahati mbaya tu, mimba hiyo?
Hiyo ina maana kwamba, kuzaa sana ni ishara ya ujinga na umasikini.Inaweza kufikia mpaka nchi kuishiwa na watu kabisa.
Hili tatizo linaonekana kama utani, ila South Korea wanalipitia sasa hivi.
Kuna kampuni ya ujenzi ya South Korea inatoa fedha kiasi cha US dollar 75,000 kwa kila mfanyakazi ambaye amepata mtoto ndani ya miaka miwili iliyopita, au atakayepata mtoto.
Hii ni kupambana na "population decline" huko South Korea.
Watu wamegoma kuzaana.
Mtihani ni kwamba, inaonekana kuwa kadiri nchi zinavyopata maendeleo ya kiuchumi na watu kuelimika, na maisha kupanda gharama, watu wanaamua kuzaa watoto wachache zaidi.
A South Korean firm is offering to pay its workers $75,000 each time they have a baby
Seoul (CNN) — A South Korean company is ready to pay million of dollars to help fix the country’s abysmally low birth rate.auburnpub.com
Mpango wa Elon Musk kuwafanya binadamu waishi sayari nyingine ni mzuri labda na overambitious pia kwa karne hii, ila utakuwa msingi mzuri kwa vizazi vijavyo kumfanya binadamu kuwa "multiplanetary species".Yeah. Hatuwezi kutabiri sayansi na teknolojia itatupeleka wapi, mengi yatakayowezekana baafaye hata hatujaanza kuyaelewa vizuri sasa.
Kuna sayansi ya cryogenic ya ku freeze watu kwa miaka mingi mpaka uwezekano wa kuwafufua utakapopatikana.
It's a bit like mummifying the Paharaohs if you ask me.
Elon Musk anataka kufanya watu wawe "multi-planetary species". Yani tuwe tunaishi katika sayari zaidi ya moja.
Ili sayari hii, kwa mfano, ikipigwa na kimondo kikubwa na kupata "extinction level event" itakayomaliza maisha ya watu wote hapa duniani, kuwepo na watu walio katika sayari nyingine kuendeleza kizazi.
Kwa sasa wote tumekaa kwenye sayari moja, sayari ikipata daflao la kumaliza maisha ya watu wote, hatuna backup ya kuendeleza kizazi kwenye sayari nyingine.
Unaonaje huu mpango?
Una mantiki ya kutufaa au ni kupoteza mabilioni ya dola tu?
Hahaa,Hiyo ina maana kwamba, kuzaa sana ni ishara ya ujinga na umasikini.
Sawa,Mpango wa Elon Musk kuwafanya binadamu waishi sayari nyingine ni mzuri labda na overambitious pia kwa karne hii, ila utakuwa msingi mzuri kwa vizazi vijavyo kumfanya binadamu kuwa "multiplanetary species".
Mimi naona bora hizo dola zake kwa sasa angezipeleka zaidi kuboresha mazingira ya hapa duniani ya sasa kupitia teknolojia za kuboresha mazingira, dunia iachane na fossil fuels kabisa, ipambane na njaa, kansa, uzee, ajali n.k lakini yeye inaonekana haya kwake sio kipaumbele zaidi ya binadamu kwenda Mars.
🙏🙏Mkuu,
Mimi nina heshima kwa wenye heshima.
Ukiketa ukauzu mimi ni kauzu kupita maelezo.
Na hizo heshima mnazonipa kama zinanizuia mimi kuwa huru, kuwa Kiranga original, kuwa Kiranga authentic, basi sizitaki.
Kwangu mimi, kuwa huru nikasema ninachotaka ni muhimu kuliko hizo heshima mnazotaka kunipa.
Ikiwa hizo heshima zitazuia uhuru wangu, basi hizo heshima zitakuwa mzigo tu, zitakuwa mtego wa kunitega nisiwe huru, nisiwe my authentic self, niwe Kiranga feki anayeogopa kusema anavyojisikia kweli eti kwa sababu watu watamuona hivi au vile.
Nakuomba sana nivue hizo heshima ulizonibandika ili nipate wepesi kujieleza.
Naona heshima hizo zinanitia udhia na mzigo tu.
Falsafa zangu ni tofauti sana na zako, usilazimishe zako ziwe zangu wakati mimi sizielewi wala sizikubali.
Ushanifahamu?
Kwa mantiki hiyo hupendi dunia kuendelea kuwa na watu as per your satisfaction with only one kid.Mkuu,
Mimi ni kama wewe, nilipata mmoja tu nikaridhika.
Kama unapenda dunia iendelee kuwa na watu, unatakiwa angalau kuwa na watoto wawili.
Actually kimahesabu ya takwimu tunatakiwa kuwa na average ya watoto 2.1, hii ndiyo replacement rate.
Ukiwa na mtoto mmoja wewe, na dunia nzima ikiwa na mtoto mmoja average, maana yake kizazi kinachofuata kitakuwa nusu ya kizazi hiki, na kinachokifuatia kitakuwa nusu ya hiki, mpaka kizazi kitaisha.
IQ kubwaSuala la kuzaa watoto wangapi, au kutozaa kabisa, ni la utashi wa mtu binafsi. Ni haki ya mtu binafsi. Hapo hakuna mwanya wa haki hiyo kuingiliwa bila kuvunja haki za kikatiba na za kibinadamu za huyo mtu.
Ila.
Kuzaa kwa hesabu zozote za watoto kuja kukusaidia kwa namna yoyote baadaye ni aina fulani ya biashara, tena biashara ya utumwa.
Watu wanatakiwa wazae bila mategemeo yoyote ya kulipwa fadhila yoyote na watoto, hata ya kutunzwa uzeeni. Wajiwekee mipango yao wenyewe.
Kwa sababu.
Kwanza mtu hawezi kujua kwamba mtoto wake ataishi maisha marefu kumpita yeye. Inawezekana mtoto akafariki awali.
Pili, si maadili mema kuzaa kwa lengo la kibiashara. Kwamba mimi namzaa mtoto namtunza ili naye aje anitunze. Hiyo si familia, hiyo ni biashara ya kutunzana.
Vipi kama mtoto hana interest yoyote ya kutunza wazazi, yeye anataka kuishi kwa uhuru wake akae mbali akiendesha maisha yake? Hiyo ni haki yake. Utataka aache maisha yake amtunze mzazi?
Hiyo ni sababu moja ya kibinafsi kabisa ya kuzaa watoto.
Sisemi kwamba kumtunza mzazi ni kitu kibaya, nasema kwamba, mzazi kuweka mahesabu kwamba nazaa watoto wengi waje kunitunza vizuri baadaye ni kama kuwafanya wale watoto ni watumwa wake, kazaa watumwa wengi waje kumtumikia, kawekeza kibiashara, hajazaa kifamilia.
Hapana,Kwa mantiki hiyo hupendi dunia kuendelea kuwa na watu as per your satisfaction with only one kid.
NB; assuming that the rest of the earth will be satisfied with only one child as well.
And my question is "kwanini hupendi dunia iendelee kuwa na watu?"
Shida inakuja kwamba, wanaotakiwa kuongeza hawahitaji, na wanaotakiwa kupunguza ndio wanazidi kufyatua watoto.Hahaa,
Mkuu sasa unataka kuniingiza kwenye matatizo ya kuwanyanyapaa rafiki zangu wenye watoto wengi, ambao wametumia turufu yao kwa haki zao kabisa, za kikatiba na kiutu.
Hiki suala ni tata sana kwa sababu wakati kuna watu wanasema kuzaa sana ni chanzo kikubwa kabisa cha uharibifu wa mazingira, na kunazuia maendeleo ya kiuchumi, kuna wengine pia wanaosema kuwa dunia inakabiliwa na tatizo la watu kutozaa vya kutosha.
Kwa hakika tunaona nchi zilizoendelea kiuchumi na kielimu watu wanapunguza idadi ya watoto. Korea ya Kusini ni mfano mmoja tu, lakini kuna nchi nyingi za Ulaya zina birth rates ndogo.
Kwa hesabu za United Nations Population Division za mwaka 2015 mpaka 2020 nchi za Afrika zilikuwa na average ya 4.4 fertility rate, Asia 2.2, Europe 1.6, Latin America and the Caribbean 2.0, North America 1.8, Oceania 2.4
Unaweza kusema kuwa nchi zenye umasikini na ujinga zaidi zina fertility rate kubwa zaidi.
Kwa hivyo, inawezekana pia nchi fulani zikawa zinahitaji kuongeza uzazi, na nchi nyingine zikawa zinahitaji kupunguza uzazi ili ki balance.
Unaweza kuangakia namba na kujua nani anahitaji kuongeza na nani anahitaji kupunguza.
Mkuu Korea Kusini huko kuna kampuni ya ujenzi imetoa ofa ya US $ 75,000 kwa wafanya kazi wake kwa kila mtoto aliyezaliwa katika miaka miwili iliyopita na kila ntoto atakayezaliwa.Shida inakuja kwamba, wanaotakiwa kuongeza hawahitaji, na wanaotakiwa kupunguza ndio wanazidi kufyatua watoto.
Mtu hana kitu kabisa lakini anazaa watoto kibao kama ngedere, imagine ofa ya pesa ingetolewa bongo ingekuwaje.
Hapana,
Again, nakujibu kwa sababu umeniuliza, sina nia ya kumnyanyapaa yeyote. Maamuzi ya kuzaa au kutozaa vyovyote ni ya mtu binafsi, ni haki za kikatiba na kibinadamu.
But kuna vitu nafikiri kuwa ni kweli, mimi binafsi, kwa kuangalia facts and figures.
Kwa sasa dunia inaweza kufikia extinction level event kwa watu kuzaliana zaidi kuliko kwa watu kupunguza kuzaa.
Ukiangalia hesabu za carbon emission na global warming na mambo mengi ya mazingira, na ukweli kwamba the single biggest contributor ni idadi ya watu, ni wazi kwamba, kwa sasa, msisitizo hapo ni "kwa sasa", kuongeza watu duniani kunaweza kuleta madhara makubwa sana kuliko kupunguza watu kwa sasa.
Kuna level ambayo tukiifikia kupunguza watu kutakuwa ni hatari, lakini hatujaifikia sasa na iko mbali sana bado.
Yani kuna happy medium figure ya average fertility rate tunatakiwa kuifikia, hatujaifikia, mimi nasaidia dunia iifikie hiyo figure.
Nahisi inaweza ikawa maangamizi, mass destruction.Mkuu Korea Kusini huko kuna kampuni ya ujenzi imetoa ofa ya US $ 75,000 kwa wafanya kazi wake kwa kila mtoto aliyezaliwa katika miaka miwili iliyopita na kila ntoto atakayezaliwa.
Vipi kampuni ya Bongo ikitoa ofa hiyo?
Kila mtu ana wajibu wa kuitunza dunia ili si tu iendelee kuwapo kwa vizazi vijavyo, bali pia iwe na mazingira bora. Pengine hata mazingira bora zaidi ya yaliyopo sasa.Asante kwa ufafanuzi mzuri.
Why umeamua kuchukua part ya kusaidi ili wanadamu tufikie hiyo figure.? Au ndio Uhuru?
Nakushauri usome post no 25.Siye tumezaliwa wawili nami nimezaa wawili.....mdogo wangu yupo mbali kidogo na home Mimi niliyekaribu na home ndo nimejua umuhimu wa watoto...mama kalazwa majuzi nilivyotingwa ni tofauti na tungekuwa wengi...mdogo wangu anafika mi nipo hoi.....lazima niongeze mtoto au watoto wawili
Umejibu kwa ufasaha kabisa.Mkuu, ukiondoka; mali unazoziacha sio zako tena... ni za warithi/ uliowaacha hai.
Wao ndio watajua wanaziangaliaje, kama wakizinywea bia au wakiamua tu kuzitom#bea hadi ziishe wewe haikuhusu kabisa! [emoji41][emoji23]
Suala kubwa hapa ni kipato, elimu, utamaduni, dini na mfumo wa maisha.Shida inakuja kwamba, wanaotakiwa kuongeza hawahitaji, na wanaotakiwa kupunguza ndio wanazidi kufyatua watoto.
Mtu hana kitu kabisa lakini anazaa watoto kibao kama ngedere, imagine ofa ya pesa ingetolewa bongo ingekuwaje.