Ni sahihi kuachana na mwanamke uliyemzalisha watoto wawili?

Sawa sawa mkuu,ushauri wako nimeuchukua
 
Mzee chanzo cha ujaribifu wa watoto uchangiwa na ujinga wa wazazi.

Usione kizazi kibovu kilichopo sasa ni Matokeo ya wazazi kutojitambua na kujua Wana wajibika kulea na kutengeneza watoto watakao kua baba na mama Bora.

Mkeo ni Mtu muhumu sana katika maisha yako brother.

Ukiona mwanamke Ana kurekebisha kwenye jambo Lolote jua Anakupenda na kukutakia Mema.

Mimi Niko kwenye ndoa zaidi ya Miaka 30 Nina uzoefu mkubwa juu ya Mke.

Ukitaka kupotea jufanye wewe unajua kila kitu Alafu Mdharau mkewako. Muda utaongea utaharibukiwa kila kitu.

Mimi Nakushauri Mtafute mkewako myatengeneze na ukubali Kushauriwa Brother na mkewako.

Wewe ni Mtu mzima ni lazima uwe mtu wa kutafakari mambo na kuamua kwa busara brother.

Matatizo Au changamoto haziondolewi kwa kulewa ndio unajipoteza kabisa.

Changamoto uondolewa kwa kutafakari na Kushauriana na mkewako.
 
Huyo tayari ni mke wako, ondoa kauli kuwa hamjafunga ndoa. Ndoa tayari hiyo hata kama hangekuzalia. Kurudi anaweza kurudi kama atapigwa na maisha vibaya ila akipata ka ajira ka kumpa kula na watoto wake, imetoka hiyo, ikirudi ina pancha, we nawe itabidi ujitafutie single mama uvute kama hutanasa kwa mishangazi. Kumchukulia poa huyo mkeo itakugharimu sana kama hatarudi
 
Dada Carol mwanamke hawez kuondoka kwako bila plan b

I mean lazima kuna muhuni uko ktaan amemchanganya

Sasa ni bora mwanamke awe na tabia zingine ila sio kutmbewa 😎
 
Sawa mkuu,umesomeka
Ikiwa ni kuomba msamaha, inakubidi,

Kingine usiamini kuwa pombe ndo mtatuzi wa shida zako, siwezi kukuambia acha pombe, Ila pombe sio dawa ya matatizo yako,

Fuatilia wanao walipo, ona uwezekano wa kutoa sapoti

Ikiwa mke kakaza ni muda tuu atarejea kama Hana mtu anayempa kiburi huko nje,

Muda wa mapumziko anayosema binafsi isizid miezi mitatu ikipita hapo
 
Sawa sawa mkuu,this is well noted
 
Sawa mkuu
 
Miaka saba huyo ni mkeo.Jishushe chini na kumuomba msamaha kwa kumchapa.Halalisha ndoa mlee watoto pamoja.Baada ya kazi fika nyumbani acha kuzurura wanawake hudhani umetoka kufanya kamanyola
 
Poa poa mkuu
 
Fahamu kuwa kuna masela huwa hawajali idadi ya watoto aliyonayo mwanamke wanabeba na watoto wake. Uko tayari kuona au kusikia watoto wako wanalelewa kwa msela mwingine? Ukute tayari mkeo kajazwa mimba na huyo msela aliyembeba
 
Fahamu kuwa kuna masela huwa hawajali idadi ya watoto aliyonayo mwanamke wanabeba na watoto wake. Uko tayari kuona au kusikia watoto wako wanalelewa kwa msela mwingine? Ukute tayari mkeo kajazwa mimba na huyo msela aliyembeba
Yote heri tu mkuu
 
Kikubwa nakusaidia kutunza Mzee mwenzangu sema ka nyau kake kadogo sana like hajawai zaa😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…