Ni sahihi kwa Mwanaume aliyeoa kupika?

Ni sahihi kwa Mwanaume aliyeoa kupika?

Mkuu, mimi hua napika na wakati waifu anaangalia tamthilia sebleni kisha nampakulia kabisa na kabla hajaanza kula nahakikisha nimemnawisha kwa maji safi tena yalio chemshwa.
Na saizi ndio nimemaliza kuosha vyombo, nikimaliza ku comment hapa nataka nika deki nyumba...😊
Ushimen kuna wadau wanauliza huku eti huwa una kuna na nazi?
 
Hayo ni malezi tu yanakuja kujenga mazoea

Mi msure huwa anapika enzi anatulea kama single Dad ila hata alipooa tuko wakubwa weekends anatoa hizo treat.

Lakin kwenye makuzi yao wanasema mama yao alikua hawatenganishi kazi za jikoni sijui za mwanamke

Hata nakua naona mabinam zangu wakiume wakiwa kwenye zamu ya upishi, vyombo sa hapo baadae kimoja kinaweza kua hobby...

Wala si kurogwa.
 
Mimi niko vizuri sana kwenye kupika. Ila hua napika siku nikijisikia, siku hiyo nawaambia wote kaeni pembeni leo napika mimi! Nafyatua kitu cha uhakka mtaa mzima wanaulizana.

Pili kuna aina ya vyakula, mfano kama nimenunua BEBERU langu nataka nile na washkaji siwezi kamwe kumpa wife anichomee!
Hahahah umenikumbusha siku nimeenda ukweni baada ya long time.

Nilikabidhiwa Kisu, Wavu wa kuchomea nyama, kiberiti na Beberu la hatari
 
Hayo ni malezi tu yanakuja kujenga mazoea

Mi msure huwa anapika enzi anatulea kama single Dad ila hata alipooa tuko wakubwa weekends anatoa hizo treat.

Lakin kwenye makuzi yao wanasema mama yao alikua hawatenganishi kazi za jikoni sijui za mwanamke

Hata nakua naona mabinam zangu wakiume wakiwa kwenye zamu ya upishi, vyombo sa hapo baadae kimoja kinaweza kua hobby...

Wala si kurogwa.
Jambo hema Baba kuwalikia wanaye. Inapendeza. Pia kuna ile akina sisi tulizaliwa madume tupu.
 
Swal la mwanaume kupika au kusaidia kazi yoyote ile ya ndani (ambayo anaiweza), likifanyika kwa utashi wa mwanaume mwenyewe bila kutumwa na mke wake haliwezi kuondoa thamani ya uanaume wake.

Mbaya ni ile kufanya kitu fulani kwasababu mke amekutaka ufanye, nasisitiza AMEKUTAKA UFANYE.
 
Jamani tuacheni masihara. Kama kuitwa mshamba bora mimi niwe hivyo.

Hivi inakuwaje mwanaume unamkuta yuko jikoni anahangaika kupika au kufua au hata kupiga deki?

Si tulikubaliana Kazi ya Mwanaume ni kutafuta pesa, kulisha familia, kusomesha watoto na kutoa ulinzi kwa familia na jamii??

Tulikubaliana kazi ya mwanaume ni kuhakikisha unawaza kununua ndege, treni, kumiliki makampuni makubwa ya biashara, Kuiangusha Urusi.

Na mwisho kabisa kazi muhimu baada ya hayo ni kutoa kichapo kitakatifu kwa mama watoto mpaka anasema kweli hapa nina mwanaume.

Yangu ni hayo tu.
Lack of exposure, ungekuwa umetoka kidogo na kuiona dunia nje ya mipaka ya Tanzania hili jambo lisingekusumbuwa akili.

Kwanza nakupa challenge ni hotel gani unayoijuwa wewe Chef ni mwanamke?
 
Mbona ni maisha ya kwaida tu. Yani kama mimi kuna mboga au msosi flani nikitaka kula kujigalagaza namuachia mzee baba jiko.

Mkuu unafikir mahaba ni mpaka ubebwe upelekwe bafuni?
 
Lack of exposure, ungekuwa umetoka kidogo na kuiona dunia nje ya mipaka ya Tanzania hili jambo lisingekusumbuwa akili.

Kwanza nakupa challenge ni hotel gani unayoijuwa wewe Chef ni mwanamke?
Hotel ni kazini. Nyumbani is home of Mahaba tu.
 
Mbona ni maisha ya kwaida tu. Yani kama mimi kuna mboga au msosi flani nikitaka kula kujigalagaza namuachia mzee baba jiko.

Mkuu unafikir mahaba ni mpaka ubebwe upelekwe bafuni?
Hahahaa yale ya kitanga
 
Kuna wanaume wenzetu wana vipaji vingi sana.

Mambo ya kupika Mimi ndio siwezagi.

Kitu pekee nachoweza kupika ni chai tu labda na kuchemsha maji ya kuoga.

Kuna siku nilijaribu kupika ugali, nikashangaa nimejaza maunga unga tu ukatokea uji mzitoooo... nikashindwa kuelewa niufanyeje [emoji848] nikaumwaga!!! Dah nikasema ngoja nijaribu kupika wali nikashangaa mchele umanasa nasa kwenye sufuria na umeungua...

Ilibidi nikubali tu yaishe nikaendelea na ratiba zangu za kula kwenye vibanda umiza [emoji848][emoji848]
Nimecheka vibaya mno...

Ila mkuu chai yenyewe huwa ina iva kweli??

Au nayo huwa inaungua pia 🤗😊
 
Siku hiz nazi hazikuniwi kwenye mbuzi tena
View attachment 2181175
Mzungu alijua wanaume wengi wanaona ni aibu kukaa kwenye mbuzi na kukuna nazi akaamua kurahisha mambo
Imewarahusishia wapishi wa kiume.

Kupika ni kwa mwanamke.

Mambo ya kumodify mpaka ukune na mashine inaonekana kazi ya upishi si yako una force tu
 
Back
Top Bottom