Ni sahihi mtu mmoja kula kitimoto nusu kilo peke yake akamaliza?

Ni sahihi mtu mmoja kula kitimoto nusu kilo peke yake akamaliza?

Hili suala la mtu mmoja kula kitimoto nusu kilo na ndizi mbili au ugali peke yake na akamaliza limekaaje kiafya? Huu sio ulafi na matumizi mabaya ya pesa?
Mtu anaweza kuagiza kitimoto kilo nzimaa peke yake. Lakini hawezi kuagiza kilo nzima ya mbuzi peke yake mara nyingi sijui kwann ? Utafiti unahitajika hapa
 
Kupata wenye IQ kubwa hili taifa tusahau,wew unakula nusu kilo yote ya nini mwilini,ukitaka kuwa timamu dhibiti unachokula haijarishi maana kinachozidi tu mwilini kinahifadhiwa kama uchafu wa awali, wale wa visinia endeleeni tu
 
Mi nikitoka out na shemeji yenu nanunua kilo 2 yaya moja nami moja na ndizi sita kila mmoja tatu. Baadaye yeye anapiga pepsi mi alvaro yangu ya chupa baaaasi burdani
 
Kwa mlaji halisi unatakiwa ule nusu kilo,ugali robo kibaba na upige mbege kimbo sita.Saaafiii hata mapepo wanakukwepa tu.
 
Hili suala la mtu mmoja kula kitimoto nusu kilo na ndizi mbili au ugali peke yake na akamaliza limekaaje kiafya? Huu sio ulafi na matumizi mabaya ya pesa?
kabla ya kukujibu nawewe jibu kwanza aya maswali machache.

-Je iyo kitimoto ina kapilipili ka ugwadu kwa mbali?

-Je iyo kitimoto ina kachumbari safi apo pembeni?

-Je iyo kitimoto imeokwa vizuri kiasi ukiitazama tu mate yanajiunda yenyewe uko mdomoni?

-Je izo ndizi ni zile zilizookwa vizuri kiasi ukizitazama tu unaishia kusema asalamalekho walah?

-na je kama ni ugali upoje nao au ni ule ugali mdogomdogo mweupe safi na laini kabisa hlf kama unang'aang'aa fulan?
 
kabla ya kukujibu nawewe jibu kwanza aya maswali machache.
-Je iyo kitimoto ina kapilipili ka ugwadu kwa mbali?
  • Je iyo kitimoto ina kachumbari safi apo pembeni?
  • Je iyo kitimoto imeokwa vizuri kiasi ukiitazama tu mate yanajiunda yenyewe uko mdomoni?
-Je izo ndizi ni zile zilizookwa vizuri kiasi ukizitazama tu unaishia kusema asalamalekho walah?
-na je kama ni ugali upoje nao au ni ule ugali mdogomdogo mweupe safi na laini kabisa hlf kama unang'aang'aa fulan?
Nipo jiranijirani nafuatilia atakavyojibu.
 
Hili suala la mtu mmoja kula kitimoto nusu kilo na ndizi mbili au ugali peke yake na akamaliza limekaaje kiafya? Huu sio ulafi na matumizi mabaya ya pesa?
Post zingine zinatufanya wanaume wa Dar tuonekane mdebwedo!
 
Sio matumizi mabaya ya hela au ulafi kama unavyodhani ila ni mapenzi tu na chakula husika, mimi naweza maliza kilo nzima peke yangu wewe unashangaa nusu?
 
Back
Top Bottom