Anigrain na
kcamp kama nyie ni wajuaji basi mnatakiwa muwe mnajua jinsi ya kutafuta taarifa za simu latest au simu za high end za TECNO.
Mkishindwa kitu kidogo kama hicho ina maana hata sifa za kujifanya wachambuzi wa simu mbele ya macho yangu mtazikosa.
Na pili mnapocompare simu msiwe shallow kuhangaika na specifications tu. Mjiulize pia hiyo specification ina umuhimu wowote wa msingi kwa matumizi ya kawaida ya simu?
Zingatieni hoja yangu ya msingi ambayo ni:
"
Kitu gani cha msingi ambacho unaweza kufanya kwenye iPhone ambacho huwezi kufanya kwenye TECNO"?
Maana kuna mwenzenu mmoja wa iPhone nilimwambiaga hii ishu akaja na hoja ya iPhone sasa hivi ina satelite calls. Nikamuuliza sasa satelite call ni jambo la msingi?
Au mfano 4G au 5G sio vitu vya msingi kabisa. Connection ya 3G inatosha sana mtu kutumia simu vizuri kabisa. Sema watu ndo huwa wanakuwa manipulated kwamba "5G ndo yenyewe, ukiwa na 3G wewe ni mtu wa kale!"
Au screen resolution. Jicho la binadamu linaona mwisho 576 Megapixels. Kwa hiyo resolution ya 720p inatosha kabisa. Ni resolution ambayo video zake unastream vizuri tu kwa 3G.
Lakini watu wamehamasishwa kwamba 1080p, au 4K au 8K ndo yenyewe!!
Unajikuta unapigwa hela nyingi kununua kitu ambacho sio cha msingi ili tu uweze kujitapa mbele ya watu kwamba wewe ni mjanja.