Ni smart TV gani 4K kwa sasa ipo vizuri sana?

Nilimuuliza bajeti yake hakusema hivyo watu wameamua wampe Kwa ujumla
 
Mkuu unajua kidogo kuhusu phillips.
 
Kwa maoni yangu,
Tv zenye ubora kuanzia quality ya picha,software&hardware

1. Sony
2. LG
3. Skyworth
4. Samsung (ubahatishe OG& latest series)
5. HISENSE
6. TCL
Afu yatafata makampuni mengine ,
ya kawaida
Vipi kuhusu phillips.
 
Hii ni only for genius , wajinga wa Samsung hawawez kuelewa , Samsung zinazouzwa Africa ni Sawa Sawa na toleo Lao la smu za Aseries yaani ni Ujinga mtupu unless ubahatishe zinazokuwa shipped to Europe
Na huu ndio ukweli mtupu.
 
Kwenye simu kuna mambo mengi sana ya ziada na siyo kupiga na kupokea kama unavyodhani wewe😆😆. Kingine sijasema kuwa Hisense ni Bora kuliko Samsung au LG Kila mtu anajua hawa wakorea wapo vizuri kwenye hii sekta. Mimi maelezo yangu yamebase kwenye bei ya laki sita sio brand. Hizo Samsung ni nzuri sana kinachofanya iwe nzuri ni hizo TV zake za mamilioni sio za laki sita. Hamna mtu ananunua brand Mimi naongelea TV wewe unaongelea brand. Angalia utofauti wa mazungumzo yetu
 
Mkuu haina haja ya kuzunguka mbuyu, kusema kitu ni famba sio kukizarau ni uhalisia wake.
 
Samsung TV fake zipo sana
Kiukweli sijawahi kusikia vitu kama hivi. Kama ipo basi ndio ndio nasikia hapa.

Ofisi zetu nchi nzima zinatumia Samsung miaka na miaka sijawahi kuona ama kusikia tatizo lolote. Ama vile tunanunua kwa authorized dealers.

Unanunua na unapewa warrant card kabisa na bado ni fake?
 
Wewe kubali hujui
 
Brands mbili nzuri zenye quality ya juu, LG na Sony, hizo unapata value for money(kibongobongo)

Brands za size ya kati, quality nzuri ni Samsung na Hisence.

Zaidi ya hapo unanunua TV za kawaida, specs kubwa lakini ubora na thamani ndogo.

Kuna brands unanunua na baada ya miaka kumi ipo vile vile, hujafungua hata screw moja, and that's Sony na LG. Japo matunzo ni muhimu pia.

Verdict: kama kweli mzigo upo, nenda na Sony au LG. Kama upo wa kawaida, nenda na Hisence au Samsung.
 
Mfano Juzi hapa nilikuwa natafuta TV...
Vigezo vyangu vilikuwa hivi...
  1. At least 55"
  2. Iwe na HDMI 2.1 120 Hz, maana nina mpango wa kununua PS5 hapo baadae
  3. Iwe na brightness ya kutosha na picture quality iridhishe
  4. Iwe na Dolby Vision
  5. Budget pia ni muhimu.
Options zilikuwa hizi:
  • Lg 55NANO86 (Niliitafuta sana na nimekuta sehemu chache, jamaa wanauza bei kubwa)
  • Samsung Q80B (Overpriced na pia haina dolby vision)
  • Hisense U8H, hii ni mini LED, nimeitafuta sana Dar sijapata ila yupo mdogo wake U7H ambayo ni qled na ndio niliyochukua.
So kama unatafuta TV weka vigezo unavyovitaka, then zama mitandaoni (Instagram maduka mengi ya kariakoo na posta wana pages zao).
 
Nimeupata mkuu
Nimekupata mkuu. Lakini hakuna TECNO inarekodi 8K simu zao za laki tano hadi nane zinarekodi 1080p na hii Phantom X2 Pro ndio simu yao bora kwa sasa na inarekodi 4K tu. Ila point yako uliyokuwa unajaribu kuiongelea nimeielewa ingawa kwa laki sita Hisense na Samsung huwezi fananisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…