Ni suala la muda tu ila Sauli na New Force mabasi yanayoelekea Tunduma na Mbeya yatamaliza watu

Madereva wamejaa kiburi, jeuri, kejeli, vijembe na nyodo kama vile wameolewa
Hapana kwasasa madereva hawakimbii kabisa hivi enzi zile Dar- Mbeya masaa 9 tu ungesemaje? Au Dar- Arusha masaa 7( Ngolika vs Buffalo), Mwanza-Dar masaa 13 tu (Ally's, Mombasa Raha, Colour star) au Kahama-Dar Masaa 11 na nusu au 12 ( Leina, Ally's ) 😂😂😂😂
 
Una akili ndogo Sana, kwasababu hazijapata ajali ndio zisinyoshewe kidole..


Mitanzania akili ziko matakoni
 
Wenye sifa nilizotaja siyo hao ulio quote ...ukiweza soma niliko quote
 
sauli ni gari bora. wanachonifurahisa wanafika mbeya mapema kwasababu hawasimami ovyo kama wengine njiani. acha kuwachafua.
 
Sikuhizi chuma mdomdo, hata ajali nyingi ni majeruhi, zenye vifo chache sana kama ile ya jana
 
Big Boys hao
 
Siku hizi Dar -Arusha unaingia saa tisa aisee ..

Mara kadhaa unatoka chuga unaenda kula Ugali dagaa DSM mchana kweupe.

Mbeye hapo to Arusha unakutana na Hood raha tupu
 
Si uishi tu mbeya mkuu....inaonyesha we ni mwenyeji kidogo
 
Kiukweli hizi bus sasa hivi hazikimbii, sema tu wako wako rough sana na overtake zisizo na maana za hovyo hovyo tu kuna bus moja ya kilimanjaro miaka ya 2005 kama kumbukumbu itakuwa sawa ilitoka ubungo saa 12 iliingia mbeya saa 7 dereva alipofika tu traffic wakambeba
 
Miaka ya 2012 hapo tulikuwa tunatoka njombe saa 06:00 Ubungo unafika saa 15:30 na bus la Budget.
 
Tanga Dar ni km 354 watu tunatumia masaa 6 Hadi Saba.
Korogwe Dar ni km 300 tunatumia masaa 5 Hadi 6.
Magari ni yale Yale, barabara zilezile Ila maadili tofauti.
Madereva wa ruti za Tanga wako makini Sana.
 
Mkuu wangu,dpk sio yutong n zhongtong climber,

Dwf sio benz ni scania gemilang,benz la sauli ni ile 226 dpc hana benzi nyingine.

Asante

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Siku hizi Dar -Arusha unaingia saa tisa aisee ..

Mara kadhaa unatoka chuga unaenda kula Ugali dagaa DSM mchana kweupe.

Mbeye hapo to Arusha unakutana na Hood raha tupu
Miaka Ile ilikuwa balaa sana mabasi yanakimbia sema uzuri malori na mizani vilikuwa vichache barabarani hata hizo speed 50 vibao vyake havikuwa vingi
 
Kwanini usipande magari mengine? Au ni lazima kupanda hizo gari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…