"Ni Tanzania tu utasikia biashara inakufa kwa sababu ina wateja wengi" Yerico Nyerere

Hivi jamaa ametumia maneno makali, mimi naona ametumia maneno sahihi kwa matendo yanayofanyika. Sijui lakini mambo yenu ya Tafsida.Kuna msemo wa Kizungu unasema call a spade a spade nafikiri ndicho alichofanya.
 
Mbona daladala hazifi au wao wamebakiwa na bei ya mafuta hio hio?
 
Do huyu aliua kabisa.
 
Hivi wale waimba nyimbo za kusifu na kutukuza za mama yao wapo?
 
Mkuu naona hapa tunazungumza lugha moja hasa kwenye hoja ya kutengeneza faida, Ili shirika lolote liwe sustainable financially lazima mapato yawe kibiashara na sio kutoa huduma tu, japo nimeshambuliwa mno humu lakini hoja Iko hapo. Tuna mashirika ambayo tunataka yalete faida na yawe sustainable kwa uendeshaji wa kutoa huduma. Hicho kitu haiwezekani.
 
Katiba Mpya bado hamuitaki? Ikiheshimiwa na kulindwa au ikijilinda kutokana na ukali wake, tutachagua na kuongozwa na tunayemtaka, tutapanga mpango ya nchi kwa pamoja na kwa utashi wa kila mtu, tutalinda Mali zetu. Miradi inakufa kwa kuwa, mtu mmoja ndio aliyeamua iwepo, mtu anayepingwa mpaka na wasaidizi wake wa karibu. Unategemea nini kitatokea kama si kuhujumiwa kwa hiyo miradi picha ya manufaa na iwepo wa wateja, ili tu kumtia aibu, kumdhalilisha aliyeiasisi?
 
Nchi inakosa national economic strategic planners kila mtu anakimbilia siasa tu.
Kwenye makaratasi tuna planners wazuri.
Tunakosa wasimamizi au waendeshaji hizo plans.
Tatizo letu lipo kwenye plan execution and how to maintain project life cycle.
Hii yote huchangiwa na uvivu, kukosa utamaduni wa kujifunza kila siku, nepotism, na wizi (ubadhirifu). Ubinafsi umetuzidi.
 
Hakuna biashara inayokufa sababu ya wateja wengi
 
Planners wetu wana plan au project plans ambazo ni unrealistic hazitekerezeki kwa mfano SGR project ya kutoka dar hadi Moro kuna mzigo gani au biashara gani watu kupanda waende Morogoro kufanya nini ?
 
Mwendokasi lazima ife kama wanajiibia wenyewe kwa nini isife hakuna watu Wazalendo hapo huo mradi upo ubia na Serikali kwa jina tu ukiwauliza wanapata kiasi gani hakuna jibu utapewa...
 
Nafikiri uko sahihi. Ila tunatofautiana kwenye sehemu moja,tofauti na wafanyabisahara wengine, tofauti na makampuni mengine, hawa jamaa wanapata favour kubwa sana(nimeziita compelling advantages). Sasa kutokana na hizo advantages wanatakiwa waendelee kuweka price zao favourable na affordable kwa watanzania. Hapa naongelea mtaji wa wateja. Kwa faida wanayopata wanatakiwa watoes huduma na wapate faida.
 
Hapo tungetoa hawa wabantu wezi wezi. Tutafute meneja, CFO, Chief engineer, Mtu wa nanunuzi. Chief Inspector wazungu wenye uzoefu. Watu wenye misimamo na utamaduni wa kusema no wakiona jambo halipo sawa au wanaingiliwa majukumu yao.
 
Hapo tungetoa hawa wabantu wezi wezi. Tutafute meneja, CFO, Chief engineer, Mtu wa nanunuzi. Chief Inspector wazungu wenye uzoefu. Watu wenye misimamo na utamaduni wa kusema no wakiona jambo halipo sawa au wanaingiliwa majukumu yao.
Kabisa, kibaya hata wakila, wakihujumu na kujilimbikizia mali. Ikijulikana papo pasipo wasiwasi na ushahidi tele , utasikia wamehamishwa idara au taasisi. Sasa unategemea nini kuhusu wengine.Tulitegema wale wanaokutwa na ubadhilifu wa mali za umma,kifungo miaka 20 na kutahifishwa mali zao zote ili iwe fundisho kwa wengine. China, Japani wameweza.
 
Nimekusikia mkuu, sihitaji kujibu maswali yako kwani hii ni free discussion, ninaweza kuwa niko sahihi au na wewe unaweza kuwa uko sahihi. tofauti yangu mimi na wewe ni suala la kupewa ruzuku na kutojiendesha kwa faida.

Sasa kama shirika limepewa mazingira wezeshi yote ili litengeneze faida kwa nini lipewe ruzuku. Hizo nchi za uropa, amerika kaskazini na kusini naomba uzitaje na ulete ushahidi hapa. Mimi nilishawahi kukaa maeneo kama hayo na walikuwa na well refurnished state of art public transport system kama mwendokasi and was runned by state. na sikuwahi kusikia wanapewa ruzuku , hivi waendeshaji wa yale mabasi ya uingereza au ile treni ya uingereza ya chini unafikiri wanapewa ruzuku na serikali au wao ndio wanacontribube faida kwa serikali. Tena bora ungeesema nchi za russia au cuba au scandinavian countries na si a pure capitalist countries. Ni kweli wana public transport na zinajiendesha kwa faida na hawapewi ruzuki labda wanapokula hasara kwa sababu ya justifiable reasons or unforeseen events ndipo serikali inawapatia addition /top up capital kustabilize shirika lisimame na kuendelea.

Swali langu la msingi ni je inamake sense serikali ya Tanzania kutoa subsidies kwa mashirika ya umma halafu baadae wanawaomba wawape gawio kutokana na faida wanayotengeneza, alifanya Magufuri na juzi tumemuona mama akifanya, mabillioni ya fedha yametolewa kwa serikali kama gawio kutokana na faida ya mashirika ya umma;leo tunaambiwa hayatakiwa kutengeneza faida,does it make sense; to summarize, kwa nini wawape gawio kama serikali inajua hawatakiwi kutengeneza faida; zaidi kama wameomba gawio la faida, kwa nini tena wawarudishie tena fedha hizo kwa nia ya subsidies au ruzuku. Ukiniambia initial running cost hapo nakubali kwani ndio shirika linaanza. Je jiulize mashirka ya umma ambayo serikali imeingia shea na firms au wwatu wengine, NMB, AIRTEL etc unaweza sema hawatakiwi kutengeneza faida, mbona tunatajiwa matrillioni ya faida kutoka NMB ni kwa sababu ya uongozi mzuri.. Tatizo linalotokea ni kutokana na wizi, usimamizi mbaya wa mashirika haya, yabaishia kula hasara kwa hiyo serikali inabidi iendelee kutop up running capital ili yasije kusimama na sio subsidies.


Ila unaweza ukawa na hoja ingawa bado sijaielewa mkuu. Kwa sababu hii ni free forum na discussion no response or proposition is wrong let agree on disagreement ambacho ni kitu chema kwenye critical discussion kama hizi ambazo hazina majibu sahihi kwani nyingi ni complex na zina attributes (visababishi vingi).

Ili kufafanua neno attributes beyond uwezo/reach ya viongozi wa mashirika haya nitatoa mifano. Kwanza tunaambiwa kuna kipindi serikali inakopa almost faida yote na sehemu ya mtaji kutoka hifadhi za jamii na mashirika ya umma kama NSSF, NHIF na sijui kama unafahamu sakata la MSD ambapo serikali iliwaagiza wapeleke consignment za madawa na vifaa tiba kwenye mahospitali ya serikali yenye thamani ya mabillioni ya shiringi kwa ahadi watawalipa na hawakuwalipa, MSD ikawa imekaribia kukauka, mkuu wake alipowakumbusha kwamba shirika linakalipia kufa tokana na deni hilo akaondolewa na wakamuweka mwingine na kuinject funds kidogo la deni lao ili shirika lisije kufa. Kwa hiyo tunawezaa tukawa tunashutumiana hapa mimi na wewe kumbe sababu iko juu ya uwezo wa uongozi wa shirika; it is the governing system itself. Nyakati za chaguzi, nyakati za majanga, nyakati serikali inakosa mapato kulipa mishahara ndipo huwaga wanaborrow.
 
Ongezea na TANESCO ......
Hayo ni ya kawaida ktk jamii ambayo wanaomba mkopo wa maendeleo na wenye masharti; wakipewa tu wanamega sehemu na kufanya sherehe ya kupata mkopo.
Kila ansyepata nafasi ya uongozi anawaza na kuzunguka kokote kunakomhusu , akifhaniwa anafuatilia maendeleo, kumbe anapotos madili yake. Wengine wanapewa escot kabisa!
 
Yaani you have nailed it, baadhi ya mashirika wanaanzisha project kubwa zisizo na faida kwa kukopa matrillioni, huku wakijua while implementing hiyo project wao watatumia huo mwanya kupiga mabilioni kwenye estimate za cost, kwenye procurement, kwenye tendering na 10% . Yaani ni taabu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…